- Mkutano Mkuu Yanga SC 2026 umefanyika kwa mafanikio makubwa leo Agosti 2, 2026.
- Kama ilivyokuwa mwaka jana, mkutano huo mkuu wa leo umefanyika kwenye ukumbi wa the Super Dome, Masaki Dar es Salaam.
- Pamoja na matukio mengi makubwa yaliyojitokeza, mkutano huo mkuu ulishuhudia Hersi Said akichaguliwa tena kuwa rais wa klabu hiyo kwa miaka 4 ijayo.
- Makala hii inachambua baadhi ya mambo muhimu yaliyotokea.
Moja ya stori kubwa za michezo leo Agosti 2, 2026 ni kuhusu kufanyika mkutano mkuu Yanga SC 2026. Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa kisasa wa The Super Dome, uliopo Masaki, Dar es Salaam. Mkutano huu amba oni utekelezaji wa kikatiba ya timu hiyo ulishuhudia, Hersi Said akichaguliwa tena kuwa rais wa Yanga SC kwa miaka 4 ijayo. Makala hii inakuletea kwa ufupi uchambuzi wa mkutano huo.
Cheza na ushinde sasa na ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni muda huu
Bado hujashinda na kindege cha SportPesa? Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda mpaka zaidi ya milioni 800 muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kupitia Kampuni bora ya michezo ya kubashiri ya SportPesa bonyeza picha hii chini.

Muhtasari kuhusu Mkutano Mkuu Yanga SC 2026

Mkutano mkuu wa Yanga SC 2025, ni utekelezaji wa maelekezo ya kikatiba na kikanuni. Mkutano huu kwa kawaida hufanyika kila mwaka, kama jukwaa rasmi la kutoa taarifa muhimu za uendeshaji wa klabu hiyo. Baadhi ya vipaumbele na Agenda muhimu za mkutano huo ni Pamoja na ufuatiliaji wa mafanikio, na kuweka msingi imara wa kiuchumi kwa msimu ujao.
Kusoma kumbukukumbu za Mkutano Mkuu 2025, soma hii: Mkutano mkuu wa Yanga SC 2025: Mambo 10 yaliyotikisa ‘Super Dome’ leo
Mgeni rasmi mkuu wa mkoa Dar es Salaam
Mgeni rasmi katika tukio la mkutano huu alikuwa mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam, Albert Chalamila. Kama sehemu ya kumkaribisha Hersi alisema: “Nichukue fursa hii kumshukuru Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Chalamila kwa kuungana nasi katika mkutano huu wa leo. Aidha, nimshukuru Waziri wa Madini Anthony Peter Mavunde, pamoja na Mjumbe wa bodi ya wadhamini mzee wetu Mh George Mkuchika na viongozi wote waliohudhuria na kuamua kuungana nasi katika mkutano huu muhimu wa kuhakikisha tunaendelea kuijenga klabu.
Mafanikio ya Yanga SC kwenye miaka 4 ya kwanza ya Hersi

Akuzungumzia mafanikio ya uongozi wake, Hersi amesema: “Katyika kipindi cha miaka 4 cha uongozi wangu, nikishirikiana na Kamati Tendaji, Yanga SC imeshinda Jumla ya Makombe 16 ndani na nje ya nchi. Ligi Kuu ya NBC, Tanzania Bara, Mataji manne (4) na kuweka rekodi ya kubeba Ubingwa mara 5 mfululizo.
“Katika kipindi hiki cha miaka minne, Yanga SC imecheza mechi 120, tumeshinda mechi 101, sare 12 na kufungwa mechi 7 tu, tukiweka rekodi ya kukusanya pointi 315. Yanga SC imefunga jumla ya magoli 286 na kufungwa 51 tu, hivyo kufanya tofauti ya magoli ya kufunga na Kufungwa kuwa magoli 235. Kwenye Kombe la Shirikisho la TFF (CRDB Federation Cup), YANGA sc imeshinda makombe mara 4 mfululizo, tukiweka rekodi ya kucheza Miaka 5 mfululizo UNBEATEN. Tumebeba Kombe la Ngao ya Jamii mara 4.
Mkuu wa mkoa Chalamila ajiunga na Yanga SC

