SIMBA YATUA DODOMA KIBABE, KAGOMA, MUTALE, MZAMIRU KUKOSEKANA

ByJoel Thomas

September 28, 2024
Simba walivyotua DodomaSimba walivyotua DodomaSimba walivyotua Dodoma
SIMBA
Augustine Okejepha

KIKOSI cha Simba leo Jumamosi tayari kimewasili jijini Dodoma kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya mchezo wao wa kesho Jumapili dhidi ya Dodoma Jiji.

Simba ambao mpaka sasa wamefanikiwa kuandikisha asilimia 100 ya ushindi baada ya kufanikiwa kuvuna pointi 9 katika michezo yao mitatya awali wanauendea mchezo huoi muhimu wakiwa na kumbukujmbu nzuri ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Azam katika mchezo uliopigwa juzi Alhamisi visiwani Zanzibar.

Ikumbukwe kikosi cha Simba kimerejea Dar es Salaam jana Ijumaa kutokea Zanzibar.

MCHEZO DHIDI YA AZAM ULIKUWAJE?

SIMBA
Denis Kibu akipambana na kipa wa Azam

Huu ulikuwa mchezo wa tatu kwa Simba kwenye Ligi Kuu Bara ambapo ulipigwa kwenye Uwanja wa New Amaan Complex Visiwani Zanzibar na kushuhudia Simba wakiibuka na ushindi wa mabao 2-0. Mchezo huo ulianza kwa kasi ambapo timu zote zilikuwa zikishambuliana kwa zamu huku Simba wakionekana kuunda mashambulizi ya hatari zaidi.

Juhudi za Simba zilizaa matunda baada ya straika, Leonel Ateba kufanikiwa kuipatia bao la kwanza dakika ya 15 kwa shuti kali la mguu wa kushoto baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa, Jean Charles Ahoua.

Bao hilo lilidumu mpaka mapumziko ambapo Simba walirejea tena na kasi kubwa kipindi cha pili na kufanikiwa kupata bao la pili kupitia kwa kiungo wao, Fabrice Ngoma dakika ya 47 ya mchezo kufuatia mpira wa adhabu uliopigwa na Ahoua kuunganishwa kwa kichwa na Kibu Denis na kuokolewa na mlinda mlango Mustafa Mohamed kabla ya kumkuta mfungaji.

Licha ya timu zote kushambuliana kwa zamu, lakini mpaka dakia 90 zinamalizika ni Simba ndio walifanikiwa kuzoa pointi zote tatu.

Ushindi Huo uliifanya Simba kufikisha pointi tisa baada ya kucheza mechi tatu huku tukifunga mabao tisa  na wakiwa hawajaruhusu nyavu zao kuguswa. Katika mchezo huo pia Simba hawakupata majeruhi yoyote, hivyo wachezaji wote walishiriki mazoezi ya mwisho kujiandaa dhidi ya Dodoma.

KIKOSI CHA SIMBA KILICHOANZA MCHEZO HUO

X1: Camara, Kapombe Zimbwe Jr Che Malone Hamza, Ngoma, Kibu (Kijili 72′), Fernandez (, Ateba (Mukwala 63′), Ahoua (Awesu 63′), Mutale (Balua 63′)

SIMBA
Mastaa wa Simba wakipata mapumziko baada ya mechi na Azam

YANGA NAO KINAWAKA KESHO CHAMAZI

SIMBA
Kocha, Miguel Gamondi

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, Yanga wanaodhaminiwa na Kampuni bora ya michezo ya kubashiri ya SportPesa chini ya Kocha wao Mkuu, Miguel Gamondi nao kesho Jumapili wanatarajia kushuka uwanjani kuvaana na KMC katika mchezo wa ligi ambapo kocha wao ametamba kuibuka na ushindi.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kocha Gamondi amesema: “Tupo vizuri na tuna motisha ya kuelekea mchezo wetu wa kesho dhidi ya KMC timu ambayo inapenda kucheza soka safi kama sisi kwahiyo tunatarajia kuwa na moja ya Mechi nzuri sana.

“Tunafahamu hautakuwa mchezo mwepesi kwakuwa wenzetu nao watafanya Jitihada ili wapate ushindi lakini tupo hapa kwaajili ya kupambana na tunaamini tutawaheshimu na tutafanya vizuri. Mara zote nasema yaliyopita huwa yamepita, kila mechi huja tofauti, msimu uliopita tulicheza nao Chamazi na Morogoro hivyo utakuwa mchezo tofauti japokuwa tuna uzoefu wa kucheza nao na kwangu mimi napenda kufunga Magoli mengi na kutengeneza nafasi nyingi lakini sote tunatambua kuwa jambo la muhimu kabisa kesho ni kupata Alama tatu.”

REKODI YA MAGOLI KIPENGELE YANGA

wametibua rekodi yao ndani ya dakika 180 kwenye mechi Licha ya maboresho makubwa kwenye safu ya ushambuliaji Yanga, lakini kocha wa timu hiyo ameonekana kutoridhishwa na kasi ya ufungaji wa mabao ambayo imeshinda kufikia rekodi yao ya msimu uliopita.

Ikumbukwe kwamba msimu wa 2023/24 chini ya Gamondi, Yanga iliondoka na pointi sita kwenye mechi mbili za mwanzo huku safu ya ushambuliaji ikifunga jumla ya mabao 10 ikiandika rekodi ya kuwa timu ya kwanza kwenye msimu kufunga mabao mengi uwanjani kwenye mechi za ligi.

Katika michezo miwili ya kwanza Yanga walizifunga KMC 5-0 kabla ya kuwabamiza Kagera Sugar kwa idadi hiyo ya mabao katika mchezo wa pili ambao ulikuwa dhidi ya JKT Tanzania mechi zote zikipigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Dar esa Salaam.

 

Share this:

ByJoel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.