Ronaldo vs YamalRonaldo vs Yamal
  • Portugal vs Spain fainali UEFA Nations League 8/6/2025, ni mchezo unaotarajiwa kupigwa dimba la Allianz Arena, Munich nchini Ujerumani.
  • Hii ni vita ya rekodi kati ya mkongwe, Cristiano Ronaldo dhidi ya kinda wamoto kwa sasa, Lamine Yamal.
  • Takwimu zinaonesha kuwa mechi 7 kati ya 9 zilizopita timu hizo zilipokutana zimeshuhudia timu zote mbili zikifunga mabao.

Tarajia vikapu vya magoli kujaa Jumapili kwenye mechi ya Portugal vs Spain fainali UEFA Nations League 8/6/2025, mchezo ambao unatarajiwa kupigwa kwenye dimba la Allianz Arena, Munich nchini Ujerumani na kushuhudia vita ya rekodi ya mkongwe, Cristiano Ronaldo dhidi ya kinda, Lamine Yamal.

Portugal vs Spain fainali UEFA Nations League 8/6/2025 mbungi kupigwa Ujerumani

DCIM MEDIADJI JPG
Dimba la Allianz Arena

Fainali ya mashindano ya UEFA Nations League msimu wa 2024/25 inakaribia kwa kishindo huku timu mbili Portugal na Spain zikikabiliana kwenye uwanja wa Allianz Arena, Munich, tarehe 8 Juni 2025. Timu hizi zote mbili ni kati ya washindi watatu waliopita wa kombe hili. Portugal mwaka 2019 na Spain 2023.

SOMA HII PIA: EURO 2024, Yamal amfunika Mbappe, Uhispani wakiitoa Ufaransa na kutinga Fainali

Portugal na nguvu ya Kikosi cha kocha Martínez

Portugal imefika fainali kwa kishindo baada ya kuiondoa Ujerumani kwa ushindi wa 2-1 kwenye nusu fainali. Mchezo huo ulianza kwa kasi ya wastani, lakini Ureno walijibu kwa nguvu baada ya kufungwa dakika ya 48, wakisawazisha dakika ya 63 na kuongeza bao la pili dakika tano baadaye.

Huu ulikuwa ushindi muhimu unaoongeza rekodi ya kutofungwa ndani ya dakika 90 katika mechi 9 kati ya 10 zilizopita. Katika mashindano haya ya Nations League, Portugal imepata ushindi dhidi ya Croatia, Scotland, Poland, na Denmark. Sare dhidi ya Croatia na Scotland, na kufungwa kwa penalti na Ufaransa katika Euro.

Spain na mashambulizi yasiyozuilika

 Portugal vs Spain fainali UEFA Nations League 8/6/2025
Yamal

Spain imefuzu Fianknali kwa njia ya kusisimua zaidi, mara baada ya kuiangusha Ufaransa kwa kuibamiza mabao 5-4 katika mechi ya nusu fainali iliyokuwa ya kufurahisha. Katika mchezo huo waliongoza 2-0 hadi mapumziko, wakafunga mabao mawili ya haraka dakika ya 54 na 55.

Japokuwa walifungwa kupitia penalti dakika ya 59, waliongeza bao la tano dakika ya 67 kabla ya kuruhusu mabao matatu ya Ufaransa katika dakika 14 za mwisho. Ushindi huo unaifanya Uhispania kuwa haijafungwa katika mechi 19 mfululizo, ikijumuisha ushindi wao wa Euro 2024 dhidi ya England.

SOMA HII PIA: Barcelona vs Real Madrid 26/4/2025, uso kwa uso fainali Copa Del Rey

 Portugal vs Spain fainali UEFA Nations League 8/6/2025 rekodi za H2H

Takwimu zinaonesha kuwa mechi 7 kati ya 9 zilizopita timu hizo zilipokutana zimeshuhudia timu zote mbili zikifunga mabao. Lakini, Portugal bado haijafanikiwa kuifunga Uhispania katika mechi 6 zilizopita kati ya timu hizo ambapo mechi 4 kati ya 5 zikimalizika kwa sare.

Spain pia katika mechi 4 zilizopita, wamefanikiwa kupata wastani wa zaidi ya magoli 3.5 na timu zote kufunga, jambo linaloashiria mchezo mwingine wa kushambulia.

Nyota wa Kuchungwa kuelekea mchezo huu

Cristiano
Cristiano

Kwa upande wa Portugal, Cristiano Ronaldo bado ni muhimu licha ya kuwa na umri wa jioni, ambapo akisaidiwa na wachezaji chipukizi kama Francisco Conceição, aliyeonesha ubora kwa mashuti matatu kwenye lango dhidi ya Ujerumani. Kwa Spain, Lamine Yamal ni nyota anayetikisa duniani.

Tathmini ya Vikosi

Portugal huenda ikafanya mabadiliko mawili pekee, ambapo Conceição na Vitinha wanaweza kuanza badala ya Trincão na Rúben Neves. Kikosi kinachotarajiwa ni: Portugal (3-4-3): Diogo Costa, Rúben Dias, Gonçalo Inácio, Nuno Mendes; Bernardo Silva, Bruno Fernandes, João Neves, Vitinha; Cristiano Ronaldo, Conceição, Pedro Neto.

Spain pia haitegemewi kufanya mabadiliko mengi, ingawa Dani Olmo na Fabian Ruiz wanaweza kupewa nafasi. Kikosi chao kinatarajiwa kuwa Spain (4-2-3-1): Unai Simón, Pedro Porro, Dean Huijsen, Robin Le Normand, Marc Cucurella; Martín Zubimendi, Mikel Merino; Pedri, Lamine Yamal, Nicolás Williams; Mikel Oyarzabal.

Matarajio ya Mchezo

Kwa rekodi ya timu zote mbili, mchezo unatarajiwa kuwa wa kasi na wenye magoli mengi. Portugal inategemea nidhamu ya Martinez na mbinu zake za kushambulia kwa kasi kupitia 3-4-3, huku Uhispania ikitawala mpira kwa mfumo wa 4-2-3-1.

Takwimu zinaonesha wastani wa kona nne kwa kila timu kwenye mechi zao za hivi karibuni, hali inayothibitisha nia ya kushambulia. Portugal imekuwa na wastani wa pasi 400+ kwa mechi, huku Spain ikibaki na pasi nyingi sahihi na umiliki mkubwa wa mpira.

Hitimisho utabiri wa Mchezo

Kwa kuzingatia uwezo wa kushambulia wa Spain ambao ulioonekana dhidi ya Ufaransa, na uthabiti wa Portugal dhidi ya timu kubwa kama Ujerumani, utabiri bora ni matokeo ya sare au Spain kushinda, na timu zote kufunga ni matokeo yanayotarajiwa.

Sare ya mabao 2-2 inaweza kuwa matokeo ya dakika 90, ikisababisha muda wa ziada na hata penalti. Hii ni fainali inayosubiriwa kwa hamu kubwa timu mbili zenye vipaji, historia, na nia ya kushinda taji kubwa barani Ulaya.

Utabiri wa Mwisho: Spain kuibuka mabingwa kupitia penalti au ushindi mwembamba baada ya muda wa ziada.

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.