
Simba Vs Al Masry ni mchezo wa kufa na kupona leo unaotarajiwa kupigwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa ambapo Kocha Mkuu wa Simba, Fadlu Davids amesema katika kipindi cha wiki nzima tangu kikosi kirejee kutoka Misri amewandaa wachezaji kufunga mabao ili kufanikiwa kufuzu nusu fainali Kombe la Shirikisho Afrika.
Fadlu amesema kwa kuwa wanahitaji kufunga mabao matatu ili kuweza kufuzu nusu fainali, lakini amewaandaa wachezaji kuhakikisha wanafunga zaidi ya mabao manne. Fadlu ameongeza kuwa Simba ni Klabu kubwa Afrika na inataka mafanikio yakiwemo kutinga nusu fainali na ikishindikana atakuwa tayari kuwajibika.
“Tunahitaji mabao matatu ili kufuzu nusu fainali na hii wiki nzima tumefanya mazoezi walau tufunge mabao zaidi ya manne na sio matatu pekee,” amesema Fadlu.
WACHEZAJI SIMBA WATANGAZA WAPO TAYARI KUANDIKA HISTORIA

Akizungumza kwa niaba ya wachezaji nahodha wa timu, Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr’ amesema kila mmoja yupo tayari kuhakikisha anakuwa sehemu ya kikosi kitakachoandika historia ya kuipeleka timu nusu fainali.
“Tukiwa na wachezaji wageni tunawaambia kuwa kufika robo fainali sio mafanikio kwakuwa sisi tushafanya mara nyingi ila wanatakiwa kuhakikisha tunasaidiana kutoka hapa na kuifikisha timu nusu fainali,” amesema Zimbwe Jr.
SEMAJI LA SIMBA AHMED AOMBA MASHABIKI KUJAZA UWANJA

Meneja Habari na Mawasiliano wa Klabu, Ahmed Ally amewaomba mashabiki kujitokeza uwanjani kesho katika mchezo wa marudiano wa robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Al Masry utakaopigwa Benjamin Mkapa saa 10 jioni.
Ahmed amesema ameyasema hayo muda mfupi baada ya kuzindua Tawi la Simba Azimio, Tandika ambapo amesema mchezo wa leo ni muhimu kwa kila Mwanasimba hivyo wanapaswa kuhakikisha tunafanikiwa kutinga nusu fainali.
Ahmed amesema itakuwa jambo la ajabu kwa mashabiki kutoka Tunduma, Mwanza, Mbeya na mikoa mingine kuja uwanjani wakati watu kutoka Temeke wapo majumbani wanatazama kupitia luninga.
“Kila zama ina kitu cha kujivunia, sisi wa zama za sasa tunatakiwa kuipeleka Simba nusu fainali ya Kombe la Shirikisho. Imetosha kujivunia historia ya mwaka 1993 na 2003 sasa ni wakati wa kuipeleka Simba nusu fainali na ‘hii tunavuka’,” amesema Ahmed.
Ahmed ameongeza kuwa “Ni wakati wa sasa wa kuandika historia yetu ili tujivunie. Na wenzetu wa zamani kuna kazi kubwa waliifanya ili kufanikiwa, na moja ya kazi hiyo ni kuujaza Uwanja wa Uhuru na mashabiki waliingia saa mbili asubuhi, sisi kesho tunaenda kuandika historia yetu.”
MZEE MANGUNGU NAYE ATOA TAMKO

Mwenyekiti wa Klabu hiyo, Murtaza Mangungu ameweka wazi kuwa pamoja na kupoteza mchezo wa mkondo wa kwanza wa robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika ugenini, bado hawana presha wala hofu ya kutinga nusu fainali kwa kuitoa Al Masry leo Jumatano.
Mangungu amesema katika Uwanja wa Benjamin Mkapa haujawahi kushindwa jambo na kupitia umoja na mshikamano wao, hakuna namna Al Masry wataweza kuepuka kipigo, kikubwa mashabiki wajitokeze kwa wingi uwanjani.
WAZIRI AWESO MGENI RASMI UWANJA WA MKAPA

Simba kupitia kwa Meneja Habari na Mawasiliano wa timu hiyo, Ahmed Ally umetangaza kuwa katika mchezo huo wanatarajia Waziri wa Maji Mhe. Juma Aweso kuwa Mgeni rasmi katika tukio hilo.
Pamoja na Aweso Uongozi wa Simba umetangaza kufanya mawasiliano na baadhi ya viongozi wakubwa na watu mashuhuri akiwemo Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia ili waweze kuwa wageni Maalum katika mchezo huu.

Ahmed ameyasema hayo katika matukio mbalimbali wakati wa ufunguzi na matukio mbalimbali ya hamasa kuelekea mchezo huo, ambazo zilifanyika katika maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam na kuzinduliwa Mbezi Shule Sokoni, zikiwa na lengo la kuwataka mashabiki wao kujitokeza kwa wingi uwanjani kuipa sapoti timu ili kuweza kupata nafasi ya kufuzu nusu fainali ya michuano hiyo.
Ahmed ameongeza kuwa sababu ya kumualika Rais Karia ni kumpa heshima na kuthamini mchango wake katika kuleta maendeleo ya soka nchini pamoja na Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA).
“Tunategemea Rais wa TFF, Wallace Karia atakuwa mgeni Maalum kwenye mchezo wetu wa marudiano dhidi ya Al Masry. Ametenda mengi kwenye mpira Tanzania na mafanikio tuliyonayo Simba Kimataifa yametokana na uimara wake.
“Simba tunatambua, tunathamini na kuheshimu mchango wa Rais Karia, leo kufikia nafasi ya sita kwenye viwango vya ubora Afrika ni kutokana na uongozi wake thabiti hivyo hatuna budi kumpa heshima hii ya kipekee na kumualika kuwa mgeni maalum wa mchezo wetu dhidi ya Al Masry siku ya Jumatano,” amesema Ahmed.
SHINDA MAMILIONI NA SPORTPESA

Kumbuka unaweza kushinda mamilioni kwa kubashiri matokeo ya mchezo huu na michezo mingine kupitia Kampuni bora ya michezo ya kubashiri ya SportPesa kwa kutembelea www.sportpesa.co.tz

