Rushine De Reuck rasmi asaini na kutambulishwa Simba SCJonathan Sowah Simba
  • Jonathan Sowah rasmi asaini Simba SC, Mabosi Simba wacharuka wasambaa Afrika kusaka vyuma.
  • Sowah msimu uliopita akiwa na Singida aliifungia mabao 13 na atavaa jezi ya Simba msimu ujao.
  • Meneja wa Habari na mawasiliano Simba SC, Ahmed Ally amefichua kuwa tayari wameshusha mashine 7 mpya.

Baada ya kimya cha muda hatimaye msimbazi kumechangamka kupitia usajili. Jonathan Sowah rasmi asaini Simba SC, huku Meneja wa Habari wa kikosi cha timu hiyo, Ahmed Ally akitangaza rasmi kumalizana na nyota saba wapya. Hii ni katika kuelekea msimu wa 2025/26.

Shinda mamilioni na ‘Kindege’ cha SportPesa

Endelea kuhabarika na makala hii, huku pia ukicheza na kushinda mamilioni kupitia mchezo wa aviator maarufu kama Kindege kutoka Kampuni bora ya michezo ya kubashiri ya SportPesa kwa kubonyeza picha hii chini.

SEO Banner LV

Dili  la Sowah na Simba

Taarifa kutoka vyanzo vya kuaminika vimethibitisha kuwa Simba imemalizana na straika wa Singida Black Stars, Jonathan Sowah. Imeelezwa Sowah anakuja kuchukua nafasi ya straika Lionel Ateba ambaye anatarajiwa kutimkia uarabuni. Imethibitishwa kuwa Simba walikamilisha dili la Sowah usiku wa kuamkia leo Jumatano.

“Usiku wa Jumanne Simba SC wamekamilisha usajili wa mshambuliaji wa Singida Black Stars, Jonathan Sowah. Usajili umetokea baada ya Sowah kuridhishwa na mpango wa Simba SC. Ni rasmi sasa, Sowah aliyemaliza msimu na mabao 13 atavaa jezi ya Simba msimu ujao,” ilieleza taarifa hiyo.

Semaji Ahmed atangaza mashine 7 mpya

Ahmed Ally
Ahmed Ally

Kufuatia taarifa za mipango ya Simba kwenye dirisha hili la usajili. Meneja wa Habari na mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally ameweka wazi kuwa Simba SC imepania kufanya usajili mkubwa kuelekea msimu wa 2025/26. Ikumbukwe kwamba timu hiyo msimu wa 2024/25 ilikosa mataji yote jambo linaloelezwa kuwapa hasira kubwa.

“Kwa sasa viongozi wa Simba SC wametapakaa kila kona kwenye nchi za Afrika. Hii ni katika kuhakikisha wanamalizia usajili wa wachezaji wapya. Huu ni usajili mwingine wa kishindo na sitaongea sana safari hii nitaacha watu waone wenyewe. Tumekamilisha usajili wa wachezaji saba na bado tunaendelea,” amesema Ahmed.

SOMA HII SASA: Mohamed Hussein aaga rasmi Simba atajwa kusaini Yanga, mabosi Msimbazi wamgeukia Kamagate Tetesi usajili Ligi Kuu NBC 2025/26

Wachezaji walioachwa na Simba SC mpaka sasa

Kama sehemu ya maboresho ya kikosi chao Simba tayari wameachana na kundi kubwa la wachezaji. Baadhi ya mastaa ambao wamepewa ‘thankyou’ na Simba ni Pamoja na Aishi Manula aliyeenda Azam FC. Wengine ni Pamoja na Omary Omary ambaye amepelekwa kwa mkopo Mashujaa FC.

Wengine ni, Fabrince Ngoma mkataba wake umeisha. Kelvin Kijili ametimkia Singida Black Stars. Valente Nouma naye ameachwa, nahodha Mohammed Hussein amemaliza mkataba na listi hii inatarajiwa kuongezeka. Hii ni pale Simba itakapoanza rasmi kutangaza mastaa wake.

Tshabalala aaga baada ya miaka 11

Katika hali ambayo haikutarajiwa na wengi nahodha wa Simba, Mohamed Hussein aliipa ‘Thankyou’ Simba. Nyota huyo ambaye amehudumu Simba kwa miaka 11 anatajwa kuwa kwenye rada za Yanga. Taarifa isiyo rasmi imethibitisha kuwa Tshabalala amesaini miaka 2 ndani ya Yanga.

Barua ya Tshabalala kwa Simba (Sababu 3 kubwa)

Baada ya ‘Tshabalala’ na Conte Yanga SC yashusha straika Boyeli
Tshabalala

“Takribani miaka 11 ya Furaha, huzuni, Shangwe, vifijo, nderemo na masikitiko ndani ya Mbuga. Kwa uaminifu mkubwa, weledi wa kiwango cha juu, Kuvuja jasho kuipigania nembo ya klabu ndio ulikuwa msingi na malengo. Wahenga walisema kila lenye mwanzo halikosi mwisho na leo nawaaga rasmi.

“Haya ni maamuzi yaliyolenga Maendeleo yangu binafsi, maslahi yangu binafsi na weledi wangu uliotukuka. Nichukue fursa hii kuwashukuru viongozi, benchi la ufundi na ‘operation staffs’ wote wa klabu ya Simba SC kwa kipindi chote cha kuhudumu ndani ya klabu.

“Kipekee niwashukuru mashabiki kwa kuwa nami kipindi chote, kama mnavyonipenda na mimi nawapenda pia na nina imani mtaendelea kuniunga mkono. Naishukuru Management Yangu ikiongozwa na Carlos Carlos kwa ushirikiano mkubwa wa kipindi chote.”

Kuaga kwa Mohamed Hussein Simba kumetafsiriwa kama hatua muhimu kwake ya kuhamia Yanga. Timu ambayo imehusishwa sana na kuhitaji Saini yake katika dirisha hili kubwa la usajili. Inatajwa kuwa taratibu za kusaini mkataba wake zimefanyika akiwa kwenye kambi ya Stars, Misri.

SOMA HII HAPA: Khadim Diaw mrithi wa Zimbwe Jr Simba SC | Msindo atajwa | Yanga SC hawapoi

Hawa wanatajwa kuwa wachezaji wapya wa Simba

Jonathan Sowah rasmi asaini Simba SC
Jonathan Sowah Simba

Baadhi ya majina ambayo yanatajwa kumalizana na Simba, na kuichezea timu hiyo msimu ujao ni; Sowah, kiungo Privat Djéssan Bi (21), Khadim Diaw (26), na Wilson Nangu (23). Nangu amesaini miaka miwili na Simba hivyo msimu ujao atavaa jezi nyekundu.

SOMA HII ZAIDI: Simba SC kuelekea msimu wa 2025/26 kupitisha panga kwa wachezaji/ Tamko latolewa/ Kupoteza Dabi 5

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.