Simba SC yafuzu Fainali CAFCCSimba SC yafuzu Fainali CAFCC

  • Simba wamefuzu Fainali ya Shirikisho Afrika kwa matokeo ya jumla ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Stellenbosch
  • Hii ni fainali ya pili katika historia ya Simba kucheza Fainali ya mashindano yaliyo chini ya Shirikisho la soka Afrika CAF, ambapo mwaka 1993 walicheza fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika wakati huo yakijulikana kama kombe la washindi.
  • Simba kuvaana na RS Berkane katika michezo miwili ya Fainali ambayo imepangwa kupigwa kati ya Mei 17 na 25, mwaka huu.

Stellenbosch FC 0-0 Simba SC ‘Simba to the final’ ndivyo matokeo ya mwisho yaliyoonekana baada ya filimbi ya mwamuzi, huku Simba wakifuzu Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa matokeo ya jumla ya bao 1-0.

Simba wamefanikiwa kufuzu Fainali ya mashindano hayo kupitia mtaji wa bao 1-0 ambalo walilipata katika mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa Aprili 20, mwaka huu hapa Tanzania.

STELLENBOSCH FC 0-0 SIMBA SC ‘SIMBA TO THE FINAL’ MCHEZO ULIKUWAJE?

Stellenbosch FC 0-0 Simba SC, Simba to the Final
Ahoua na wachezaji wa Stellenbosch

Simba walioingia katika mchezo huo wakiwa na mtaji wa bao 1-0 walitumia sehemu kubwa ya mchezo Stellenbosch FC 0-0 Simba SC ‘Simba to the final’ leo kucheza kwa tahadhari na kulinda uongozi wao.

VAR yaamua mchezo

-----------------------------------------------n
VAR

Hakuna namna unaweza kuepuka kuuongelea mchezo wa leo wa Stellenbosch FC 0-0 Simba SC ‘Simba to the final’ bila kuitaja VAR, yaani ‘Video Assistance Referee’ ambayo kwa kiasi kikubwa ilifanikiwa kuamua matukio tata matatu makubwa.

Tukio la kwanza ni Penalti ya mapema ambayo waliipata Simba kipindi cha kwanza kupitia kwa nyota wao Kibu Denis kabla ya VAR kuikataa penalti hiyo.

Tukio la pili ni pale VAR ilipokataa Penalti ya wenyeji Stellenbosch dakika za mwanzoni mwa kipindi cha pili, kufuatia madai ya Chamou kuunawa mpira wa krosi ndani ya 18.

Tukio la tatu ni pale VAR ilipokataa bao la wenyeji Stellenbosch dakika za mwisho za kipindi cha pili baada ya kugundua uwepo wa ‘offside’ wakati wa ujenzi wa shambulizi hilo.

WANASIMBA WAFANYA SHANGWE UWANJA WA MOSES MABHIDA

Mara tu, baada ya kumalizika kwa mchezo huo, mashabiki wa Simba waliosafiri kutoka maeneo mbalimbali duniani, viongozi wa timu na wachezaji walionekana kufanya shangwe la furaha ndani ya Uwanja wa, Moses Mabhida ambao ulitumika kwa mchezo huo.

Ikumbukwe mchezo huo ulikuwa unafuatiliwa na mamilioni ya watu duniani hususani Watanzania na Waafrika Kusini kutokana na matokeo ya mchezo wa kwanza uliopigwa Tanzania na kumalizika kwa suluhu yaani 0-0.

KOCHA SIMBA ATOA TAMKO ZITO BAADA YA KUTINGA FAINALI

------------------------------------------------n
Wanasimba wakishangilia kufuzu fainali

Mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo Kocha Mkuu wa Simba, Fadlu Davids ameweka wazi kuwa walitarajia mchezo Stellenbosch FC 0-0 Simba SC ‘Simba to the final’ kuwa mgumu zaidi ya ule kwanza walioshinda bao 1-0 nyumbani Tanzania na ndicho kilichotokea.

Fadlu amesema waliwasoma wapinzani wao, Stellenbosch na kugundua ni timu ambayo haichezi kwa kumiliki mpira, lakini inafanya mashambulizi ya kushtukiza pamoja na kurusha mipira kuelekea golini jambo ambalo Simba inapaswa kuchukua tahadhari.

Akizungumzia kikosi chake, Fadlu amesema amefurahi kuona wachezaji wake walikuwa kwenye hali nzuri na kupambana kwa dakika zote 90, ambapo walijitahidi kutafuta bao la ugenini, huku wakiwa makini kwenye kuzuia wasiruhusu bao.

“Tulitarajia mchezo mgumu lakini malengo yetu yalibaki katika kuhakikisha tunavuka na kutinga fainali. Tulifahamu tunahitaji sare ya aina yoyote kama ikishindikana kabisa hata bila kufungana ili kufuzu na tumefanikiwa.

KOCHA SIMBA AUTAJA UBINGWA SHIRIKISHO AFRIKA

Kocha Fadlu amendelea kusema: “Kweli tuna furaha kubwa ya matokeo haya, lakini tunajua hii inakuja na wajibu mkubwa uliopo mbele yetu.

“Tunapaswa kufanyia kazi makosa tuliyokuwa tunafanya kuanzia hatua ya awali, makundi mpaka nusu nafurahi kuona yamepungua kwa kiasi kikubwa lakini tuna kazi kubwa kuelekea fainali.

KIKOSI CHA SIMBA KILICHOANZA MCHEZO WA LEO

Kama ilivyotarajiwa Simba haikuwa na mabadiliko makubwa ya kikosi katika mchezo Stellenbosch FC 0-0 Simba SC ‘Simba to the final’ kulinganisha na kile kilichocheza mchezo wa kwanza kama wazungu wasemavyo ‘Winning team never changes’ Kikosi cha Simba kilichoanza leo kilikuwa;

Camara, Kapombe Zimbwe Jr, Chamou, Hamza, Kagoma, Kibu Ngoma, Mukwala, Ahoua, Mpanzu.

SIMBA AFRIKA KUSINI KAMA BONGO

Licha ya kuwa ugenini Simba wametamba sana uwanjani leo na kujisikia kuwa nyumbani kutokana na sapoti kubwa ambayo wamepewa na Serikali, mashabiki wa timu hiyo waliosafiri na wale wanaoishi nchini humo.

Kulikuwa na mashabiki wengi ambao walijitokeza uwanjani kuisapoti Simba kiasi kwamba ungedhani mchezo Stellenbosch FC 0-0 Simba SC ‘Simba to the final’ unapigwa Tanzania.

DAKA HAYA MAMBO MUHIMU KUHUSU MCHEZO WA LEO STELLENBOSCH FC 0-0

Stellenbosch FC 0-0 Simba SC 'Simba to the Final'
Kikosi cha Simba

Stellenbosch FC 0-0 Simba SC ‘Simba to the final’, hii ni fainali ya pili katika historia ya Simba kucheza Fainali ya mashindano yaliyo chini ya Shirikisho la soka Afrika, ambapo mwaka 1993 walicheza fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika wakati huo likijulikana kama kombe la washindi.

Simba kuvaana na RS Berkane katika mchezo wa Fainali ambao umepangwa kupigwa kati ya Mei 17 na 25, mwaka huu.

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.