Akizungumza katika hafla hiyo mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Chalamila amesema: “Ni heshima kubwa kwangu kuwa sehemu ya siku hii muhimu, na ya kihistoria kwa Young Africans Sports Club. Niseme ukweli, kila klabu ya Dar es Salaam inapopata ushindi, mimi nakuwa na furaha. Lakini Yanga SC inaposhinda, furaha yangu huwa kubwa zaidi, nimevutiwa sana kuitwa Shalulile, nafikiri ni moja ya sababu ambazo zimefanya leo nichague kuwa mwanachama wa klabu hii. Ni heshima kubwa kwa taifa kuwa mchezaji kama Shalulile.
KUJUA KILA KITU KUIHUSU YANGA SC, SOMA HII: Yanga SC: Historia, Usajili wote, kikosi, Ratiba, Matokeo na Takwimu
Muhtasari wa Ripoti ya Fedha (mapato na matumizi) ya Yanga SC
Akiwasilisha ripoti ya fedha mkurugenzi wa Fedha, Justina Ernest amesema: “Kwa msimu wa 2025/2026, klabu ilikusanya jumla ya TSh 29.36 bilioni, matumizi ya klabu yalifikia TSh 29.34 bilioni. Sehemu kubwa ilielekezwa kwenye mishahara na marupurupu ya watumishi, usajili na uhamisho wa wachezaji, maandalizi ya mechi, usafiri, chakula na malazi. Baada ya matumizi hayo, klabu ilibaki na bakaa ya TSh 17.5 milioni na kwa msimu wa 2026/2027, klabu imepanga kukusanya TSh 20.70 bilioni, huku ikitarajia kutumia TSh 36.01 bilioni.”
Taarifa kuhusu Baraza la wadhamini (Waziri Mkuu Mwigulu ‘out’, Ridhiwani Kikwete ‘in’

Bodi ya wadhamini ilikuwa imeundwa na wajumbe watano ambao ni;
Mwenyekiti:
Mheshimiwa George Mkuchika
Wajumbe:
* Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba
* Bi. Fatma Karume
* Mheshimiwa Anthony Peter Mavunde
* Mheshimiwa Abbas Tarimba
Kwa heshima kubwa, klabu inatambua nafasi ya Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba ambaye aliteuliwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kutokana na majukumu hayo makubwa ya wadhifa huo, Waziri Mkuu ameomba kujiondoa katika nafasi yake ya ujumbe wa Kamati ya Uchaguzi ili kupata wasaa wa kutumikia taifa. Kutokana na mabadiliko hayo, Kamati tendaji, imeridhia kujaza nafasi yake na Mheshimiwa Ridhiwani Jakaya Kikwete, ambaye sasa atahudumu kama mjumbe wa Baraza la Wadhamini.
Kuhusu uwanja wa yanga soma hii: Uwanja wa Yanga SC watikisa! GSM aonyesha jeuri ya pesa, Ali Kamwe afunguka mazito
Mdhamini mkuu SportPesa waahidi makubwa
Kwa niaba ya mdhamini mkuu kampuni ya SportPesa kupitia kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi SportPesa Tanzania, Abbas Tarimba amesema: “Ni dhahiri kuwa hakuna klabu imepata mataji kama Yanga, mpaka sasa hivi makombe yamekuwa ya mfululizo kwa mipango niliyoiona, Yanga watakwenda kufanya vizuri sana msimu huu.”
Hitimisho

Mkutano mkuu Yanga SC 2026 ni udhihirisho wa wazi wa kazi kubwa ambayo inafanywa na Yanga SC, kuwa klabu yenye mafanikio makubwa ndani nan je ya mpiaka ya Tanzania. Mafanikio yao na mipango yao inaonyesha matokeo ya utashi wa kuhakikisha wanachama wanashirikishwa, na usawa wa kifedha unatiwa mkazo. Kila la kheri Yanga SC. Endelea kufuatilia taarifa mbalimbali kupitia SportPesa blog.

