Che Malone (-)Che Malone (-)
  • Che Malone yamkuta Simba SC kuelekea msimu wa 2025/26 akitajwa kuwa miongoni mwa nyota watakaowekwa kando katika timu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu ya NBC.
  • Simba SC imemaliza msimu ikiwa nafasi ya pili, Che Malone raia wa Cameroon alitwaa tuzo mbili katika mechi za ushindani.
  • Yanga SC walimpa tabu katika mechi zote mbili msimu wa 2024/25 ndani ya dakika 180 kwenye Kariakoo Dabi.

Che Malone yamkuta Simba SC akitajwa kuwa miongoni mwa wachezaji watakaowekwa kando msimu ujao. Che Malone msimu wa 2024/25 alicheza jumla ya mechi 25 akikomba jumla ya dakika 2,065. Inaelezwa kuwa huenda akapewa Thank You licha ya kuvuja jasho kwenye kutimiza majukumu ndani ya Simba SC.

Aviator banner
Che Malone- Zimbwe
Che Malone, Zimbwe, Hamza miongoni mwa mabeki wa Simba SC. Source: Simba SC.

Soma hii: Yanga SC inaongoza orodha ya timu zilizofungwa mabao machache

Simba SC ni namba mbili kwa timu ambazo zimefungwa mabao machache. Baada ya mechi 30 ni mabao 13 timu hiyo ilifungwa. Yanga SC ni timu ambayo imeifunga Simba SC mabao mengi ambayo ni matatu.

Ipo wazi kwamba timu namba moja kufungwa mabao machache ni Yanga SC. Yanga SC baada ya mechi 30 ni mabao 10 ilifungwa. Mchezo dhidi ya Tabora United iliruhusu mabao mengi, ilikuwa Yanga SC 1-3 Tabora United.

Mabao aliyofunga Che Malone ndani ya ligi

Simba SC ikiwa imefunga jumla ya mabao 69 yeye kafunga mabao mawili. Ni mechi 30 Simba SC ilishuka uwanjani ambazo ni dakika 2,700. Ina wastani wa kufunga bao moja kila baada ya dakika 39.

Che Malone anaingia kwenye orodha ya mabeki waliofunga kwenye mechi za ligi. Huyu ni mfungaji wa bao la kwanza katika kikosi cha Simba SC kinachonolewa na Kocha Mkuu, Fadlu Davids. Bao la ufunguzi la Simba SC lilifungwa kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Tabora United.

Che Malone alifungua ukurasa huo ilikuwa dakika ya 13. Pigo la kichwa akiwa ndani ya 18 Agosti 18 2024 lilitosha kufungua ukurasa wa mabao kwenye ligi. Katika mchezo huo beki huyo alichaguliwa kuwa mchezaji bora.

Pasi ya bao ilitoka kwenye miguu ya kiungo mshambuliaji Jean Ahoua. Simba SC ilikomba pointi tatu mazima katika mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa. Hati safi ya kwanza kwa kipawa Simba SC, Moussa Camara ilipatikana.

M- Camara
Camara kipa namba moja wa Simba SC 2024/25. Source: Simba SC.

Soma hii: Tetesi usajili ligi Kuu ya NBC 2025/26 wanaoondoka Yanga hawa hapa – SportPesa Tanzania

Mchezo huo ulichezwa Uwanja wa KMC Complex. Baada ya dakika 90 ubao ulisoma Simba SC 3-0 Tabora United. Mwamuzi wa kati alikuwa ni Nassoro Mwinchui.

Bao la pili Che Malone alifunga kwenye mchezo dhidi ya Tanzania Prisons.  Bao hilo alifunga dakika ya 5 akiwa ndani ya 18 kwa mguu wa kulia. Ni bao la mapema ndani ya kikosi cha Simba SC msimu wa 2024/25 kufungwa na Che Malone.

