Simba SC 2-1 Singida Black Stars Kagame Cup 2026I- Doumbia
  • Mchezo wa mwisho Simba SC 2-1 Singida Black Stars Kagame Cup 2026 hatua ya makundi
  • Ibrahim Doumbia afungua akaunti ya mabao kwa mara ya kwanza mara baada ya kusajiliwa
  • Ellie Mpanzu afunga goli la ushindi, Clatous Chama bado yumo
  • Jonathan Sowah amrejea Singida Black Stars 2026/27

Simba SC 2-1 Singida Black Stars Kagame Cup 2026 hatua ya makundi wametoana wawakilishi hawa kutoka Tanzania. Mshambuliaji wa mabao Ibrahim Doumbia alifungua akaunti kwa kufunga dakika ya 27. Hili linakuwa bao la kwanza mara baada ya kusajiliwa na Simba SC raia huyu wa Mali. Singida Black Stars walifunga kupitia kwa kupitia kwa Methew Tegisi dakika ya 50 na Ellie Mpanzu alifunga la ushindi dakika ya 66.

Bado hujashinda? Cheza na ushinde mamilioni ya aviator ‘Kindege’ cha SportPesa

Je, hujashinda na kindege cha SportPesa? Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kubashiri SportPesa bonyeza picha hii chini.

Huu hapa mkakati wa usajili Simba SC: Mkakati wa usajili mpya Simba SC 2026/27 | Kelvin Nashon, Chilambo na Bakari Msimu kazi imeanza | SportPesa Blog

SportPesa Aviator Maximum Payout – TZS Million

FT: Simba SC 2-1 Singida Black Stars Kagame Cup 2026

Simba SC 2-1 Singida Black Stars Kagame Cup 2026
Ellie Mpanzu kwenye mchezo vs Singida Black Stars

Ubao umesoma Simba SC 2-1 Singida Black Stars Kagame Cup 2026 hatua ya makundi Julai 31,2026. Unakuwa ni ushindi wa kwanza wa Simba SC hatua ya makundi 2026 wakiwashinda mabingwa watetezi. Matokeo hayo sio rafiki kwa wawakilishi wote kutoka Tanzania wametoana kwa kuishia hatua ya makundi.

Singida Black Stars walikuwa ni mabingwa watetezi walitwaa taji hilo 2025 mashindano yalipofanyika Tanzania. Msimu wa 2026 wameishia hatua ya makundi. Kutoka Kundi B ni Jamus SC imetinga hatua ya nusu fainali ya michuano baada ya kupata ushindi wa mabao 2-1 Mogadishu City.

Doumbia afungua akaunti ya mabao

Simba SC 2-1 Singida Black Stars Kagame Cup 2026
Ibrahim Doumbia mshambuliaji wa Simba SC.

Mjue mshambuliaji Doumbia: Ibrahim Doumbia mshambuliaji wa mabao Simba SC raia wa Mali | SportPesa Blog

Mshambuliaji mpya wa Simba SC, Ibrahim Doumbia amefungua akaunti ya mabao. Mchezaji huyo katika mechi mbili zilizopita hakupata nafasi yakufunga. Mchezo wa tatu dhidi ya Singida Black Stars hapo alionyesha uwezo wake kwa kufunga dakika ya 27.

Kama ambavyo uchambuzi wa SportPesa kwenye makala iliyopita ulieleza ubora wa mchezaji huyo na hatari ilipo. Tulibainisha kwamba ni mzuri kwa mipira ya kichwa hasa krosi na ile yakutengwa. Imekuwa hivyo bao lake la kwanza amefunga kutokana na krosi iliyopigwa na Libase Gueye yeye akafunga kwa pigo la kichwa.

Bao la pili limefungwa na Ellie Mpanzu ambaye ni winga tegemeo akiwa ameongeza mkataba kuendelea kuitumikia Simba SC. Winga huyo alitumia vema krosi iliyopigwa na Duchu. Timu hiyo kwa sasa bado kambi yake ipo Rwanda katika maandalizi ya msimu mpya 2026/27.

Kikosi cha Simba SC vs Singida Black Stars

Langoni

Kassali

Mabeki

Duchu

Kibabage

Toure

De Reuck

Viungo

Yusuph Kagoma

Gueye

Kelesto

Oura

Mshambuliaji

Doumbia

Sowah amekosa nafasi ya dhahabu

Mshambuliaji wa Singida Black Stars, Jonathan Sowah katika dakika za lala salama alikuwa kwenye nafasi ya kusawazisha bao. Akiwa karibu la lango la Simba SC alipiga shuti ambalo lilikwenda nje ya lango. Shuti hilo lilimfanya ajilaumu kwa kuwa alikosa utulivu kukamilisha jukumu lake akiwa kwenye eneo zuri la kufunga.

Huyu ni mshambuliaji wa mabao ambaye amerejea kwa mara nyingine Singida Black Stars. 2025/26 alikuwa katika kikosi cha Simba SC. Kutokana na matatizo ya utovu wa nidhamu mabosi wa Simba SC walisitisha mkataba wa nyota huyo ambaye amerejea kwenye timu yake ya zamani.

Clatous Chama bado yumo

Kiungo mshambuliaji wa Simba SC, Clatous Chama bado yumo kutokana na ubora alionao uwanjani. Nyota huyo ameongezewa kandarasi kuendelea kuwa katika kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu, Steve Barker. Alianzia benchi kwenye mchezo huo dhidi ya mabosi wake wa zamani.

Chama amecheza timu kubwa 3 Tanzania. Alianza na Simba SC kisha Yanga SC na Singida Black Stars. Amerejea kwa mara nyingine Simba SC ni chaguo la kwanza unyamani.

Hitimisho

Simba SC 2-1 Singida Black Stars Kagame Cup 2026 ni matokeo ya mchezo wa mwisho hatua ya makundi. Timu zote zimeishia hatua ya makundi katika mashindano hayo yanayofanyika Rwanda. Ni sare 2 na ushindi mchezo mmoja katika mechi za maandalizi ya msimu wa 2026/27.

Share this: