- Mauritania imepoteza pointi tatu muhimu mbele ya Tanzania kwenye mchezo wa CHAN 2024 baada ya dakika 90.
- Shomari Kapombe beki wa Tanzania alifunga bao pekee la ushindi katika dakika za lala salama akitumia pasi maridhawa kutoka kwa Nado.
- Mudathir Yahya na Feisal Salum watwaa tuzo za uchezaji bora wote wakiwa ni viungo wa timu ya taifa ya Tanzania.
TIMU ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars inanukia kufuzu hatua ya robo fainali ya Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN 2024). Agosti 6 2025 baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Mauritania 0-1 Tanzania. Ushindi huo ni wa pili mfululizo kwa wenyeji Tanzania.
Mamilioni yanakusubiri sasa hivi
Cheza Aviator uvune mamilioni ambayo yapo kwa ajili yako. Rahisi sana unachotakiwa kufanya ni kupaisha Kindege. Wakati rubani ukiwa hewani, unapata mgao wako kutoka SportPesa.

Huyu hapa muuaji wa Mauritania

Soma hii: Tanzania vs Burkina Faso na Kenya vs DR Congo: Wenyeji waanza kwa kishindo CHAN 2024.
Agosti 6 2025 ilikuwa ni moto kwa wenyeji Tanzania kutokana na upinzani mkubwa. Mauritania walikuwa katika ubora dakika 89 kulinda huku wakishambulia kwa kushtukiza. Tanzania ilifanya mashambulizi mengi lakini hayakuwa na matokeo mazuri.
Katika dakika za lala salama beki wa Tanzania Shomari Kapombe alifunga bao la ushindi. Ilikuwa dakika ya 90 Kapombe alifunga bao hilo lililowanyanyua mashabiki wa Tanzania. Ni pasi maridhawa kutoka kwa mguu wa kulia wa kiungo Idd Nado.
Nado kwenye mchezo huo uliokuwa ukifuatiliwa na wengi duniani alitoa pasi ya dhahabu akiwa nje ya 18. Kapombe ambaye ni beki mwenye uzoefu kitaifa na kimataifa alikuwa kwenye hali ya utulivu. Akiwa ndani ya 18 alifanya maamuzi ya haraka kuupokea mpira ukiwa juu akitumia mguu wa kushoto kupiga shuti.
Shuti hilo lilikwenda moja kwa moja nyavuni likimshinda mlinda mlango wa Mauritania Abderrahmane Sarr. Kipa huyo hakuwa na chaguo zaidi ya kuokota mpira nyavuni. Mwisho wa mchezo pointi tatu zikawa ni mali ya Tanzania iliyopata ushindi kwenye mchezo wa pili.
Mashuti ambayo yalipigwa kuelekea langoni
Mauritania walipiga jumla ya mashuti matano. Katika mashuti hayo matano kuelekea kwenye lango la Tanzania mawili yalilenga lango. Kipa Yacouba Sulemani ambaye alianza kikosi cha kwanza aliokoa hatari hizo.
Katika dakika ya 90 mwamuzi alimuonyesha kadi ya njano kipa wa Tanzania. Sababu kubwa ya kadi hiyo ya njano ni kile alichotafsri kuwa alikuwa anapoteza muda. Hiyo ilitokea baada ya Tanzania kupata bao la kuongoza.
Timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars iliongoza kwenye chati yakupiga mashuti mengi.Ni mashuti 12 ilipiga kwenye mchezo huo. Katika mashuti hayo ni mawili pekee yalilenga lango.
Shuti ambalo lilileta ushindi lilipigwa na Kapombe. Beki huyo anakuwa ni beki wa pili kufunga kwenye mechi za CHAN 2024 Uwanja wa Mkapa. Beki wa kwanza alikuwa ni Mohamed Hussen Zimbwe Jr ambaye alifunga kwenye mchezo dhidi ya Burkina Faso uliochezwa Agosti 2 2025 ukiwa ni mchezo wa ufunguzi.
Hapa ndipo Tanzania ipo kwa sasa Kundi B

Soma hii: SportPesa TZ: Matokeo ya Moja kwa Moja | Burudani Halisi 2025
Baada ya ushindi kwenye mechi mbili Tanzania inaongoza Kundi B. Imekusanya jumla ya pointi sita. Ndani ya dakika 180 ilizoshuka uwanjani haijaruhusu kufungwa bao.
Ni Dickson Job ambaye alikuwa nahodha kwenye mchezo dhidi ya Mauritania.Job alikuwa anaingoza safu ya ulinzi ya Tanzania kuhakikisha inakuwa salama. Kiungo mkabaji ambaye ni chaguo la kwanza la Kocha Mkuu Hemed Suleman ni Yusuph Kagoma.
Safu ya ushambuliaji ya timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars imefunga jumla ya mabao matatu. Katika mabao hayo mawili yamefungwa na mabeki. Shomari Kapombe na Mohamed Hussen.
Bao moja la Tanzania limefungwa na kiungo Sopu. Kiungo huyo alifunga bao kwa mkwaju wa penati mchezo dhidi ya Burkina Faso. Ni Clement Mzize alisababisha penati hiyo baada ya kuchezewa faulo ndani ya 18.
Tanzania ikiwa inaongoza Kundi B na pointi 6 wanafuata Burkina Faso wakiwa na pointi 3. Madagascar na Mauritania hawa kila timu ina pointi moja. Jamhuri ya Kati haijakusanya pointi na mchezo ujao itacheza na Mauritania na huku Tanzania ikicheza na Madagascar itakuwa ni Agosti 9 2025, Uwanja wa Mkapa.
Mashabiki bega kwa bega na timu ya Tanzania, Uwanja wa Mkapa

Soma hii: Tanzania 2-1 Senegal CECAFA 2025 Arusha
Mashabiki wameendelea kujitokeza Uwanja wa Mkapa wakiwa bega kwa bega na timu. Kuanzia mchezo wa ufunguzi uliochezwa Agosti 2 2025. Mchezo wa pili dhidi ya Mauritania bado wamejitokeza kwa wingi.
Hemed Suleman, Kocha Mkuu wat imu ya Tanzania amesema hilo ni kubwa. Kocha huyo amebainisha kuwa kujitokeza kwa mashabiki kunawapa nguvu wachezaji kupambana kila wakati. Amewaomba kuendelea kujitokeza katika mechi zote.
“Mashabiki wamekuwa wakijokeza kwenye mechi zetu zote. Hakika wanatupa nguvu hasa wachezaji kupambana kutafuta ushindi. Haya mashindano yana ushindani mkubwa hivyo uwepo wao unaongeza nguvu.
“Wachezaji wanajituma kutafuta matokeo. Makosa tunayafanyia kazi ili kuwa bora lakini wanakazi kulipa deni kwa mashabiki. Deni hilo ni kupata ushindi kwenye mechi zetu ambazo tunacheza,”.
Tuzo kwa viungo wa mpira
Viungo wa mpira walitwaa tuzo kwenye mechi mbili mfululizo. Mchezo wa kwanza wa CHAN Feisal Salum alitwaa tuzo ya mchezaji bora. Kwenye mchezo wa pili ni Mudathir Yahya alitwaa tuzo hiyo.
Hitimisho
Tanzania inahitaji ushindi kwenye mech izote kuandika rekodi kutinga hatua ya robo fainali ya CHAN 2024. Ushindi kwenye mechi mbili mfululizo ni rekodi kubwa. Ili kuandika rekodi kubwa zaidi wachezaji wanakazi kushinda mechi zilizobaki.