Ilikuwa ni Okroba 22 2024 alipachika bao hilo akiwa ndani ya 18. Baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Sokoine ulisoma Tanzania Prisons 0-1 Simba SC. Lilikuwa ni bao la ushindi kwa Simba SC ugenini. Katika mchezo huo alichaguliwa kuwa mchezaji bora.

Tuzo zake mkononi

Kwenye ligi msimu wa 2024/25 Che Malone alikusanya tuzo mbili. Hizo ni zile za baada ya dakika 90 kugota mwisho na kuchaguliwa kuwa mchezaji bora. Mechi moja ilikuwa nyumbani na mechi moja ilikuwa ugenini.

Tuzo ya kwanza ilikuwa Uwanja wa KMC Complex Simba SC ikiwa nyumbani. Tuzo ya pili ilikuwa Uwanja wa Sokoine, Mbeya Simba SC ikiwa ugenini. Kwenye mech izote hizo Che Malone alifunga na kuchaguliwa kuwa mchezaji bora.

image

Mechi alizokosekana ndani ya Simba SC

RS Berkane vs Simba SC 17/5/2025
Kikosi cha Simba SC bila ya uwepo wa Che Malone 2024/25. Source: Simba SC.

Che Malone alikosekana kwenye mechi tano pekee za ligi msimu wa 2024/25. Sababu ya kukosekana kwenye mechi hizo ni maumivu ya nyama za paja aliyopata. Ilikuwa kweye mchezo wa ligi dhidi ya Azam FC uliochezwa Uwanja wa Mkapa.

Katika mchezo huo baada ya dakika 90 ubao ulisoma Simba SC 2-2 Azam FC. Wababe hao wawili waligawana pointi mojamoja. Simba SC iliruhusu bao la jioni dakika ya 88 kupitia kwa Zidane ambaye alianzia benchi.

Zidane Zireri wa Azam FC alimtungua kipa namba moja wa Simba SC, Moussa Camara. Baada ya dakika 90 Zidane alichaguliwa kuwa mchezaji bora kwa kuwa alifunga bao lililoipa pointi moja Azam FC. Pasi ya bao hilo ilitoka kwa kiungo mchezeshaji Feisal Salum.

Che Malone mbele ya Yanga SC

Aziz KI V Chemalone
Aziz KI wa Yanga SC vs Chemalone wa Simba SC mzunguko wa kwanza 2024/25.

Soma hii: Pacome wa Yanga SC na Jean Ahoua wa Simba SC vita yao waliimaliza kibabe

Beki huyo mbele ya Yanga SC nje ndani alipata tabu kwenye msako wa pointi sita alianza kikosi cha kwanza mechi zote mbili. Ni dakika 180 kaziyeyusha akiwa uwanjani kutimiza majumu yake. Kariakoo Dabi zote mbili zilikuwa na ushindani mkubwa Uwanja wa Mkapa.

Juni 25 2025 ulikuwa ni mchezo wa funga kazi ndani ya ligi. Ilikuwa Yanga SC 2-0 Simba SC. Che Malone alianza kikosi cha kwanza. Kwenye mchezo huo aliokoa baadhi ya hatari kama alivyofanya dakika ya 21, 29.

Che Malone raia wa Cameroon alikuwa ndani ya kikosi kwenye mechi zote mbili msimu wa 2024/25 dhidi ya Yanga SC. Ule mzunguko wa kwanza ilikuwa Simba SC 0-1 Yanga SC. Yanga SC imevuna pointi sita mbele ya Simba SC kwenye mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara inayodhaminiwa na NBC.

Simba SC imemaliza msimu ikiwa haina taji lolote ndani ya 2024/25. Kwenye ligi ni nafasi ya pili pointi 78 katika Kombe la Shirikisho Afrika ni washindi wa pili walicheza fainali na kupoteza mbele ya RS Berkane. Kwenye CRDB Federation Cup waligotea hatua ya nusu fainali kwa kufungashiwa virago na Singida Black Stars.

Aviator banner

Paa na kindege ushinde mamilioni kila siku

Share this: