Kapombe ShomariKapombe Shomari

HII Tunavuka ya Simba imetimia baada ya dakika 180 kwenye mechi  mbili za hatua yar obo fainali kwa ushindi wa penati 4-1 dhidi ya Al Masry, Waarabu wa Misri.

Ni Simba inabaki kwenye anga la kimataifa katika hatua ya nusu fainali huku Yanga ya Tanzania inayodhaminiwa na SportPesa ikiwa na rekodi ya kutinga fainali ikigotea kuwa mshindi wa pili.

DAKIKA 45 BALAA

Mukwala Steven
Mukwala Steven akishangilia moja ya bao alilofunga kwenye Hii Tunavuka, Uwanja wa Mkapa dhidi ya Al Masry, Uwanja wa Mkapa. Source: Simba.

Dakika 45 za kwanza zilikamilika kwenye mchezo wa kimataifa hatua ya robo fainali Kombe la Shirikisho Afrika katika kutafutwa tiketi ya kutinga hatua ya nusu fainali kwa wababe wawili hao kuwa ni faida kwa Simba kupata mabao ya kuongoza.

Ubao wa Uwnja wa Mkapa ulikuwa unasoma Simba 2-0 Al Masry huku Al Masry wao kwenye mchezo wa ugenini Aprili 2 2025 baada ya dakika 90 ilikuwa Al Masry 2-0 Simba

WATUPIAJI WA SIMBA KWA MKAPA

Ndani ya dakika 45 Simba ilipata mabao mawili kupitia kwa Ellie Mpanzu dakika ya 22 na Steven Mukwala dakika ya 32. Mpanzu alipachika bao hilo kwa mguu wa kulia akiwa nje ya 18 kwa mguu wa kulia na Mukwala alikuwa ndani ya 18 kwa pigo la kichwa akitumia pasi ya Mohamed Hussen Zimbwe Jr.

Mukwala alianza kikosi cha kwanza kwenye mchezo wa leo akimuweka benchi Leonel Ateba ambaye alianza katika mchezo wa robo fainali ya kwanza nchini Misri.

DAKIKA 15 ZAMOTO

Katika dakika 15, Jean Ahoua alikosa nafasi ya wazi dakika ya 5 akiwa ndani ya 18 baada ya pigo lake kwenda nje ya lango, kona tatu Simba wamepiga kupitia kwa Ellie Mpanzu, dakika ya 2,11,14, 18, 23, 45 na Ahoua alipiga kona dakika ya 26.

Kona zote hizo hazikuwa na faida kwa Simba kwa kuwa wapinzani Al Masry waliokoa na kuongeza mashambulizi kuelekea kwa Simba na langoni alianza Moussa Camara aliyekuwa na kumbukumbu zakufungwa mabao mawili nchini Misri.

Gad
Gad mlinda mlango wa Al Masy kwenye majukumu yake mbele ya Simba, Uwanja wa Mkapa. Source: Simba.

Ni dakika ya 24 na 28 Camara aliokoa hatari ambazo zilikwenda kwenye lango la Simba ndani ya dakika 45 za mwanzo ambazo zilikuwa na ushindani mkubwa mwanzo mwisho, huku Mpanzu akiwa katika ubora kwenye majaribio yake ya mipira akiwa nje ya 18.

Ni dakika ya 28 na 45 Mpanzu mashuti yake yalikwenda nje ya lango la Al Masry ambao walianza kwa kujilinda zaidi ndani ya dakika 45 za mwanzo kwa kuwa walikuwa na faida ya mabao mawili waliyopata katika mchezo wa nyumbani.

Mchezaji wa kwanza kuonyesha kadi ya njano alikuwa ni Abdlahim wa Al Masry dakika ya 44 huku nyota wa Al Masry Mido akiwa ni miongoni mwa wachezaji waliokuwa wakifanya kazi kubwa kulinda ngome yao.

KIPINDI CHA PILI

Kipindi cha pili Al Masry walianza kwa kasi ili kutafuta bao la ugenini ambapo mashambulizi yao yalikuwa ni yakushtukiza kulifuata lango l Moussa Camara ambapo Simba bado hesabu zao ilikuwa ni hii tunavuka.

Simba walijibu mashambulizi dakika ya 47 kupitia kwa Jean Ahoua ambaye shambulizi lake lilizuiwa na mlinda mlango wa Al Masry huku akionekana alichezewa faulo na nyota wa Al Masry.

Tukio hilo lilifanya VAR itoea maamuzi kwamba haikuwa ni faulo bali sehemu ya mchezo kwa wababe hao wawili ndani ya uwanja katika kusaka matokeo chanya.

Ahoua alipiga faulo dakika ya 47 ambayo ilisababishwa na Kibu Dennis aliyechezewa faulo na nyota wa Al Masry Makhlouf aliyeonyeshwa kadi ya njano na mwamuzi wa mchezo ikiwa ni kadi ya njano ya pili kwa Al Masry.

Pigo hilo alitumia mguu wa kulia akiwa nje ya 18 liligonga mwamba wa Al Masry ikiwa ni miongoni mwa faulo iliyokuwa na hatari kwenye mchezo huo kutoka kwenye miguu ya Ahoua.

Steven Mukwala alichezewa faulo dakika ya 67 huku Shomari Kapombe akichezewa faulo dakika ya 66, 79 akisababisha kadi ya njano kwa Gaber wa Al Masry dakika ya 80 ya mchezo huo.

WALIOFUNGA PENATI ZA SIMBA

Ahoua v Al Masry
Ahoua kiungo mshambuliaji wa Simba alianza kupiga penati ya kwanza dhidi ya Al Masry, Uwanja wa Mkapa.Source: Simba.

Kipa Camara aliokoa penati ya kwanza ya Al Masry iliyopigwa na Mido ikawapa nguvu Simba kufunga penati zao ambapo mpigaji wa kwanza alikuwa ni Jean Ahoua, Steven Mukwala alifuata, Kibu Dennis alikuwa wa tatu na penati ya nne ilipigwa na Shomari Kapombe ambaye alifunga.

Ikumbukwe kwamba Kapombe dakika ya 90 kwenye mchezo alikosa nafasi ya kufunga baada ya pasi aliyopewa na Mpanzu kwenda nje kidogo ya lango.

KIKOSI CHA SIMBA KILICHOANZA

Fabrince
Fabrince Ngoma kiungo wa Simba ambaye alianza kikosi cha kwanza dhidi ya Al Masry, Uwanja wa Mkapa. Source: Simba.

 Moussa Camara, Chamou, Jean Ahoua, Steven Mukwala, Shomari Kapombe.
 Hamza Jr, Mohamed Hussen, Yusuph Kagoma,Ellie Mpanzu, Kibu Dennis, Fabrince Ngoma.
Wachezaji wa akiba ni Ally Salim, Duchu, Nouma, Edwin Balua, Chasambi Ladack, Mavambo, Awesu, Mutale, Ateba

Share this: