Kamwe AliKamwe Ali
  • Clement Mzize kinara wa utupiaji mabao Yanga akiwa katupia mabao 13 anamtaja Ali Kamwe kuwa miongoni mwa watu ambao huzungumza naye mara kwa mara.
  • Yanga inashikilia rekodi yakuwa timu yenye mabao mengi ndani ya ligi msimu wa 2024/25 ikiwa imetupia mabao 68.
  • Wakali wawili kwenye kucheka na nyavu wapo ndani ya tatu bora katika mbio za kuwania tuzo ya ufungaji bora.

ALI Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga ameweka kuwa huwa anazungumza na wachezaji kuwapa siri za mabeki wa timu pinzani na mbinu mbalimbali ambazo anazijua.

Ali Kamwe
Ali Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga ambao ni vinara wa ligi msimu wa 2024/25. Source: Yanga.

Kamwe amebainisha kuwa kulinga na malengo ambayo yapo na kujua kwake mpira kunampa mwanga wakutambua aina ya wapinzani wao namna walivyo jambo ambalo likifanyika linawapa nguvu wachezaji kupata matokeo mazuri.

Yanga inayodhamiwa na SportPesa katika mechi 26 ilipata ushindi kwenye mechi 23 ikipoteza mechi mbili ilikuwa Yanga 0-1 Azam FC na Yanga 1-3 Tabora United, sare ni JKT Tanzania 0-0 Yanga. Safu ya ushambuliaji ni namba moja kwenye kutupia ikiwa na mabao 68.

Kwenye dakika 2,340  ina wastani wakufuga bao moja kila baada ya dakika 34 huku ukuta wao ukiwa na wastani wakuokota bao moja nyavuni kila baada ya dakika 234.

Bakari
Bakari Nondo nahodha wa Yanga ambaye ni beki katika kikosi hicho 2024/25. Source: Yanga.

Chini ya Dickson Job, Bakari Mwamnyeto, Ibrahim Bacca hawa wamekuwa wakiunda ukuta wa timu hiyo ambayo inaongoza ligi ikiwa kwenye mbio za kutetea ubingwa waliotwaa msimu wa 2023/24.

Ipo wazi kwamba timu ambayo imeokota mabao machache kwenye nyavu ndani ya ligi namba nne kwa ubora Afrika ni Simba chini ya Kocha Mkuu, Fadlu Davids. Watani haw awa jadi ni mabao 8 wamefungwa ambapo kipa namba moja ni Moussa Camara.

KUHUSU SIRI ZA MABEKI

Kamwe amebainisha kuwa kulingana na ushindani uliopo huwa anapata muda wa kuzungumza na wachezaji wa Yanga kuwapa taarifa mbalimbali zinazowahusu mabeki wa timu pinzani.

“Huwa ninafuatilia sana mechi zetu hivyo kuna vitu ambavyo ninakuwa ninavijua hasa kwa mabeki wa baadhi ya timu jambo ambalo linanifanya nizungumze na wachezaji kwa kuwaambia kwamba kwa beki huyu ukifanya hivi kitatokea hiki na ukifanya hivi itakuwa vile.

“Hii inasaidia kwa kuwa tupo kwenye vita na ninajua mpira kwa namna yake muda mwingi ninapokuwa na wachezaji tunazungumza kwa urafiki kabisa, malengo ni kuona kwamba tunapata ushindi kwenye mechi zetu.

VITA YA UFUNGAJI BORA YASHIKA KASI

Kwenye ligi Yanga wakiwa wanaongoza katika ufungaji wa mabao ambayo ni 68 kinara wa utupiaji wa mabao anatoka Yanga ni Clement Mzize mwenye mabao 13 anafuatiwa na Prince Dube mwenye mabao 12 naye yupo Yanga.

Dube
Dube Prince mshambuliaji wa Yanga mwenye mabao 12 ndani ya msimu wa 2024/25. Source: Yanga.

Ipo wazi kwamba msimu wa 2023/24 ni Aziz Ki wa Yanga aliibuka kuwa mfungaji bora alipotupia mabao 21 alifuatiwa na Feisal Salum wa Azam FC ambaye alifunga jumla ya mabao 19.

Mzize alifikisha mabao hayo 13 baada ya kufunga mabao mawili kwenye mchezo uliopita wa ligi Aprili 21 2025, Uwanja wa Tanzanite Kwaraa baada ya dakika 90 ubao ulisoma Fountain Gate 0-4 Yanga, Mzize alifunga  dakika ya 38 kwa mguu wa kulia akiwa ndani ya 18 baada ya makosa ya kipa John Noble kutema mpira wa faulo iliyopigwa na Aziz Ki.

Mzize alifunga bao jingine dakika ya 69 akitumia pasi ya Jonathan Ikangalombo akiwa ndani ya 18 akifikisha mabao 13 ndani ya ligi. Aziz Ki alipachika bao moja dakika ya 43 kwa mguu wa kushoto akiwa ndani ya 18 baada ya kipa John aliyekuwa ametoka ndani ya 18 kutoa pasi iliyokutana na Ki.

Kiungo ambaye alianzia benchi kwenye mchezo huo Clatous Chama alipachika bao moja kwa pigo la faulo dakika ya 89 akitumia mguu wa kulia. Hivyo walikomba pointi tatu mazima ugenini.

Mzize kwenye mchezo huo alihusika kwenye mabao matatu anafikisha mabao 13 ndani ya ligi akiwa kinara kwenye eneo la wakali wenye mabao mengi anafuatiwa na Prince Dube mwenye mabao 12.

KOCHA HESABU ZAKE BALAA

Kocha Mkuu wa Yanga, Miloud Hamdi ameweka wazi kuwa hesabu kubwa zilizopo ni kupata matokeo kwenye mechi ambazo wanacheza bila kutegemea mchezaji mmoja bali wote wanacheza kwa ushirikiano.

Hamdi Yanga
Hamdi Miloud, Kocha Mkuu wa Yanga inayoongoza ligi msimu wa 2024/25. Source: Yanga.

“Tukiwa uwanjani tunafanya kazi kwa ushirikiano kila mchezaji anatambua kuwa ambacho kinahitajika ni ushindi hivyo hakuna kuzembea kwenye mechi zetu ambazo tunacheza.

“Sipendi kulalamika ikiwa atakosekana mchezaji fulani kutokana na sababu fulani hapana kikubwa ni kuona kwamba hawa waliopo wanafanya kazi kwa umakini na ukiwa ndani ya Yanga kinachohitajika ni matokeo.”

Share this: