- Che Malone wa Simba SC aanza kazi kwa Waarabu ikiwa ni maandalizi kuelekea msimu mpya wa 2025/26.
- Mrithi wake Simba SC ni raia wa Afrika Kusini anaitwa Rushine De Reuck mchezaji wa kwanza kutambulishwa kuwa nyekundu na nyeupe.
- Fadlu Davids, Kocha Mkuu wa Simba SC alifanya naye kazi kwenye mechi 25 za ligi akikosekana katika mechi tano pekee kati ya 30 msimu wa 2024/25.
Che Malone beki wa zamani wa Simba SC ameanza kazi kwa Waarabu wa Algeria. Ni USM Alger atakuwa hapo baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili. Tayari Simba SC imemtambulisha mrithi wake kuelekea msimu wa 2025/26.
Wiki inaanza kwa kicheko kwa kushinda mamilioni sasa
Mwanzo wa wiki mpya ni kicheko kwa marubani wale wanaopaisha ndege. Ushindi mkubwa unakusubiri cheza Aviator sasa uvune mamilioni. Mgao ni mkubwa kwa ajili yako ukicheza kindege unashinda.

Julai 30 2025 alianza kazi ndani ya timu yake mpya. Ni USM Alger ya Algeria atakuwa huko kwenye changamoto mpya. Nyota huyo ameuzwa na Simba SC.

Soma hii: Che Malone anafuata Simba SC | Yanga SC wampa tabu nje ndani | Tuzo na mabao yote
Aliwaaga mashabiki na uongozi wa Simba SC
Beki huyo aliwaaga mashabiki wa Simba SC na uongozi rasmi Julai 30 2025. Che Malone aliweka wazi kuwa maisha ya mpira kuna changamoto ambazo zinatokeo hivyo huwezi kuzikwepa. Mbali na hilo alibainisha kuwa Simba SC itabaki kwenye moyo wake.
“Ninawashukuru mashabiki na uongozi wa Simba SC kwa namna ambavyo tumekuwa bega kwa bega katika kila hatua.Nyakati ngumu na zile za furaha tulikuwa pamoja. Hakika tulikuwa ni familia moja,”.
Huyu hapa mrithi wa Che Malone

Beki anayetajwa kurithi mikoba ya Che Malone ni Rushine De Reuck. Huyu ni mchezaji wa kwanza kutambulishwa ndani ya kikosi cha Simba SC. Rushine ni rai awa Afrika Kusini.
Alitambulishwa Julai 29 2025. Aliwahi kucheza Mamelod Sundowns akitajwa kuwa beki mwenye uwezo mkubwa uwanjani. Yupo kwenye orodha ya wachezaji waliopo kambini Misri.
Magoli na rekodi zake akiwa na uzi wa Simba SC
Beki Che Malone msimu wa 2024/25 alicheza jumla ya mechi 25 akikomba jumla ya dakika 2,065. Baada ya mechi 30 ni mabao 13 timu hiyo ilifungwa. Yanga SC ni timu ambayo imeifunga Simba SC mabao mengi ambayo ni matatu.
Simba SC ikiwa imefunga jumla ya mabao 69 yeye kafunga mabao mawili. Ni mechi 30 Simba SC ilishuka uwanjani ambazo ni dakika 2,700. Ina wastani wa kufunga bao moja kila baada ya dakika 39.
Che Malone ni mfungaji wa bao la kwanza katika kikosi cha Simba SC kinachonolewa na Kocha Mkuu, Fadlu Davids. Bao la ufunguzi la Simba SC lilifungwa kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Tabora United. Che Malone alifungua ukurasa huo ilikuwa dakika ya 13.
Bao hilo alifunga kwa pigo la kichwa akiwa ndani ya 18. Mchezo ulichezwa Agosti 18 2024 lilitosha kufungua ukurasa wa mabao kwenye ligi. Katika mchezo huo beki huyo alichaguliwa kuwa mchezaji bora.
Pasi ya bao ilitoka kwenye miguu ya kiungo mshambuliaji Jean Ahoua. Simba SC ilikomba pointi tatu mazima katika mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa. Hati safi ya kwanza kwa kip awa Simba SC, Moussa Camara ilipatikana.
Mchezo huo ulichezwa Uwanja wa KMC Complex. Baada ya dakika 90 ubao ulisoma Simba SC 3-0 Tabora United. Mwamuzi wa kati alikuwa ni Nassoro Mwinchui.
Bao la pili Che Malone alifunga kwenye mchezo dhidi ya Tanzania Prisons. Bao hilo alifunga dakika ya 5 akiwa ndani ya 18 kwa mguu wa kulia. Ni bao la mapema ndani ya kikosi cha Simba SC msimu wa 2024/25 kufungwa na Che Malone.
Ilikuwa ni Okroba 22 2024 alipachika bao hilo akiwa ndani ya 18. Baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Sokoine ulisoma Tanzania Prisons 0-1 Simba SC. Lilikuwa ni bao la ushindi kwa Simba SC ugenini. Katika mchezo huo alichaguliwa kuwa mchezaji bora.
Kabatini kuna tuzo alibeba

Soma hii: Wachezaji wa Simba SC watakao achwa msimu wa 2025/26
Msimu wa 2024/25 Che Malone alikusanya tuzo mbili. Hizo ni zile za baada ya dakika 90 kugota mwisho na kuchaguliwa kuwa mchezaji bora. Mechi moja ilikuwa nyumbani na mechi moja ilikuwa ugenini.
Tuzo ya kwanza ilikuwa Uwanja wa KMC Complex Simba SC ikiwa nyumbani. Tuzo ya pili ilikuwa Uwanja wa Sokoine, Mbeya Simba SC ikiwa ugenini. Kwenye mech izote hizo Che Malone alifunga na kuchaguliwa kuwa mchezaji bora.
Dakika 450 alikosekana Che Malone kwenye ligi
Ni dakika 450 Che Malone alikosekana kwenye mechi za ligi ya NBC msimu wa 2024/25 ambazo ni mechi tano. Sababu ya kukosekana kwenye mechi hizo ni maumivu ya nyama za paja. Alipata maumivu hayo kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Azam FC uliochezwa Uwanja wa Mkapa.
Katika mchezo huo baada ya dakika 90 ubao ulisoma Simba SC 2-2 Azam FC. Wababe hao wawili waligawana pointi mojamoja. Simba SC iliruhusu bao la jioni dakika ya 88 kupitia kwa Zidane ambaye alianzia benchi.
Ni Zidane Zireri wa Azam FC alimfunga kipa namba moja wa Simba SC, Moussa Camara. Baada ya dakika 90 Zidane alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mchezo. Pasi ya bao hilo ilitoka kwa kiungo Feisal Salum maarufu kwa jina la Fei Toto.


