JKU vS YangaJKU vS Yanga

  • Mara ya mwisho Yanga na JKU walikutana Oktoba 10, 2021 na Yanga kuibuka na ushindi wa bao 1-0.
  • Mashindano hayo yameshirikisha timu 8 msimu huu, 4 kutoka Tanzania Bara na 4 kutoka Tanzania Visiwani.
  • Yanga sc yatinga Fainali kwa changamoto ya matuta 1-3 dhidi ya Zimamoto katika mchezo wa Nusu Fainali.

JKU Vs Yanga Fainali Muungano Cup 2025 unatarajia kuwa mchezo mkali ambao unapigwa Mei Mosi mwaka huu, kwenye Uwanja wa Gombani, Zanzibar.

Yanga wamefanikiwa kutinga Fainali kwa changamoto ya matuta 1-3 dhidi ya KVZ katika mchezo wa Nusu ambao ulikuwa na ushindani wa aina yake ulipigwa kwenye Uwanja wa Gombani, Zanzibar na kukosekana mshind ndani ya dakika 90.

Mchezo wa Nusu Fainali Vs Zimamoto ulikuwaje?

JKU Vs Yanga Fainali Muungano Cup 2025
Maxi akipambana na walinzi wa JKU

Yanga ndio walikuwa wa kwanza kupata bao kutoka kwa kiungo mshambuliaji wao Mkongomani, Maxi Nzengeli na mara baada ya bao hilo Yanga waliendelea kutawala mchezo lakini hawakufanikiwa kutumia nafasi walizotengeneza.

Zimamoto walipata bao lao la kusawazisha dakika za mwishoni mwa kipindi cha pili kupitia mkwaju wa Penalti mara baada ya kipa wa Yanga, Aboutwalib Mshery kumfanyia madhambi mshambuliaji wa Zimamoto ndani ya eneo la 18.

Mpaka dakika 90 zinakamilika hakiukuwa na mbabe kwani mchezo ulimalizika kwa sare ya bao 1-1, hali iliyofanya hatua ya mikwaju ya Penalti kufuata.

Mlinda mlango wa Yanga, Mshery alisimama vyema na kuibuka shujaa wa mchezo huo kwa kuokoa penalti 2 na kuifanya Yanga kuibuka na ushindi wa Penalti 1-3.

Ni JKU Vs Yanga Fainali Muungano Cup 2025

KI Aziz
KI Aziz

Baada ya Yanga SC yatinga fainali Muungano Cup 2025, sasa mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Bara wanatarajia kuvaana na kikosi cha JKU katika mchezo wa Fainali ambao unasubiriwa kwa hamu na mamilioni ya mashabiki wa soka nchini.

Ikumbukwe JKU wao walikata tiketi ya kucheza Nusu Fainali baada ya kuwaondosha Azam FC katika mchezo wa Nusu fainali kwa ushindi wa mabao 2-1.

Hizi zilifuzu nusu fainali ya Muungano Cup 2025

Robo Fainali ya Muungano Cup msimu huu ilishuhudia mzani ukisawazwa, kwa kuwa na timu mbili kutoka Tanzania Bara na timu mbili kutoka Tanzania Visiwani.

Ukiachana na Yanga waliofuzu fainali, timu nyingine ambazo zilifuzu Nusu Fainali mpaka sasa ni, Azam FC, Zimamoto na JKU.

walichosema Yanga kuelekea fainali

Ki- Muda
Kikosi cha Yanga

Mara Baada ya ushindi huo sasa ni JKU Vs Yanga Fainali Muungano Cup 2025. wameweka wazi kuwa malengo yao ni kuhakikisha wanaibuka na ushindi katika mchezo wa fainali na kubeba ubingwa.

Akizungumzia malengo yao, Nahodha wa Yanga, Bakari Mwamnyeto amesema: “Ulikuwa mchezo mgumu, tunawapongeza Zimamoto kwa kuonyesha ushindani mzuri lakini imekuwa jambo jema kwetu kufuzu fainali.

 “Malengo yetu ni kushinda mchezo wa fainali wa JKU Vs Yanga Fainali Muungano Cup 2025 ili kushinda ubingwa huu, tunajua haitakuwa rahisi lakini tumejiandaa kufanya vizuri.”

Nalo benchi la ufundi la Yanga SC limeelezea furaha yake kuhusu ushindi huo, ambapo wamesema kuwa Yanga SC yatinga Fainali Muungano Cup 2025 ni matokeo ya maandalizi mazuri na ushirikiano.

Benchi hilo limetamba na kuongeza kuwa wachezaji wako tayari kwa changamoto ya mchezo wa hatua ya fainali zinazofuata katika michuano ya Kombe la Muungano 2025.​

Mashabiki wa Yanga SC walijitokeza kwa wingi katika Uwanja wa Gombani, wakishangilia timu yao kwa nguvu. Baada ya mchezo, mashabiki walionyesha furaha yao kwa kusherehekea ushindi huo.

Sehemu ya mashabiki hao walisema kwao hatua hiyo ni ya kujivunia  na ni ishara ya mafanikio makubwa katika michuano ya Kombe la Muungano 2025.​

Yanga waanza maandalizi ya fainali

Baada ya ushindi huo, Yanga SC hakuna kulaza damu ambapo tayari wameanza maandalizi ya mechi ya Fainali ya Kombe la Muungano 2025, ambapo kama makala haya yalivyoeleza wanatarajia kuvaana na JKU.

Mchezo huo ni miongoni mwa michezo inayosubiriwa kwa hamu kubwa kuona nani ataibuka mbabe na kutabgazwa bingwa wa Fainali, huku ikionekana ni kama kuna vita ya Tanzania Bara na Visiwani

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.