Mashabiki StarsMashabiki Stars
  • CHAN 2024 imepamba moto kwa kila timu kusaka ushindi hatua za makundi ambapo ni Kenya, Tanzania na Uganda ni wenyeji wa mashindano haya makubwa.
  • Tanzania mechi mbili mfululizo imepata ushindi ikiwa inaongoza kundi B na pointi zake sita.
  • Hemed Suleman Kocha Mkuu wa Tanzania ameandika rekodi nzuri katika dakika 450 za ushindani.

Timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars Agosti 9 2025 inatarajiwa kucheza mchezo wa  Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN 2024). Utakuwa ni mchezo wa tatu kwa Tanzania. Ni Tanzania vs Madagascar CHAN 2024 Uwanja wa Mkapa.

Shinda mamilioni ukipaisha Kindege na SportPesa

Ni muda wakushinda mamilioni sasa hivi. Cheza Aviator uvune mkwanja. Rubani makini anakutana na mgao wake kila siku.

Aviator banner

Mwendo wa Tanzania CHAN 2024

Nado Stars
Idd Nado kiungo wa timu ya Tanzania kwenye mchezo dhidi ya Mauritania. Source: TFF.

Soma hii: Mauritania 0-1 Tanzania CHAN 2024

Kwenye mechi mbili zilizopita Tanzania ilipata ushindi kwa kuvuna pointi sita muhimu. Inatarajiwa kukutana na upinzani mkubwa kutoka kwa Madagascar. Timu hizi zote mbili zipo Kundi B ambalo vinara ni Tanzania.

Hemed Suleman Kocha Mkuu wa Tanzania amesema kuwa kila mchezo ni muhimu. Kocha huyo alibainisha kuwa hakuna timu ambayo haifikirii kupata ushindi. Licha ya yote hayo kocha huyo aliweka wazi kuwa ambao wanahitaji ni ushindi.

“Tuna kazi kubwa kwenye mechi zetu ambazo tunacheza. Maandalizi yapo vizuri hasa ukizingatia kwamba tulikuwa na kambi imara. Licha ya kwamba tumepata ushindi kwenye mechi zetu zilizopita bado tuna kazi kwa ajili ya mchezo wetu ujao,”.

Rekodi za kocha wa Tanzania

Kocha wa timu ya taifa ya Tanzania, Hemed Suleman amekuwa na rekodi nzuri. Katika mechi tano ambazo alikuwa benchi alishinda zote. Hakuna sare katika mechi hizo zilizopita.

Ilikuwa Eswatini 1-2 Tanzania, mchezo huu ulichezwa Juni 11 2025. Tanzania 1-0 Uganda ulichezwa Julai 22 2025. Tanzania 2-1 Senegal ulichezwa Julai 27 2025.

Tanzania 2-0 Burkina Faso ulichezwa Agosti 2 2025. Huu ulikuwa ni mchezo wa ufunguzi wa CHAN 2024 Uwanja wa Mkapa. Mauritania 0-1 Tanzania, Agosti 6 2025.

Katika mechi tano, safu ya ushambuliaji ya Tanzania imefunga mabao 8. Ukuta wa Tanzania umeruhusu mabao manne. Kwenye dakika 450 Suleman mipango yake ilijibu kwa wachezaji kutimiza majukumu kwa umakini.

Safu ya ushambuliaji ina wastani wakufunga bao moja kila baada ya dakika 56. Safu ya ulinzi ina wastani wakufungwa bao moja kila baada ya dakika 112.

Dakika 180 za ushindi kwa timu ya taifa ya Tanzania

Feisal na Mo Hussein
Feisal na Mo Hussein wachezaji wa timu ya taifa ya Tanzania.

Soma hii: Tanzania vs Burkina Faso na Kenya vs DR Congo: Wenyeji waanza kwa kishindo CHAN 2024.

Kwenye mechi mbili za CHAN ambazo ni dakika 180 iliambulia ushindi. Imekusanya jumla ya pointi sita. Timu hiyo imekuwa na mwendelezo mzuri kupata matokeo kwenye mechi za ushindani katika hatua ya makundi.

Safu ya ulinzi ya Tanzania inaongozwa na beki Dickson Job. Beki huyo ameweka wazi kuwa watazidi kupambana kuwa imara. Aidha amewaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi kwenye mechi zote.

“Tuna malengo yakufanya vizuri kwenye mechi ambazo tunacheza. Tuliweka wazi tangu awali. Tunatambua kazi ni kubwa tunapambana, mashabiki waendelee kujotokeza kwenye mechi zetu.”

Safu ya ushambuliaji ya timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars imefunga jumla ya mabao matatu. Katika mabao hayo mawili yamefungwa na mabeki. Shomari Kapombe na Mohamed Hussen.

Bao moja la Tanzania limefungwa na kiungo Sopu. Kiungo huyo alifunga bao kwa mkwaju wa penati mchezo dhidi ya Burkina Faso. Ni Clement Mzize alisababisha penati hiyo baada ya kuchezewa faulo ndani ya 18.

Tanzania inaongoza Kundi B

Shomari Kapombe (-)
Shomari Kapombe nyota wa timu ya taifa ya Tanzania. Source: TFF

Soma hii: Tanzania 2-1 Senegal CECAFA 2025 Arusha

Timu ya taifa ya Tanzania inaongoza Kundi B na pointi 6, Burkina Faso iafuata nafasi ya pili ina pointi 3. Madagascar na Mauritania hawa kila timu ina pointi moja.

Jamhuri ya Kati haijakusanya pointi na mchezo ujao itacheza na Mauritania. Agosti 9 2025 Tanzania itakuwa uwanjani kusaka pointi dhidi ya Madagascar. Vinara hao wa Kundi watacheza mchezo huo saa 2:00 usiku Uwanja wa Mkapa.

Wachezaji wenye tuzo kwenye mechi za CHAN 2024

Kwenye mechi mbili mfululizo, wachezaji wa Tanzania wametwaa tuzo ya mchezaji bora. Haya ni mashindano makubwa hivyo tuzo zina hadhi kubwa. Viungo wawili walitwaa tuzo hizo.

Katika Mchezo wa kwanza wa ufunguzi wa CHAN kwa Tanzania Feisal Salum alitwaa tuzo ya mchezaji bora. Agosti 2 2025 Tanzania 2-0 Burkina Faso. Pointi tatu zilikuwa mali ya Tanzania.

Kiungo Feisal alisema kuwa ni furaha kutwaa tuzo hiyo. Aliongeza kuwa haikuwa rahisi kutokana na ushindani uliopo. Aliongeza kwa kuwaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi uwanjani.

“Ninafurahi kutwaa tuzo. Haikuwa rahisi kwani ushindani ni mkubwa. Shukrani kwa mashabiki na ninaomba waendelee kujitokeza kwenye mechi zetu,”.

 Kwenye mchezo wa pili ni Mudathir Yahya alitwaa tuzo hiyo. Ilikuwa ni Agosti 6 2025. Baada ya dakika 90 ilikuwa Mauritania 0-1 Tanzania.

Hitimisho

Timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars inahitaji ushindi kwenye mchezo ujao. Wachezaji wamekuwa kwenye mwendelezo mzuri katika kutengeneza nafasi. Benchi la ufundi lina kazi kuboresha makosa ambaye yalitokea kwenye mechi mbili hasa katika umaliziaji.

image

Share this: