Simba Sc Vs Stellenbosch FCSimba Sc Vs Stellenbosch FC

RS Berkane Simba SC CS Constantine Stellenbosch FCThe ------- #TotalEnergiesCAFCC semi-finalists have their eyes set on victory- Who will reach the finals
Timu nne zilizofuzu Nusu Fainali
  • Hii ni mara ya kwanza kwa Simba kukutana na Stellenbosch, pia ni mara ya kwanza kwa mchezo mkubwa wa mashindano yaliyo chini ya Shirikisho la soka Afrika ulio katika hatua kubwa kupigwa visiwani Zanzibar.
  • Timu zote mbili zimefuzu Nusu Fainali kwa mara ya kwanza, timu zote mbili zimewahi kuwavua ubingwa mabingwa watetezi.
  • Simba wanakamatia nafasi ya pili kwenye Ligi Kuu Bara na pointi zao 57 katika michezo 22, Stellenbosch wanashika nafasi ya tatu ligi Kuu Afrika Kusini na pointi zao 38 katika michezo 23

Wawakilishi pekee wa Tanzania katika mashindano ya kimataifa Simba ambao wanashiriki Kombe la Shirikisho Afrika keshokutwa Jumapili watashuka Uwanjani kuvaana na wageni wao Stellenbosch katika mchezo wa Nusu Fainali ya kwanza ya mashindano hayo huku mipango mizito ikitarajiwa kufanyika.

Simba Vs Stellenbosch ni miongoni mwa michezo ambayo inasubiriwa kwa hamu kubwa na unatarajiwa kupigwa siku ya Jumapili kuanzia saa 10 jioni ambapo tayari wenyeji wa mchezo huo Simba tayari wamewasili visiwani Zanzibar.

Ikumbukwe Simba ni miongoni mwa timu nne ambazo zimefuzu Nusu Fainali ambapo timu tatu zilizosalia ni pamoja na Stellenbosch, RS Berkane na Constantine.

SIMBA SC YAPIGA TIZI LA KUFA MTU ZANZIBAR

Safari ya kwenda kutwaa ubingwa wa Kombe la Shirikisho Afrika itaendelea Jumapili hii- #HatuishiiHapa #TunaitakaFainali #WenyeNchi #NguvuMoja (-)
Kikosi kikiwa mazoezini Zanzibar; Source Simba

Kikosi kimeendelea na mazoezi katika Uwanja wa Amaan Zanzibar kujiandaa na mchezo wa kwanza wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Stellenbosch utakaopigwa Jumapili Aprili 20, saa 10 jioni. Ikumbukwe kikosi cha wenyeji wa mchezo kimewasili Zanzibar Aprili 16 tayari kwa mchezo huo, ambao malengo yao ni kupata ushindi mzuri nyumbani ili kujiweka kwenye hali nzuri katika mechi ya marudiano ugenini.

Wachezaji wote wameshiriki mazoezi hayo kikamilifu na morali zao zipo juu na wanaonekana wapo tayari ajili ya kuipambania timu kufikia malengo waliyojiwekea. Kikosi hiko kinaendelea na programu ya mazoezi kesho kabla ya kushuka dimbani siku ya Jumapili.

SEMAJI LA SIMBA, AHMED LAWAOMBA WAZANZIBAR KUIPELEKA TIMU FAINALI

------------------------------------------------n
Ahmed Ally; Source Simba

Meneja Habari na Mawasiliano wa timu hiyo, Ahmed Ally amewaomba mashabiki hasa kutoka Visiwani Zanzibar kuhakikisha wanapambana na kuiwezesha timu kutinga fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa kuitoa Stellenbosch ya Afrika Kusini.

Ahmed amesema ni zamu ya watu kutoka Zanzibar kuweka historia ya kuipeleka timu kutinga fainali ya michuano hii ambayo safari wamedhamiria kutwaa taji lenyewe.

“Niwaombe watu wa Zanzibar na hasa mashabiki wafanye kila kinachowezekana kuipeleka Simba fainali. Nilisema kila kizazi na historia yake, hii imekuja wakati muafaka na sisi kuandika historia ya kuipeleka Simba fainali. Tufanye kila kinachowezekana Mnyama kwenda fainali,” amesema Ahmed.

Ahmed ameongeza kuwa: “wapinzani wetu Stellenbosch sio timu dhaifu, hadi inafika hatua hii inaonyesha ni timu ambayo imejiandaa. Wanasimba wote tulijiandaa kucheza na Zamalek lakini Stellenbosch akammaliza pale pale nyumbani kwake, hajamtoa Zamalek kwa bahati mbaya.

“Ni kweli Stellenbosch ni timu ngeni lakini ina wachezaji wenye ubora mkubwa na wana kocha mkubwa. Tuna kazi kubwa kwelikweli kuhakikisha tunamthibiti, tunamfunga ili tukienda kwenye mechi ya ugenini ni iyenaiyena Mnyama hadi fainali,” amesema Ahmed.

SIMBA KUCHEZA NUSU FAINALI NYINGINE NA MBEYA CITY

Mutale- Ngoma na Ateba
Mutale, Ngoma na Ateba wakishangilia bao

Ukiachana na Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika, Simba pia wamefanikiwa kutinga nusu fainali ya michuano ya CRDB Federation Cup baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Mbeya City katika mchezo uliopigwa Uwanja wa KMC Complex.

MCHEZO ULIKUWAJE?

Unahisi jambo gani walikuwa wanaongea hapa #WenyeNchi #NguvuMoja
Mastaa wa Simba

Wenyeji walianza mchezo huo kwa kasi huku tukifika zaidi langoni mwa City ambao muda mwingi walikuwa nyuma huku walifanya mashambulizi machache ya kushtukiza. Mudathir Said aliipatia Mbeya City bao la kwanza dakika ya 22 kwa shuti kali la mguu wa kushoto lililomshinda mlinda mlango, Ally Salim kufuatia walinzi wake kujichanganya.

Kiungo Fabrice Ngoma aliisawazishia bao hilo dakika ya 24 kwa kichwa baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Ladaki Chasambi. Leonel Ateba aliipatia bao la pili dakika ya 29 kwa kichwa baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Ngoma.

Joshua Mutale aliipatia bao la tatu dakika ya 43 baada ya kupokea pasi ya Ngoma na kuwapiga chenga walinzi wa City na kupiga shuti la chini chini lililomshinda mlinda mlango Hashim.

Kipindi cha pili kasi ya mchezo ilipungua ingawa wenyeji waliendelea kumiliki sehemu kubwa na kutengeneza nafasi kadhaa lakini hawakuweza kuzitumia.

NI SIMBA SC Vs SINGIDA BLACK STARS NUSU FAINALI

Nusu Fainali CRDB Bank Federation
Nusu Fainali CRDB Bank Federation

Ushindi huu umewafanya kukutana na mshindi mchezo kati ya Singida Black Stars na Kagera Sugar katika mchezo wa nusu fainali, ambapo tayari Singida Black Stars wamefuzu.

KIKOSI SIMBA KILICHOIVUSHA TIMU ROBO FAINALI FA

Ally, Duchu, Nouma, Karaboue (Balua 54′), Hamza (Okajepha 61′), Ngoma (Kapombe 77′) Chasambi, Fernandez, Ateba (Mukwala 77′), Awesu (Adolf 87′) Mutale

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.