SemfukoSemfuko
  • Simba SC yasajili mashine hizi mbili kwa mpigo, wapania kuuwasha moto Ligi Kuu NBC 2025/26.
  • Mastaa hawa wawili walitangazwa rasmi na Simba SC jana Alhamisi.
  • Mara tu, baada ya kutambulishwa, nyota hao wanatarajiwa kusafiri leo Ijumaa kwenda kambini Ismailia, Misri kwa ajili ya ‘Pre-season’

Kuelekea msimu ujao wa 2025/26, huko Simba SC mambo ni mengi muda mchache. Hii ni baada ya jana Alhamisi, kutambulisha mashine zao mbili mpya. Nyota hao ni viungo Morice Abraham na Hussein Semfuko. Mara tu, baada ya kutambulishwa mastaa hao leo Ijumaa wanatarajiwa kujiunga na wenzao nchini Misri.

‘Kindege’ cha Sportpesa kinakupa mamilioni leo

Ukiendelea kuhabarika na makala hii, kumbuka unaweza kushinda mamilioni muda huu. Cheza sasa mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kupitia Kampuni bora ya michezo ya kubashiri ya SportPesa bonyeza picha hii chini.

Kuhusu usajili wa Simfuko na Morice

Morice
Morice

Simba jana Alhamisi walikamilisha usajili na kuwatangaza kiungo mkabaji, Hussein Semfuko. Huku pia wakimtangaza kiungo mshambuliaji Morice Abraham. Nyota hao wanatarajiwa kuunda kikosi cha Simba kuelekea msimu wa mashindano 2025/2026.

Semfuko mwenye umri wa miaka 21, amesaini mkataba wa miaka mitatu. Nyota huyo rai awa Tanzania alionyesha uwezo mkubwa msimu uliopita akiwa na Coastal Union ya Tanga. Semfuko ni pendekezo la kocha mkuu wa Simba Fadlu Davids.

SOMA HII PIA: Baada ya Rushine Simba yamshusha Allasane Kante huyu hapa: Tetesi usajili Ligi Kuu NBC 2025/26

Kuhusu safari ya kwenda Misri

Budo safarini
Budo safarini

Ikumbukwe tayari kundi la kwanza la kikosi cha Simba liliondoka Tanzania juzi Jumatano kuelekea nchini Misri. Safari hii ni kwa ajili ya kuweka kambi ya maandalizi ya kabla ya msimu wa mashindano (Pre Season), ya mwezi mmoja. Timu hiyo imeweka kambi katika mji wa Ismailia.

Inatazamiwa kundi la pili ambalo litawahusisha Morice, Semfuko, Allasane Kante na wengine wataondoka leo Ijumaa. Ikumbukwe kambi hiyo ya Misri ilitumiwa na Simba pia msimu uliopita. Kambi hiyo inatarajiwa kuhusisha wachezaji ambao wamesalia na mastaa wote wapya.

Ahmed akizungumzia hilo amesema: “Sehemu ya kikosi chetu iliondoka Jumatano kuelekea Misri. Kundi la pili nalo litaondoka saa yoyote kutoka sasa. Hii ni kwa ajili ya kuweka kambi ya maandalizi ya kabla ya msimu. Kambi inatarajiwa kuwa na nyota wetu wote isipokuwa waliopo kwenye majukumu ya timu ya Taifa inayojiandaa na michuano ya CHAN.

“Kikosi cha Simba kinatarajiwa kurejea nchini Agosti 28, mwaka huu. Mara baada ya kurudi Simba tutaanza msimu mpya wa mashindano 2025/2026 tukiwa na matumaini makubwa ya kufanya vizuri.”

SOMA HII ZAIDI: Rushine De Reuck rasmi asaini na atambulishwa Simba SC: Mashine nyingine 6 kutangazwa tetesi usajili Ligi Kuu NBC 2025/26

Zoezi la kutambulisha mashine mpya linaendelea

Rushine De Reuck rasmi asaini na kutambulishwa Simba SC
Jonathan Sowah Simba

Kuhusu zoezi la kutambulisha mastaa wapya waliowasajili kwenye dirisha hili. Meneja wa Habari na mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally ameweka wazi kuwa Simba SC imepania kufanya usajili mkubwa. Ikumbukwe kwamba timu hiyo msimu wa 2024/25 ilikosa mataji yote jambo linaloelezwa kuwapa hasira kubwa na wametamba kuendelea kushusha vyuma.

“Kwa sasa viongozi wa Simba SC wametapakaa kila kona kwenye nchi za Afrika. Hii ni katika kuhakikisha wanamalizia usajili wa wachezaji wapya. Huu ni usajili mwingine wa kishindo na sitaongea sana safari hii nitaacha watu waone wenyewe. Tumekamilisha usajili wa wachezaji saba na bado tunaendelea,” amesema Ahmed.

SOMA HII PIA: Simba SC yashtua na fumbo la jezi namba 6 ni Feisal au udhamini?

Hawa hapa wachezaji walioachwa na Simba SC mpaka sasa

Simba SC yasajili mashine hizi mbili kwa mpigo,
TETESI Tshabalala kutua Yanga

Kuhusu maboresho ya kikosi chao, Simba tayari wameachana na kundi kubwa la wachezaji. Baadhi ya mastaa ambao wamepewa ‘thank you’, Simba ni Pamoja na Aishi Manula aliyeenda Azam FC. Wengine ni Pamoja na Omary Omary ambaye amepelekwa kwa mkopo Mashujaa FC.

Wengine ni: Che Malone aliyetimkia USMA, Fabrince Ngoma mkataba wake umeisha. Kelvin Kijili ametimkia Singida Black Stars. Valente Nouma naye ameachwa, nahodha Mohammed Hussein amemaliza mkataba na listi hii inatarajiwa kuongezeka. Hii ni pale Simba itakapoanza rasmi kutangaza mastaa wake.

Hitimisho: Wanaofuatia kutambulishwa hawa hapa

Ukiachana na Rushine na Kante ambao tayari wametambulishwa, Simba inaelezwa kumalizana na mastaa wakubwa. Baadhi ya majina ambayo yanatajwa kumalizana na Simba, na kuichezea timu hiyo msimu ujao ni; Sowah, kiungo Privat Djéssan Bi (21), Khadim Diaw (26), na Wilson Nangu (23). Nangu amesaini miaka miwili na Simba hivyo msimu ujao atavaa jezi nyekundu.

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.