Fadlu SimbaFadlu Simba
  • Simba SC iliwatungua Mashujaa FC mzunguko wa kwanza bao la ushindi dakika ya 90.
  • Mashujaa FC kocha mpyaa anabalaa zito alishusha dozi ya tatutatu kwa wapinzani wake dakika 180.
  • Ni mchezo wa kwanza kwa Simba SC kati ya minne iliyopo kwenye ratiba yake mzunguko wa pili.

SIMBA SC vs Mashujaa FC mchezo wa ligi unaosubiriwa kwa shauku kubwa na mashabiki kwa wababe wawili wenye kisasi kukutana ndani ya Uwanja wa KMC Complex Mei 2 2025 ni mwenye kisu kikali atakula nyama ya pointi tatu baada ya dakika 90.

Fadlu Kocha Mkuu Simba
Fadlu Kocha Mkuu Simba 2024/25. Source: Simba SC.

Ipo wazi kwamba Simba SC ipo nafasi ya pili kwenye msimamo inakutana na wapinzani wao Mashujaa FC iliyo nafasi ya 10 takuwa na mechi nne ndani ya Mei ambazo ni msako wa pointi 12.

Dakika 270 wote wagumu

Wababe hawa wawili Simba SC na Mashujaa FC kwenye mechi zao tatu zilizopita ndani ya ligi ngoma ni ngumu kwa kuwa katika msako wa pointi 9, kila timu ilikomba pointi 7.

Ushindi kwa Simba SC ilikuwa kwenye mechi mbili na iliambulia sare moja saw ana Mashujaa FC iliyoambulia pointi moja ugenini na Simba SC iliambulia pointi moja ikiwa nyumbani.

Tatu za Simba SC

Steven Mukwala
Steven Mukwala nyota wa Simba SC aliyefunga bao mbele ya Mashujaa FC mzunguko wa kwanza. Source: Simba SC.

Februari 24 2025 ilikuwa Simba 2-2 Azam FC, kwenye Mzizima Dabi waligawana pointi mojamoja na Azam FC katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa.

Machi Mosi 2025 katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid baada ya dakika 90 ubao ulisoma Coastal Union 0-3 Simba SC na kete ya tatu kwa Simba SC ilikuwa ni Machi 14 2025 ubao wa Uwanja wa KMC Complex ulisoma Simba 6-0 Dodoma Jiji.

Hizi hapa tatu za Mashujaa FC

Mashujaa vibe
Wachezaji wa Mashujaa kwenye moja ya mchezo wa ushindani. Source: Mashujaa FC.

Aprili 20 2025 Mashujaa ilikuwa kwenye msako wa pointi tatu muhimu dhidi ya Namungo FC ilishuhudia ubao wa Uwanja wa Majaliwa ukisoma Namungo 1-1 Mashujaa, waligawana pointi mojamoja na mtupiaji kwa Mashujaa alikuwa ni Jaffary Kibaya.

Aprili 10 2025, Mashujaa FC walikuwa nyumbani, Kigoma mwisho wa reli baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Lake Tanganyika ulisoma Mashujaa 3-0 Tabora United wakigawa dozi kwa wapinzani wao na kusepa na pointi tatu.

Aprili 5 2025 wakiwa Uwanja wa Lake Tanganyika, ubao ulisoma Mashujaa 3-0 Fountain Gate walipeleka kilio kwa wanafunzi wa Fountain Gate kwa kuwapa somo la kusaka pointi tatu ndani ya uwanja.

Kocha mpya Mashujaa FC balaa

Mayanga
Salum Mayanga, Kocha Mkuu wa Mashujaa FC iayotumia Uwanja wa Lake Tanganyika mechi za nyumbani. Source: Mashujaa FC.

Machi 21 2025 ni Salum Mayanga alitambulishwa kuwa Kocha Mkuu wa Mashujaa FC akichukua nafasi ya Mohamed Abdallah Bares aliyekutana na Thank You, Februari 26 2025 kwa makubaliano ya pande zote mbili.

Kocha huyo balaa lake sio la kitoto kwa kuwa aliwaondoa matajiri wa Dar, Azam FC kwenye CRDB Federation Cup alipokuwa na kikosi cha Mbeya City kinachoshiriki Championship.

Kwenye mechi ambazo ameongoza timu hiyo imekuwa ikifunga na kukomba pointi tatu kama ilivyosepa na pointi tatu mbele ya Tabora United na mchezo wake wa kwanza ilikuwa Machi Mosi mchezo wa CRDB Federation Cup ubao ulisoma Mashujaa 1-0 Ken Gold.

Kuna kisasi kwa wapinzani hawa

Novemba Mosi 2024 ubao wa Uwanja wa Lake Tanganyika ulisoma Mashujaa 0-1 Simba SC, bao la ushindi likifungwa na Steven Mukwala. Wababe hawa wanakisasi, Simba SC kwenye hesabu za kulinda rekodi na Mashujaa FC kutibua.

Simba SC inayonolewa na Kocha Mkuu, Fadlu Davids baada ya mechi 22 ipo nafasi ya pili na pointi zake kibindoni ni 57. Safu ya ushambuliaji ya Simba SC imetupia mabao 52 na kinara ni Jean Ahoua mwenye mabao 12 na pasi 7 za mabao ambapo mabao yake yote kafunga kwa mguu wa kulia.

Mashujaa FC nafasi ya 10 kwenye msimamo pointi 30 baada ya mechi 26 huku safu ya ushambuliaji ikitupia jumla ya mabao 26 wastani wakufunga bao moja kila baada ya dakika 90.

Semaji hili hapa la Simba SC

Ahmed Ally, Meneja wa idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC ameweka wazi kuwa mchezo wao dhidi ya Mashujaa FC unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa KMC Complex utakuwa mgumu kulingana na wapinzani wao kuwa bora.

Mchezo huo ni kiporo ratiba yake imepangwa upya kwa kuwa Simba SC ilikuwa kwenye mechi za kimataifa kwenye Kombe la Shirikisho Afrika ikiwa imetinga hatua ya fainali na inatarajiwa kucheza na RS Berkane.

Simba SC kutoka Tanzania itaanzia ugenini kwenye fainali yake ya kwanza inayotarajiwa kuchezwa Mei 17 na fainali ya pili inatarajiwa kuchezwa Mei 25 Dar itakayotoa mshindi wa jumla atakayetwaa taji hilo la Afrika.

Ally amesema kuwa kila mchezo wanauchukulia kwa umuhimu na wanatambua hakukuna kazi nyepesi hivyo watapambana kupata matokeo chanya ndani ya uwanja.

“Ni mchezo muhimu kwetu katika kupata pointi tatu muhimu na tunatambua wapinzani wetu wapo imara tutakabiliana nao ili kupata pointi tatu muhimu inawezekana na tupo tayari.

“Mashabiki wajitokeze kwa wingi kuongeza nguvu kwa wachezaji kwa kuwa uwepo wao ni muhimu na silaha yetu kubwa kupata matokeo kwenye mechi zetu zote huwa inakuwa kwa shabiki ambaye ni mchezaji wa 12.”

Share this: