- Yanga SC 2-0 JKT Tanzania, umesoma hivyo ubao Uwanja wa Mkwakwani baada ya vita ya jasho na damu kuishuhudia Yanga wakitinga Fainali yua Kombe la Shirikisho la CRDB.
- Kwa ushindi huu, Yanga SC sasa ni rasmi wanasubiri mshindi wa mchezo wa Nusu Fainali ya pili kati ya Simba SC na Singida Big Stars ambao wanatarajia kuvaana mwishoni mwa mwezi huu kati ya tarehe 28 hadi 31.
- RYanga wamefuzu fainali 5 mfululizo za mashindano hayo ambapo wamefanikiwa kushinda ubingwa mara 4, na mara ya mwisho kupoteza fainali ilikuwa msimu wa 2020/21 dhidi ya Simba walipofungwa bao 1-0.
Yanga SC 2-0 JKT Tanzania, umesoma ubao Uwanja wa Mkwakwani baada ya vita ya jasho na damu kuishuhudia Yanga wakitinga Fainali yua Kombe la Shirikisho la CRDB, sasa wanasubiri mshindi wa nusu fainali nyingine kati ya Simba na Singida BS kujua wataumana na nani fainali.
Yanga SC 2-0 JKT Tanzania, mchezo ulikuwaje?

Yanga walionesha dhamira yao ya kutaka ushindi tangu dakika za mwanzo, kwa kushambulia kwa kasi na kuilazimisha JKT kucheza kwa tahadhari kubwa.
Mashambulizi yao ya haraka yaliwalazimu JKT kujilinda kwa nguvu, lakini presha hiyo ilizaa matunda dakika ya 41 pale mshambuliaji kutoka Zimbabwe, Prince Dube alipoipa Yanga bao la uongozi kufuatia makosa ya ulinzi ya JKT ndani ya eneo la 18.
SOMA HII PIA: Yanga SC vs JKT Tanzania Mei 18 2025 Kariakoo Dabi yanukia
JKT walijitahidi kujibu mashambulizi hayo, lakini walikumbana na safu ya ulinzi imara ya Yanga iliyoongozwa na Ibrahim Bacca na Dickson Job na mchezo kukamilisha ngwe ya kwanza kwa uongozi wa wa bao 1-0 kwa Yanga.
Yanga waliendelea na kasi yao kipindi cha pili na kuonekana kuwa na mpango mahsusi wa kumaliza mchezo mapema, lakini ilibidi wasubiri mpaka dakika ya 90 kupata bao la pili kupitia kwa Mudathir Yahya akitumia asisti ya Chama.

Bao hilo lilizima kabisa matumaini ya JKT kurejea mchezoni, huku Yanga wakiendelea kutawala mchezo na kupata bao la 3 dakika za nyongeza, lakini lilikataliwa na mwamuzi.
Ushindi huo si tu, uliihakikishia Yanga tiketi ya kucheza fainali, bali pia umeendeleza ubabe wao katika soka la Tanzania, huku wakionesha ubora wao wa kiuchezaji katika kila idara ya mchezo.
Mbinu za Kocha Miloud Hamdi
Kocha mkuu wa Yanga, Miloud Hamdi, alionesha ubora wa mbinu zake kwa kuchagua kikosi cha ushindani kilichocheza kwa nidhamu na mpangilio mzuri. Kiungo Stephane Aziz Ki na Maxi Nzengeli walimiliki katikati ya uwanja na kuamua kasi ya mchezo.
Kwa sehemu kubwa ya mchezo viungo, Duke Abuya na Mudathir Yahya walikata mipango ya JKT na kuhakikisha timu yao inabaki na mpira muda mwingi. Kwa upande wa ulinzi, Yanga walikuwa na nidhamu ya hali ya juu.
Makocha wa timu ya JKT walijaribu kufanya mabadiliko, lakini kila juhudi zilikwama mbele ya safu ya ulinzi ya Yanga iliyoonyesha uzoefu na maarifa ya hali ya juu.
SOMA HII PIA: Zanzibar kumenoga huku Simba SC vs RS Berkane kule Yanga watangaza jambo zito
JKT Tanzania waonyesha Moyo wa ushindani
Licha ya kupoteza mchezo huo, JKT Tanzania walionesha mapambano na nidhamu ya hali ya juu, ambapo viungo wao Said Ndemla na Shiza Kichuya ni miongoni mqwa wale walionyesha mapambano ya kweli kwa dakika zote za mchezo.
Licha ya kazi kubwa waliyofanya na kupambana kwa nguvu kubwa kujaribu kutengeneza mashambulizi, lakini walionekana kukosa makali kwenye eneo la ushambuliaji.
Yanga na safari ya Fainali

Kwa ushindi huu, Yanga SC sasa ni rasmi wametinga fainali kwa zaidi ya msimu wanne mfululizo na sasa wanasubiri mshindi wa nusu fainali nyingine kati ya Simba SC na Singida Black Stars ambao wanatarajia kuvaana mwishoni mwa mwezi huu kati ya tarehe 28 hadi 31.
Yanga, ambao ni mabingwa watetezi wa kombe hilo, wanatarajiwa kupambana kuhakikisha wanabeba taji hilo tena na kuongeza mafanikio mengine katika historia yao ndefu ya soka la Tanzania.
Kwa ubora waliouonesha dhidi ya JKT, mashabiki wa Yanga wana kila sababu ya kuamini kuwa kikosi chao kiko tayari kuendeleza utawala wao na kutwaa kombe hilo kwa mara nyingine.
Tanzania sasa inasubiri kwa hamu mechi ya fainali ambayo inatarajiwa kuwa ya kuvutia na yenye ushindani mkubwa, huku Yanga SC wakijivunia historia, uzoefu na ari ya ushindi.
SOMA HII PIA: Yanga na kocha Rulani Mokwena nini kinaendelea?

