- Yanga na kocha Rulani Mokwena nini kinaendelea? Ndilo swali ambalo limepamba moto kuulizwa na maelfu ya wapenda soka, baada ya taarifa za ndani kuthibitisha Yanga wanawinda saini ya kocha huyo?
- Taarifa za kuaminika kutoka Yanga zimethibitisha kuwa, uongozi wa timu hiyo umefanya maamuzi ya kuachana na kocha wao wa sasa Miloud Hamdi mara baada ya kumalizika kwa msimu.
- Miloud ameiongoza Yanga kwenye mechi 13, ambapo ameshinda mechi 12 na sare 1, huku Yanga ikionyesha wastani mzuri wa kufunga ambapo imefunga goli 45 na Clean Sheets 8.
Yanga na kocha Rulani Mokwena nini kinaendelea? Ndilo swali ambalo limepamba moto kuulizwa na maelfu ya wapenda soka, hasa baada ya taarifa za ndani kuthibitisha kuwa Yanga wanawinda Saini ya kocha huyo?
Nini kinaendelea kuhusu sakata la kocha mpya Yanga?

Taarifa za kuaminika kutoka ndani ya Yanga zimethibitisha kuwa, uongozi wa timu hiyo umefanya maamuzi ya kuachana na kocha wao wa sasa Miloud Hamdi mara baada ya kumalizika kwa msimu.
Yanga wamefikia uamuzi huo kama sehemu ya kurejesha makali ya timu hiyo na kuifanya kuwa tishio, wakati huu wakijipanga na ushiriki wa mashindano ya Ligi ya Mabingwa msimu ujao.
SOMA HII PIA: Rekodi wachezaji wa Yanga SC 3-0 Namungo FC, 2024/25, Nondo, Maxi, Nahimana walivuja jasho
Hizi hapa rekodi za Miloud tangu atue Yanga
Tangu ajiunge na kikosi cha Yanga kocha, Miloud Hamdi akitokea kikosi cha Singida Black Stars ameiongoza Yanga kucheza mechi 13 za mashindano yote.
Kwenye hizo mechi 13 timu yake imeshinda mechi 12 na sare 1 na ndani ya hizo mechi, Yanga imeonyesha kuwa na wastani mzuri wa kufunga ambapoimefunga goli 45 na Clean Sheets 8.
Yanga na kocha Rulani Mokwena

Mara baada ya kuelezwa kuwa Yanga tayari wamefikia makubaliano ya kuachana na kocha Miloud, taarifa za ndani zaidi zimeeleza kuwa Yanga wameanza mchakato wa kocha mpya ambapo wapo kwenye mazungumzo na kocha wa zamani wa Wydad Casablanca, Rhulani.
Yanga na kocha Rulani Mokwena wamehusishwa mara kadhaatangu alipokuwa na kikosi cha Mamelodi Sundowns. Akithibitisha tetesi hizo mchambuzi, Hans Raphael amesema: “Yanga wako kwenye mazungumzo ya kina na kocha wa zamani wa Mamelodi na Wydad Casablanca, Rhulani Mokwena mwenye umri wa miaka 38.
“Kuhusu Yanga na kocha Rulani Mokwena yuko tayari kupunguza kiwango chake cha mshahara ili kuja kushinda vikombe na Yanga. Yanga wanamuhitaji kocha huyu aje na wasaidizi wake (kocha wa viungo, fitness na Video analyst). Yanga wanamtaka Rhulani Mokwena haraka sana na chochote kinaweza kutokea wiki hii.”
SOMA HII PIA: Nusu Fainali ASFC- Je Dabi ya Simba na Yanga Kujirudia Fainali?
Ishu ya kocha Ibenge imekuwaje?

Kabla ya kuwekeza nguvu kwa kocha, Rhulani Mokwena inaelezwa kuwa Yanga walikuwa kwenye mchakato wa mazungumzo na kocha Mkongomani, Florent Ibenge.
Kwa mujibu wa mchambuzi, Hans amesema: “Jina la Ibenge lilikuwa juu kwenye list ya makocha wanaohitajika na yanga ila mazungumzo ya pande zote mbili yamekufa baada ya kushindwa kukubaliana baadhi ya vitu muhimu.
Yanga yaendeleza dozi kwenye Ligi Kuu Bara

Ukiachana na masuala ya mchakato wa kusaka kocha mpya ndani ya kikosi chao, Yanga wameendelea kuwa na wakati mzuri kwenye Ligi Kuu Bara ambapo wameendeleza dozi mbele ya Namungo.
Hii ni baada ya Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Namungo katika mchezo wao uliopigwa siku ya Jumanne katika mchezo ambao ulishuhudia staa, Maxi Nzengeli akiibuka na tuzo ya mchezaji bora.
Maxi alipokea tuzo hiyo mara baada ya kuhusika kwenye mabao mawili kati ya matatu ya mchezo huo akifunga bao moja na kuasisti mara moja kwa lililofungwa na Aziz Ki.
Huu unakuwa ushindi wa pili wa Yanga mbele ya Namungo kwernye Ligi Kuu Bara msimu huu, hivyo kuzoa pointi nyumbani na ugenini. Ikumbukwe kwamba kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza uliochezwa Novemba 30, 2024 Yanga walishinda mabao 2-0.
