Fei TotoFei Toto
  • Yanga yaifunika Simba kwenye eneo la utupiaji mabao ndani ya ligi ikiwa namba moja msimu wa 2024/25.
  • Jonath Sowa wa Singida Black Stars usimchukulie poa licha ya kuingia dirisha dogo ana balaa huyo.
  • Ahoua wa Simba uchawi wake umejificha kwenye mguu wa kulia kafunga mabao 12

Ukiweka kando suala la vita yakuwania taji la Ligi Kuu Bara msimu wa 2024/25 ambao unazidi kushika kasi kuna suala la tuzo ya mfungaji bora ambayo nayo imeshika kasi kila kona wakali wakiwa kazini. Huku Clement Mzize wa Yanga na Jean Ahoua wakiwa ni miongoni mwa nyota wenye zali katika utupiaji.

Jean Ahoua (-)
Jean Ahoua kiungo mshambuliaji wa Simba mwenye mabao 12 msimu wa 2024/25. Source: Simba.

Ipo wazi kwamba msimu wa 2023/24 tuzo ya mfungaji bora ilikwenda kwa kiungo mshambuliaji wa Yanga, Aziz Ki ambaye alifunga jumla ya mabao 21 na alikuwa kwenye vita kali na kiungo mzawa Feisal Salum wa Azam FC ambaye msimu wake wa kwanza akiwa na uzi wa Azam FC aliamsha dude.

Feisal yeye alifunga jumla ya mabao 19 akiwa ni mzawa namba moja kufunga mabao mengi kwa msimu uliopita ambapo msimu huu wa 2024/25 katupia mabao manne pekee akiwa na deni kutimiza mabao 15 kufikia rekodi yake.

MGAWANYO MABAO YA KI NA FEI

Aziz Ki
Aziz Ki kiungo mshambuliaji wa Yanga aliyetwaa tuzo ya ufungaji bora 2023/24. Source: Yanga.

Katika mabao hayo 21 ya Ki wa Yanga alifunga jumla ya mabao 17 akitumia mguu wa kushoto na Feisal aligotea kufunga mabao 4, Feisal alikuwa namba moja kwa kutumia mguu wa kulia  alipofunga mabao 13 na Ki alifunga matatu pekee.

Nyota hawa wawili walikuwa wakali wakiwa ndani ya 18 ila Feisal alikuwa na hatari zaidi ambapo alifunga jumla ya mabao 17 akiwa kwenye eneo hilo ni Aziz Ki alifunga jumla ya mabao 15 akiwa ndani ya 18. Hivyo alizidiwa mabao mawili pekee kwenye ukali wa kutupia mabao ndani ya 18.

Nje ya 18 Aziz Ki alitupia mabao sita akiwa nje ya 18. Miongoni mwa timu aliyofunga akiwa nje ya 18 ilikuwa dhidi ya Tabora United alipofunga bao lake la 10 ndani ya ligi ilikuwa kwa pigo huru akitumia mguu wake wa kushoto.

KASI YA MSIMU WA 2024/25

Kasi ndani ya msimu mpya inazidi kuendelea ikiwa ni mzunguko wa pili unakaribia kugota mwisho kwa wababe wanaowania tuzo binafsi na timu kujulikana itakapokamilika 2024/25.

Clement Mzize ambaye alichaguliwa kuwa mchezaji bora kwenye mchezo uliopita dhidi ya Fountain Gate alicheka na nyavu mara mbili ilikuwa ni Aprili 21 2025 ubao wa Uwanja wa Tanzanite Kwaraa uliposoma Fountain Gate 0-4 Yanga.

Jonathan na Mzize
Jonathan Ikangalombo na Clement Mzize kinara wa kucheka wakucheka na nyavu akitupia mabao 13. Source: Yanga.

Yanga  ni vinara wa ligi wakiwa na jumla pointi 70 baada ya kucheza mechi 26 ambazo ni dakika 2,340 safu ya ushambuliaji imetupia jumla ya mabao 68 ikiwa na wastani wakuwa na hatari kila baada ya dakika 34 uwanjani.

Nyota mwingine mwenye mabao mengi ni Prince Dube wa Yanga ambaye ni msimu wake wa kwanza kuwa na uzi wa njano na kijani akitokea Azam FC alikokuwa na walipokutana na mabosi wake wa zamani kwenye Dar Dabi, Dube alifunga bao moja ubao wa Uwanja wa Azam Complex uliposoma Azam FC 1-2 Yanga bao la kwanza lilifungwa na Pacome.

SIMBA NYOTA WAO HUYU HAPA

Davids Fadlu
Davids Fadlu Kocha Mkuu wa Simba msimu wa 2024/25. Source: Simba.

Kutoka kikosi cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Fadlu Davids ni kiungo mshambuliaji Jean Ahoua katupia jumla ya mabao 12 huku uchawi wake ni mguu wa kulia akifunga yote. Simba kwenye msimamo ni nafasi ya pili safu yake ya ushambuliaji imetupia jumla ya mabao 52 ikiwa ni timu namba mbili kwenye kufunga mabao mengi.

Simba ni mechi 22 imeshuka uwanjani, ushindi kwenye mechi 18, sare tatu ilipoteza mchezo mmoja dhidi ya Yanga kwenye Kariakoo Dabi kwa ubao wa Uwanja wa Mkapa kusoma Simba 0-1 Yanga. Katika dakika 1,980 ina wastani wakufunga bao moja kila baada ya dakika 38.

SINGIDA BLACK STARS HAWAPOI

Wakali wanaoutumia Uwanja wa Liti kwenye mechi za ushindani wakiwa nyumbani, Singida Black Stars hawapoi kutokana na kuwa na mastaa wawili ambao wapo vizuri kwenye eneo la kucheka na nyavu.

Jonathan Sowa raia wa Ghana huyu ni namba moja katika kikosi hicho kilicho nafasi ya nne katupia mabao 11 ni ingizo jipya ndani ya kikosi cha Singida Black Stars ambacho kipo nafasi ya nne kwenye msimamo na pointi zake ni 53.

Elvis Rupia naye yupo ndani ya Singida Black Stars katupia mabao 10. Singida Black Stars imecheza mechi 27 ni pointi 53 zipo kibindoni.

Share this: