Offen ChikolaOffen Chikola
  • Usajili wa Yanga SC kuelekea msimu mpya wa 2025/26 umepamba moto kutokana na wapya wenye rekodi kubwa kutambulishwa.
  • Mohamed Doumbia mrithi wa mikoba ya Aziz Ki kijana mdogo wa miaka 26 kipaji chake kinatajwa kumleta Jangwani.
  • Balla Conte anashikilia rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kutambulishwa Jangwani kuelekea msimu mpya.

Mabingwa mara 31 wa Ligi Kuu Tanzania Bara inayodhaminiwa na NBC, Yanga SC imefikisha orodha ya wapya 11 waliotambulishwa. Ni benchi la ufundi na wachezaji ikiwa ni maandalizi kuelekea msimu wa 2025/26. Ikumbukwe kwamba Yanga SC ni mabingwa watetezi msimu wa 2025/26 hivyo wapo kwenye maboresho ya kikosi hicho kuelekea msimu mpya.

Paisha Kindege sasa hivi uvune mamilioni

Muda wa kupaisha kindege ni sasa ili kuwa kwenye mgao wa mamilioni. Marubani wapo makini kwenye kazi hivyo wana uhakika na ushindi. Ni rahisi cheza Aviator ushinde rubani kwa kishindo.

Aviator banner

Hapa tunakuletea orodha ya wapya waliotambulishwa ndani ya Yanga SC. Rekodi zao na timu ambazo walitoka. Bado kuna wengine watatambulishwa hivi karibuni, hawa hapa ni wapya namna hii:-

Ecua Elastin

Ecua C
Ecua ingizo jipya Yanga SC 2025/26. Source: Yanga SC.

Soma hii: Yanga SC imetambulisha wapya 10 dirisha la usajili

Agosti Mosi 2025 alitambulishwa Yanga SC kwa dili la miaka miwili. Msimu wa 2024/25 alikuwa anacheza Zoman FC alifunga magoli 15 na pasi 12 za magoli. Rekodi hizo ni kwenye mashindano yote. Yeye ni raia wa Ivory Coast.

Doumbia

Doumbia
Doumbia ingizo jipya ndani ya Yanga SC. Source: Yanga SC.

Soma hii: Yanga SC yashusha mashine hii nyingine usiku: Tetesi, usajili Ligi Kuu ya NBC 2025/26

Agosti 3 2025 Yanga SC ilimtambulisha kiungo, Mohamed Doumbia. Nyota huyu ana umri wa miaka 26 amejiunga na Yanga SC kutokea FC Slovan Liberec ya Jamuhuri ya Czech. Anatajwa kuwa na uwezo kwenye majaribio ya mashuti ya mbali na kutengeneza nafasi za mabao kwa wengine.

Anatajwa kurithi mikoba ya Aziz Ki. Ikumbukwe kwamba Aziz Ki msimu wa 2024/25 alikuwa ndani ya Yanga SC yupo kwenye changamoto mpya. Ni Wydad Casablanca ya Morocco nyota huyo yupo.

Mshambuliaji wa mabao Boyeli

Yanga SC walifunga ukurasa wa Julai 31 2025 kwa kumtambulisha Andy Bobwa Boyeli. Nyota huyo mwenye miaka 24 alikuwa anacheza Sekhukhune United ya Afrika Kusini kwa mkopo kwa msimu mmoja. Julai 31 alifunga ukurasa kwa wachezaji waliotambulishwa Julai.

Paul Mattews  

Anaitwa Paul Matthews alitambulishwa ndani ya Yanga SC Julai 29 2025. Hivyo atakuwa Jangwani msimu wa 2025/26. Anainga kwenye benchi la ufundi yeye ni Mkurugenzi wa Ufundi.

Manu Rodriguez

Jina lake ni Manu alitambulishwa Julai 29 2025. Anaingia kwenye benchi la ufundi akiwa ni kocha msaidizi ndani ya Yanga SC. Kocha Mkuu ni Romain Folz ambaye naye ni mpya mrithi wa mikoba ya Miloud Hamdi.

Lassine Kouma

Kouma
Kouma

Soma hii: Lassine Kouma mrithi wa Khalid Aucho Yanga SC

Utambulisho wake ni Lassine Kouma mchezaji mpya ndani ya kikosi cha Yanga SC. Huyu ni mrithi wa mikoba mikoba ya Khalid Aucho. Kasajiliwa Yanga SC akitokea Stade Malien.

Ni jezi namba 8 amekabidhiwa kuwa utambulisho wake akiwa Jangwani. Msimu wa 2025/26 uzi namba 8 ulikuwa ni utambulisho wa Khalid Aucho. Kiungo huyo mkabaji hatakuwa ndani ya kikosi cha Yanga SC baada ya mkataba wake kuisha.

Balla Conte

Huyu usajili wake ulikuwa na muvtano mkubwa kwa kuwa alikuwa anatajwa kuwa kwenye rada za Simba SC. Julai 18 2025 Yanga SC ilimtambulusha Moussa Balla Conte. Ingizo hili jipya ni kutoka CS Sfaxien ya Tunisia yeye ni raia wa Guinea.

Offen Chikola

 Mkali wa kutumia mguu wa kushoto akiwa uwanjani kwenye majukumu yake ni njano na kijani. Anaitwa Offen Chikola alitambulishwa Yanga SC Julai 22 2025. Ni kandarasi ya miaka miwili. 2024/25 akiwa na Tabora United alifunga mabao 8 kati ya 28 yaliyofungwa na timu hiyo. Yanga SC inaingia kwenye orodha ya timu ambazo Chikola alizifunga msimu wa 2024/25.

Casemiro

 Jina lake ni Abdulnassir Mohamed maarufu kwa jina la Casemiro alitambulishwa rasmi Jangwani, Julai 23 2025. Ni mzawa ambaye atakuwa kwenye changamoto mpya. Anaingia kwenye orodha ya wachezaji wapya ndani ya kikosi cha Yanga SC chenye maskani yake Jangwani, Dar.

Ninju

Jina lake ni Abubakar Nizar Othuman, maarufu kwa jina la Ninju kutoka Azam FC alitambulishwa rasmi Julai 27 2025.

Romain

Romain Folz
Romain Folz Kocha Mkuu wa Yanga SC 2025/26.

Soma hii: Romain Folz kocha mpya Yanga SC mwenye CV kubwa

Ilikuwa ni Julai 23 2025 Kocha Mkuu wa Yanga SC Romain Folz alitambulishwa. Kocha huyo anabeba mikoba ya Miloud Hamdi aliyekuwa akikinoa kikosi hicho. Msimu wa 2025/26 atakuwa kwenye benchi la ufundi.

Yanga SC wakutana Dar na mikakati mizito

Yanga SC, Agosti 3 2025 walikutana Dar kwa mikakati mizito kuelekea msimu mpya wa 2025/26. Katika kikao hicho kizito kilichofanyika katika Hotel yenye hadhi ya nyota tano hesabu kubwa ilikuwa kuelekea msimu mpya. Miongoni mwa wachezaji alikuwepo Maxi Nzengeli, Djigui Diarra, Aboutwalib Mshery.

Hitimisho

Yanga SC inafanya maboresho kwenye kikosi hicho kwa maandalizi ya msimu mpya wa 2025/26. Kazi kwenye ligi ni kutetea taji la NBC ililotwaa 2024/25. Kambi yake ya ndani ipo Kigamboni, Dar.

image
Share this: