Issa MbuziIssa Mbuzi
  • Yanga iliipiga mkono Fountain Gate Desemba 29 2025 kwa ushindi wa mabao 5-0 Uwanja wa KMC Complex.
  • Fountain Gate ni namba mbili kwa timu iliyofungwa mabao mengi ambayo ni 47 kwenye ligi baada ya mechi 26.
  • Yanga ni namba moja kwa timu yenye mabao mengi ndani ya ligi ambayo ni 64 baada ya mechi 25.

FOUNTAIN Gate v Yanga ambazo zinashiriki Ligi Kuu Tanzania Bara namba nne kwa ubora zimetambia kuelekea mchezo wao unaotarajiwa kuchezwa Aprili 21 2025 Uwanja wa Tanzanite, Kwaraa kwa kila mmoja kupigia hesabu pointi tatu za mpinzani hivyo hatumwi mtoto dukani dakika 90 mpaka zigote mwisho.

Fountain Gate inayodhaminiwa na SportPesa kupitia kwa Ofisa Habari Issa Mbuzi wamebainisha kuwa wamepata mbinu za wapinzani wao hivyo wanajua namna watakavyofanya kazi kuwadhibiti ndani ya dakika 90 kwenye mchezo wao wa ligi.

Kulandana
Kulandana kiungo wa Fountain Gate 2024/25. Source Fountain Gate.

Ipo wazi kwamba katika mzunguko wa kwanza, Fountain Gate iliacha pointi tatu mazima Uwanja wa KMC Complex kwa kupigwa mkono wa mabao 5-0 hivyo ni mchezo ambao utakuwa ni kisasi kwa Fountain Gate na Yanga hesabu ni kulinda ushindi wao.

Ikumbukwe kwamba wababe hawa wawili wote wanadhaminiwa na SportPesa hivyo mashabiki watakuwa wanashuhudia burudani kutoka kwa timu na mkeka ukisoma mkwanja unaingia kwenye simu kiulaini.

REKODI ZA WABABE HAWA

Fountain Gate ni namba mbili kwa timu ambazo zimeruhusu mabao mengi ndani ya ligi ambayo ni 47 baada yakucheza mechi 26 ikiwa nafasi ya 9 na pointi zake kibindoni ni 29.

Safu ya ushambuliaji ya Fountain Gate imefunga jumla ya mabao 29 ilipata ushindi kwenye mechi 8 huku ikipoteza 13 nakuambulia sare 5 kwenye hizo sare miongoni waliwabana mbavu watani wa jadi wa Yanga, Simba ubao uliposoma Fountain Gate 1-1 Simba.

Katika dakika 2,340 ni wastani wa kila dakika 80 kufunga bao na kila baada ya dakika 49 timu hiyo ina wastani wakuokota mpira kwenye nyavu zake ndani ya mechi za ligi msimu wa 2024/25.

HAWA HAPA YANGA

Yanga ni vinara ndani ya Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya mechi 25 ni pointi 67 wamekusanya kibindoni na safu ya ushambuliaji imetupia jumla ya mabao 64 ikiwa ni safu kali kwenye kumalizia nafasi ambazo zinatengenezwa ndani ya uwanja kwenye ligi.

Dube Prince (-)
Mchezo uliopita kwa Yanga kwenye ligi ilikuwa Dar Dabi dhidi ya Azam FC, Uwanja wa Azam Complex. Source: Yanga.

Kwenye dakika 2,225 ina wastani wakufunga bao moja kila baada ya dakika 35 huku ukuta ukiwa na wastani wakuokota bao nyavuni kila baada ya dakika 225 kwenye mechi za ushindani wakiwa uwanjani kutimiza majukumu yao.

Ukuta wake ni namba mbili ndani ya ligi kuruhusu mabao machache ambayo ni 10, timu namba moja kwenye ligi ambayo imeruhusu mabao machache zaidi kwa sasa ni Simba ikiwa imetunguliwa mabao 8 na yote aliyetunguliwa ni kipa Moussa Camara.

Yanga ilipata ushindi kwenye mechi 22, ilikubali sare dhidi ya JKT Tanzania 0-0 Yanga na mechi mbili ilipoteza dhidi ya Azam FC na Tabora United. Wababe hawa wawili ambao walikomba pointi tatu dhidi ya Yanga kwenye mzunguko wa pili walilipa kisasi.

Yanga ilipokutana na Tabora United ugenini ilipata ushindi wa mabao 3-0 na ilipokutana na Azam FC ilipata ushindi wa mabao 2-1. Ni mchezo wao wa ligi dhidi ya Azam FC waliruhusu bao moja langoni akiwa Djigui Diarra ambaye ni chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, Miloud Hamdi.

WATAKOSEKANA KWA YANGA

Khalid Aucho huyu alipata maumivu kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Coastal Union uliochezwa Uwanja wa KMC Complex. Alikosekana kwenye mchezo dhidi ya Azam FC ambao ulikuwa ni Dar Dabi Uwanja wa Azam Complex na dhidi ya Stand United ambao ulikuwa ni CRDB Federation Cup.

Aucho Hsp
Khalid Aucho, kiungo wa Yanga huenda akakosekana kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Fountain Gate, Aprili 21 kwa kuwa hayupo fiti. Source: Yanga.

Mbali na Aucho, Pacome alikosekana kwenye mchezo dhidi ya Stand United huku Ibrahim Bacca aliyepata maumivu mchezo dhidi ya Stand United ripoti ya madaktari itaamua.

TAMBO ZA WASEMAJI

Issa Mbuzi, Ofisa Habari wa Fountain Gate amesema kuwa wanatambua ubora wa Yanga ulipo na udhaifu kwa kuwa waliwatazama kwa ukaribu kwenye mchezo dhidi ya Stand United uliochezwa Uwanja wa KMC, Complex, Aprili 15 2025 na ubao ukasoma Yanga 8-1 Stand United.

Mbuzi
Issa Mbuzi, Ofisa Habari wa Fountain Gate itakayokutana na Yanga, mchezo wa ligi.Source: Fountain Gate.

“Tunawatambua vizuri hawa Yanga na kwenye mchezo wao dhidi ya Stand tulikuwa na wataalamu wakusoma mbinu zaidi ya wanne, wameniambia wameona namna itakayotupa matokeo kwenye mchezo wetu Aprili 21 tukiwa nyumbani.

Ali Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga amesema kuwa kila mchezo ulipo mbele kwao ni fainali na malengo ni kupata pointi tatu muhimu. “Kila mchezo ambao upo mbele yetu kwetu ni fainali na malengo ni kupata pointi tatu muhimu, wachezaji wapo tayari na tunaamini tutatoa burudani.”

Share this: