Sowah RedSowah Red
  • Jonathan Sowah saini mpya Simba SC kuelekea msimu wa 2025/26 ameahidi makubwa msimu ujao.
  • Simba SC ipo kambini nchini Misri chini ya Kocha Mkuu, Fadlu Davids ilipishana na mataji 2024/25 hivyo ina hasira kuelekea msimu mpya.
  • Ahmed Ally asimulia namna walivyomfuatilia nyota mpya katika kikosi hicho ambaye amezaliwa kucheza maisha yake yote.

Jonathan Sowah mshambuliaji mpya wa Simba SC amesema mashabiki watafurahi. Ahadi hiyo ni maalumu kuelekea msimu mpya wa 2025/26 unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa. Simba SC imeweka kambi nchini Misri.

Paisha kindege uvune mamilioni sasa hivi

Ni muda wa kupaisha kindege ushinde mamilioni sasa hivi na SportPesa. Ni rahisi sana kuwa milionea. Cheza Aviator upate mgao wako wa uhakika.

Aviator banner

Sowah na Simba SC

Sowah Mnyama
Sowah Jonathan mshambuliaji mpya wa Simba SC. Source: Simba SC.

Soma hii: Jonathan Sowah rasmi asaini Simba SC: Ahmed atangaza mashine 7 mpya  tetesi usajili Ligi Kuu NBC 2025/26

Sowah alitambulishwa ndani ya kikosi cha Simba SC akitokea Singida Black Stars. Msimu wa 2024/25 alifunga jumla ya magoli 13. Katika mabao hayo aliwafunga watani wa jadi Yanga SC kwenye mchezo wa ligi uliochezwa Uwanja wa KMC Complex.

Mbali na Sowah kuwafunga Yanga SC kwenye ligi, aliwafunga na Simba SC. Katika mchezo wa hatua ya nusu fainali Kombe la CRDB hapo Simba SC waliadhibiwa. Hivyo ni mchezaji ambaye anafurahia kufunga.

Sowah na sakata lake Yanga SC

Sowah Misri
Sowah akiwa kambini na Simba SC Misri. Source: Simba SC.

Soma hii: Usajili mpya Yanga balaa! Sowah, Bada, Chikola kwenye Yanga mpya

Awali Sowah alikuwa anatajwa kuwa katika rada za Yanga SC. Mshambuliaji huyo aliwahi kubainisha kuwa anaipenda Yanga SC. Mbali na hilo aliweka wazi kuwa Rais wa Yanga SC, Injinia Hersi Said ni baba kwake.

Kwenye tetesi timu zote mbili zilikuwa zinatajwa kuwania saini yake. Mwisho alitambulishwa ndani ya kikosi cha Simba SC akiwa ni mshambuliaji mpya. Agosti Mosi 2025 mshambuliaji huyo alitambulishwa rasmi kuwa ni mnyama.

Sowah katika mchezo wa fainali ya CRDB dhidi ya Yanga SC alionyeshwa kadi nyekundu. Katika mchezo huo mkubwa Sowah alionyeshwa kadi mbili za njano. Hivyo hakumaliza mchezo na Singida Black Stars ilipishana na kombe hilo ambalo lipo mikononi mwa Yanga SC.

Ahadi ya Sowah ndani ya Simba SC

Mshambuliaji huyo amebainisha kuwa watafanya kazi kubwa msimu ujao. Kutokana na Simba SC kukosa mataji wanaamini kuna jambo kubwa litatokea. Aliongeza kuwa mashabiki watafurahi wakienda uwanjani na hata wale ambao watakuwa nyumbani.

“Mimi naitwa Jonathan Sowah ni Simba mweusi. Ninapenda kuwaambia mashabiki wa Simba SC kuwa watafurahi. Kwa kila shabiki ambaye atakuja uwanjani na yule ambaye atakuwa nyumbani hakika atafurahi.

“Kuna mengi ambayo tunaamini tutafanya. Ushirikiano mkubwa kwa wachezaji na benchi la ufundi. Hakika kila mmoja atafurahi, mashabiki tuzidi kuwa pamoja.”

Kambini Misri kazi ipo

Simba SC imeweka kambi nchini Misri. Chini ya Kocha Mkuu, Fadlu Davids wachezaji hao wanaendelea na maandalizi. Miongoni mwa wachezaji ni Leonel Ateba, Jean Ahoua, Ellie Mpanzu.

Kazi ambayo ipo kwa wachezaji hao ni kuwa tayari kwa msimu mpya. Mipango yote inaratibiwa na benchi la ufundi. Mazingira ya Misri yanaonekana kuwa ni rafiki kwa kila mchezaji.

Ahmed Ally ampa maua yake nyota mpya Morice

Morice
Morice ingizo jipya Simba SC 2025/26. Source: Simba SC.

Soma hii: Simba SC yasajili mashine hizi mbili kwa mpigo, kuelekea Ligi Kuu ya NBC 2025/26

Kwenye orodha ya wachezaji waliopo kambini yupo Morice Abraham. Huyu ni mchezaji mpya ndani ya kikosi cha Simba SC. Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC Ahmed Ally amesema Abraham amezaliwa kucheza mpira.

“Morice Abraham unapozungumzia pure talent, yaani mchezaji halisi wa mpira wa miguu unamzungumzia Morice Abraham. Morice ni binadamu aliyezaliwa kucheza mpira tu. Kuna binadamu ambaye anazaliwa anakuwa na shughuli nyingi, leo anauza ubuyu, leo analima shamba, kesho anapiga picha.

“Ila Morice Abraham amezaliwa kwa ajili ya mpira tu. Maisha yake ni mpira tu. Amezaliwa katika ulimwengu wa wazi, tumemuona Morice akipita katika Academy ya Alliance, timu za vijana, timu ya taifa ya Tanzania anakwenda Gabon.

Ahmed Ally
Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari Simba SC. Source: Simba SC.

Soma hii: Mpanzu atua kwa kishindo Misri, Simba watoa tamko zito

“Anatoka hapo anakwenda nje ya nchi Ulaya anakwenda anafanya balaa kubwa huko sisi tulikuwa tunamuangalia tu. Na tumepata mtu haswa, Morice ana uwezo mkubwa wa kumiliki mpira. Unajua mpira haumilikiwi kwenye miguu peke yake bali katika akili.

“Kipindi pekee ambacho Morice hajacheza mpira ni kipindi kile ambacho hajazaliwa. Ila baada ya kuzaliwa alianza kucheza mpira. Maisha yake ni mpira tu.

“Morice ana uwezo wa kucheza kushoto ana uwezo wa kucheza kulia. Huwezi kuchukua mpira kwa Morice Abraham kirahisi. Ana akili kwelikweli huyo ndo Morice.

“Morice ana akili katika umiliki wa mpira. Tuliangalia uwezo wake na kupata nafasi ya kucheza Serbia tukamwambia kijana una hitajika kwenye taifa kubwa la Simba SC. Tupo naye ndani ya Simba SC kwa sasa,”.

Hitimisho

Simba SC itawakilisha Tanzania kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika msimu wa 2025/26. Katika msimu wa 2024/25 ilikuwa kwenye Kombe la Shirikisho Afrika. Huku iliishia kuwa mshindi wa pili na bingwa alikuwa ni RS Berkane ya Morocco.

image
Share this: