- Zanzibar kumenoga huku Simba SC vs RS Berkane, ndiyo taarifa yamoto kwa sasa ikifutatiliwa na umati wa watu, kufuatia kuhamishiwa Zanzibar kwa mchezo wa Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.
- Sasa uongozi wa Yanga nao leo Mei 15, 2025 wametangaza kuendeleza mashirikiano ya kuitangaza Zanzibar, kwa kushiriki kwenye mchezo maalum wa magwiji ‘legends’ kutoka Brazil utakaopigwa Julai 27, mwaka huu.
- Ikumbukwe mara ya mwisho Simba SC kucheza fainali ya mashindano ya CAF ilikuwa 1993, ambapo waliibuka washindi wa pili na sasa wanajiandaa na fainali ya Mei 17 ugenini na nyumbani Mei 25, 2025.
Huko Zanzibar kumenoga huku Simba SC vs RS Berkane, ikiwa taarifa yamoto kwa sasa kufuatia kuhamishwa kwa mchezo wa Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika, Yanga nao wametangaza kuandaa jambo zito visiwani humo.
Yanga wana jambo gani Zanzibar?

Uongozi wa Yanga leo Mei 15, 2025 wametangaza kuendeleza mashirikiano ya kuitangaza Zanzibar, kwa kuhusika katika ushiriki na uandaaji wa mchezo maalum wa magwiji ‘legends’ ambao unatarajiwa kupigwa siku ya Julai 27, mwaka huu.
Mchezo huo mkubwa na wa kihistoria unatarajiwa kuhusisha magwiji wa soka la Brazil wakiongozwa na staa wa zamani wa Barcelona na mshindi wa mchezaji bora wa dunia Ballon D’or mwaka 2005, Ronaldinho dhidi ya wale wa Tanzania hususani wa Zanzibar.
SOMA HII PIA: Yanga SC inawadai Simba SC 2024/25
Rais Yanga atangaza kupeleka watu Zanzibar
Akizungumza katika hafla fupi iliyofanyika Zanzibar, Rais wa Yanga injinia Hersi Said amesema: “Nichukue fursa hii kumpongeza Rais wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Hussein Mwinyi kwa juhudi zake za kuendelea kuitangaza Zanzibar duniani.
“Hili tukio la ‘Match of the legends’ tunalolizindua leo naamini ni tukio kubwa na la kihistoria kuwahi kufanyika katika ardhi hii. Tunakwenda kumpokea mmoja wa wachezaji bora kuwahi kucheza mpira duniani, Ronaldinho Gaucho akiwa na wenzake.
Yanga kushiriki asilimia 100

Rais wa Yanga ameendelea kusema: “Dhamira ya Klabu yetu ya kushiriki kwenye ‘Match of the Legends’ ni kuongeza thamani ya tukio hili. Tutashikiri kwa asilimia mia moja kwenye kufanya ‘promotion’ na kutoa baadhi ya watendaji wa klabu yetu kuja kusaidia uratibu wa mechi.
“Niwaalike Watanzania wote, lakini na rafiki zetu wapenda mpira kutoka sehemu mbalimbali Barani Afrika kuja Zanzibar kushuhudia tukio hili la kihistoria. Naamini kila mpenda soka atapenda kumuona Ronaldinho na wenzake wakicheza huku ukiwa umeketi jukwaani.”
SOMA HII PIA: Simba SC vs RS Berkane Uwanja wa Mkapa waleta sekeseke CAF, tamko latolewa
Waziri wa Utalii Zanzibar naye atoa ahadi nzito
Naye Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar, Mudrick Ramadhan Soraga amesema: “Hivi karibuni tulisaini mkataba na klabu ya Young Africans SC kwenye kuibeba ajenda yetu ya kuutangaza utalii wetu kupitia ‘Visit Zanzibar’.
“Hivyo naamini ujio wa mchezo huu wa ‘Match of The Legends’ na ushiriki wa Young Africans, jambo hili litakuwa kubwa sana na lenye mvuto wa aina yake
“Mchezo huu wa ‘Match of the Legends’ kama Serikali tunautazama pia kama kipimo cha kuionyesha dunia ni kwa kiasi gani Zanzibar iko tayari kuandaa matukio makubwa ikiwemo AFCON. Naamini tuko tayari kwa tukio hili la kihistoria.”
Fainali Zanzibar kumenoga huku Simba SC vs RS Berkane kupigwa Zanzibar?
Mapema leo Alhamisi vyanzo mbalimbali zikiwemo akaunti rasmi za mitandao ya kijamii za Shirikisho la soka Afrika CAF kueleza uwepo wa mabadiliko ya uwanja wa Fainali ya pili kutoka Uwanja wa, Benjamin Mkapa mpaka New Amaan Complex.
Hatua hiyo imeibua hisia tofauti miongoni mwa wadau wa soka nchini, ambao wengi wamehusianisha tukio hilo na siasa za mpira wa Afrika, hasa kutokana na ushawishi wa mmiliki wa RS Berkane ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Caf.
Simba watoa tamko zito
Kutokana na sakata hilo, wenyeji wa mchezo huo Simba wameweka wazi kuwa taarifa rasmi ya uwanja utakaotumika kwa mchezo wa marudiano inatarajiwa kutolewa mara baada ya kumalizika kwa mchezo wa mkondo wa kwanza utakaopigwa Jumamosi.
Mpaka sasa mashabiki uongozi wa Simba umeendelea kuwahimiza mashabiki wake kuendelea kununua tiketi kwa ajili ya mchezo huo wa Mei 25, 2025.
Mashabiki waendelea kumaliza tiketi
Huku sintofahamu hiyo ikiendelea, mashabiki wa Simba wameonekana kuwa na mwitikio mkubwa wa kununua tiketi hizo, ili kupata fursa ya kuandika rekodi ya kushuhudia fainali hiyo ya kihistoria.
Ikumbukwe mara ya mwisho Simba SC kucheza fainali ya mashindano ya CAF ilikuwa 1993, ambapo waliibuka washindi wa pili na sasa inakwenda kucheza kwa mara nyingine fainali hiyo Mei 17 ugenini na ile ya pili itakayoamua mshindi inatarajiwa kuchezwa Mei 25 2025.

