Kikosi cha Simba kikipokewa Afrika Kusini------------------------------------------------n
------------------------------------------------n (-)
Mapokezi Simba Sauz

  • Mechi ya marudiano Stellenbosch FC Vs Simba SC itapigwa Jumapili saa 10:00 jioni nchini Afrika Kusini.
  • Mchezo wa kwanza uliopigwa Tanzania uliisha kwa Simba kushinda bao 1-0
  • Rais Samia aiongeza mzuka Simba

Stellenbosch FC Vs Simba SC 27/4/2025 ni mchezo na habari kubwa ya soka wikiendi hii, ambapo Kikosi cha Simba kimetua rasmi Afrika Kusini Jumatano hii tayari kwa ajili ya maandalizi ya mwisho kuelekea mchezo huo, wa marudiano Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Stellenbosch. huku wakitamba kutinga fainali.

Stellenbosch Vs Simba utakaopigwa kwenye Uwanja wa Moses Mabhida ni mchezo unaotarajiwa kufuatiliwa zaidi kutokana na matokeo ya mchezo wa kwanza uliopigwa jijini Dar es Salaam.

KUTOKA ZANZIBAR, SAFARI IMEANZIA DAR ES SALAAM

Kikosi cha timu hiyo kilirejea jijini Dar es Salaam kutoka Zanzibar baada ya mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Stellenbosch ambao waliibuka na ushindi wa bao 1-0.

Baada ya kufika Dar es Salaam mchana wachezaji walipewa mapumziko ya saa chache na jioni walifanya mazoezi ya Gym kuweka miili sawa.

SIMBA YATENGA SIKU 6 ZA MAZOEZI

Mara baada ya kufika Dar es Salaam, kocha mkuu wa kikosi hicho, Fadlu Davis aliandaa program ya siku 6 kwa ajili ya kuvaana na Wasauz hao.

SIMBA SC Vs STELLENBOSCH FC MCHEZO WA KWANZA ULIKUWAJE?

Ahoua v Stellenbosch FC
Mpanzu v Stellenbosch FC

Wenyeji waliuanza mchezo kwa kasi na kutengeneza nafasi nyingi za kufunga lakini umaliziaji haukuwa mzuri huku Stellenbosch wakitumia muda mwingi kujilinda na kafanya mashambulizi ya kushtukiza.

Jean Charles Ahoua aliipatia bao hilo pekee dakika ya 45 baada ya kupiga mpira wa adhabu uliotinga wavuni moja kwa moja na kuwashinda walinzi wa Stellenbosch.

Kipindi cha pili Simba hatwakurudi kwa kasi kama ilivyokuwa cha kwanza, huku Stellenbosch nao wakipata nafasi ya kufanya mashambulizi ingawa wenyeji walikuwa imara kuwadhibiti.

Ahoua alipoteza nafasi nzuri ya kuipatia bao la pili dakika ya mwisho ya mchezo baada ya kumpiga hadi chenga mlinda mlango, Oscarine kufuatia pasi safi ya Mpanzu lakini mpira aliopiga ulitoka nje kidogo ya lango.

KIKOSI KILICHOCHEZA MCHEZO WA KWANZA

Kibu v Stellenbosch FC
Kibu v Stellenbosch FC

Camara, Kapombe Zimbwe Jr (Nouma 73′), Chamou (Mavambo 80′), Hamza, Kagoma, Kibu (Mutale 73′) Ngoma, Mukwala (Ateba 84′), Ahoua, Mpanzu

KOCHA SIMBA ANASEMAJE?

Kocha Mkuu wa Simba, Fadlu Davids amesema maandalizi ya mchezo wa marudiano yameenda vizuri na wanatarajia kufanya maandalizi ya mwisho Afrika Kusini.

Fadlu amesema kikosi kipo kwenye hali nzuri na tayari kimeanza kuzoea mazingira ya Afrika Kusini na malengo yao ni kuhakikisha wanafanya vizuri zaidi.

Fadlu ameongeza kuwa utakuwa mchezo mgumu kwakuwa hata Stellenbosch wanahitaji nafasi ya kufuzu na kutinga fainali lakini ametamba kuwa wapo tayari kwa vita ya dakika 90 na kufanikisha malengo yetu.

“Kikosi kipo kwenye hali nzuri, tunafahamu haitakuwa mechi rahisi lakini tupo ugenini na wenyeji wana faida yakuwa na mashabiki wao. Kikosi chetu kimezidi kuimarika siku hadi siku.

“Makosa tuliyokuwa tunafanya kuanzia hatua ya awali, makundi mpaka robo fainali yamepungua kwa kiasi kikubwa na tupo tayari kwa ajili ya malengo yetu kama timu ya kuvuka hatua hii.

“Hatupaswi kufanya makosa ambayo yanaweza kutugharimu, tunahitaji kucheza kwa umakini,” amesema Fadlu.

SIMBA YAPOKEWA KIBABE SAUZ, MABOSI WATOA TAMKO

------------------------------------------------n
Mapokezi ya Simba Sauz

Uongozi wa timu hiyo umetamba kuwa katika mechi hiyo ya marudiano itakayopigwa Jumapili Afrika Kusini ndio maana ya ‘Ama zetu ama zao’, ambapo wamepokewa na balozi wa Tanzania nchini Misri.

DONDOO MUHIMU STELLENBOSCH FC Vs SIMBA SC

Timu hizo mbili hazijawahi kukutana na Stellenbosch hivyo hii inakuwamara ya kwanza katika ezo wa leo ni wa kwanza kukutana na Stellenbosch

Katika historia ya timu hizi wote wamekutana kuanzia mchezo wa kwana ambao ulipigwa katika ardhi ya Zanzibar ikiwa ni mara ya kwanza kwetu kucheza mechi ya nusu fainali Visiwani humo.

Stellenbosch FC Vs Simba SC 27/4/2025
Kikosi Simba kuelekea mchezo Stellenbosch FC Vs Simba SC 27/4/2025

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.