Huku Ligi Kuu Bara ikisimama kwa muda kupisha ratiba ya michezo ya kusaka tiketi ya kufuzu mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON), uongoziwa Simba ambao ni wawakilishi pekee wa Tanzania katika mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika wameanza rasmi maandalizi ya mchezo wao wa kwanza wa hatua ya makundi ya mashindano hayo.
Simba ambao wamewahi kula udhamini wa Kampuni bora ya michezo ya kubashiri ya SportPesa wamepangwa kundi A la mashindano hayo wanatarajia kuanza mchezo wao wa kwanza Novemba 27, mwaka huu katika uwanja wa Mkapa pale watakapovaana na Bravos kutokea nchini Angola.

Bravos ambao katika hatua ya mtoano waliwaondosha Uhamiaji kutokea visiwani Zanzibar, watakabiliwa na kibarua kigumu cha kuvaana na Simba ambayo mara ya mwisho kushiriki mashindano hayo walitolewa kwenye hatua ya robo fainali kwa changamoto ya mikwaju ya penalti dhidi ya Orlando Pirates ya Afrika Kusini.
Hatua hiyo ilifikiwa mara baada ya Simba na Orlando kutoa sare ya bao 1-1 ambapo kila timu ilishinda mchezo wa nyumbani kwao.
MASTAA SIMBA WAPEWA SIKU NNE ZA MAPUMZIKO
Baada ya kufanikiwa kuibuka na ushindi muhimu wa mabao 4-0 dhidi ya KMC, kikosi cha Simba kimepewa mapumziko ya siku nne kabla ya kurejea tena na kuanza kujiandaa na mchezo huo wa Kombe la Shirikisho Afrika.
Mchezo Vs KMC ulikuwaje?

Kwenye mchezo huo ambao ulipigwa kwenye dimba la KMC Complex Simba wameibuka na ushindi wa mabao 4-0 ambapo ushindi huo umewafanya warejee kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya NBC kwa mara ya pili msimu huu.
Ni kiungo mshambuliaji, Awesu Awesu ndiye aliyeipatia bao la kwanza dakika ya 25 kwa shuti kali akiwa ndani ya 18 baada ya kupokea pasi ya, Steven Mukwala. Mara baada ya bao hilo Simba waliendelea kulisakama lango la KMC na Jean Charles Ahoua alifanikiwa kuipatia bao la pili kwa mkwaju wa penati dakika ya 36 baada ya mlinzi, Shomari Kapombe kufanyiwa madhambi ndani ya 18.
Edwin Balua aliipatia bao la tatu dakika ya 66 Kwa shuti kali ndani ya 18 lilomshinda mlinda mlango wa KMC, Fabien Mutombora baada ya kupokea pasi kutoka kwa Valentine Nouma. Dakika mbili baadae, Ahoua aliifungia bao la nne baada ya Kutumia vizuri makosa ya Mlinzi wa KMC, Ismail Gambo.
AHOUA MCHEZAJI BORA WA MECHI
Katika mchezo huo ambao kocha, Fadlu Davids alifanya mabadiliko ya kuwatoa Awesu Awesu, Debora Fernandes, Ladaki Chasambi, Karaboue Chamou na Fabrice Ngoma kuwaingiza Omary Omary, Mzamiru Yassin, Edwin Balua, Kibu Denis na Hussein Kazi ni staa wa Ivory Coast, Ahoua ndiye alichaguliwa nyota bora wa mchezo baada ya kuhusika kwenye mabao mawili pamoja na kuonyesha kiwango safi.
Ushindi huo umewafanya Simba kufikisha pointi 25 baada ya kucheza mechi 10.
WATANO SIMBA WAITWA STARS

Kuielekea ratiba hiyo ya michezo ya AFCON, nyota watano kutoka katika kikosi cha, Fadlu ni miongoni mwa wachezaji 26 walioitwa na Kocha, Hemed Morocco kwa ajili ya mchezo wa kufuzu fainali za Afrika (AFCON), dhidi ya Ethiopia na Guinea.
Stars ina mechi mbili muhimu ambazo ikishinda itajihakikishia tiketi ya kushiriki michuano ya AFCON ambayo itafanyika nchini Morocco Januari 2025. Nyota hao walioitwa ni mlinda mlango, Aishi Manula, walinzi Shomari Kapombe, Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr’ na Abdulrazack Hamza.
Mwingine aliyejumuishwa kwenye kikosi hicho akiwa ni kiungo mshambuliaji, Kibu Denis. Kikosi cha Stars tayari kipo kambini kujiandaa na mechi hizo ambapo ya kwanza itakuwa ugenini dhidi ya Ethiopia Novemba, 16 na kumaliza nyumbani dhidi ya Guinea Novemba, 19.
SIMBA YA MECHI 10, FADLU ANAIONAJE?
Katika kikosi hiki cha raia huyu wa Afrika Kusini ameelezea mambo matatu makubwa;
- Anasema yupo kwenye Episode ya pili kwenye ujenzi wa hii timu, baada ya utimamu wa kimwili wa wachezaji kwasasa amehamia kwenye ‘tactical make up’ yaani suala la mifumo, kifupi mpaka sasa bado anajaribu kila kijana kuona nani anafit wapi na mfumo upi unafaa.
- Kocha, Fadlu mpira ametumia wachezaji wote waliosajiliwa na Simba msimu huu wa 2024/25 kasoro, David Kameta Duchu pekee, yaani kila Mchezaji wa ndani amemtumia na kila mmoja amepata dakika za kuonesha ubora wake, hakuna timu nyingine iliyofanya zaidi yake yeye.
- Timu inaongoza ligi, mpira unapigwa wa maana sana ila yeye anadai yupo kwenye 40% ya Episode hii ya pili, yaani Simba inachokifanya sasa ni kikubwa ila yeye bado anaona timu haijafika pale anapotaka kwakuwa bado ana kundi kubwa la Wachezaji vijana na timu ni mpya.

