Mutale SGRMutale SGR

MZIZIMA Dabi inanukia ambapo Azam FC itawakaribisha Simba kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara mzunguko wa kwanza unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa New Amaan Complex Septemba 26 2024 huku kila timu ikitamba kukomba pointi tatu za mpinzani wake baada ya dakika 90.

Mechi za Ligi Kuu Bara, Ligi Kuu England kuna mikeka yake ambayo ipo SportPesa hivyo ni muda wako kutengeneza mkeka na kuvuna mkwanja wako chap kwa haraka.

FADLU Davids
KOCHA Mkuu wa Simba 2024/25 Fadlu Davids. Source: Simba.

Ikumbukwe kwamba msimu wa 2024/25 Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Fadlu Davids ni mechi mbili imecheza ndani ya ligi ambazo ni dakika 180 na kupata ushindi kwenye mechi zote hizo huku Azam FC ikicheza mechi nne ambazo ni dakika 360, ushindi ni kwenye mechi mbili na iliambulia sare kwenye mechi mbili.

Mchezo uliopita kwa Azam FC ilikuwa nyumbani Uwanja wa Azam Complex baada ya dakika 90 ubao ulisoma Azam FC 1- Coastal Union hivyo walikomba pointi tatu kwenye mchezo wa pili mfululizo baada ya ule wa kwanza kupata ushindi dhidi ya KMC wa mabao 4-0 uliochezwa Uwanja wa KMC, Complex.

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba ameweka wazi kuwa hawana hofu na wapinzani wao Azam FC kikubwa ni utayari na wanahitaji pointi tatu muhimu. Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Septemba 26 2024.

“Tunakwenda kwenye mchezo wetu tukiwa na ari ya kutafuta ushindi hatuna hofu kuwakabili wapinzani wetu na tunatambua ni timu nzuri lakini tunakwenda kukabiliana nao ili kupata pointi tatu muhimu uwanjani hatuna mashaka na hilo na mchezo utakuwa mzuri.”

SEMAJI LA AZAM FC HILI HAPA

Ibwee
Ibwee Hasheem, Ofisa Habari wa Azam FC, 2024/25. Source: Azam FC.

Wakati Simba wakitamba kuvuna pointi tatu kwenye mchezo huo Ofisa Habari wa Azam FC, Hasheem Ibwe ameweka wazi kuwa wanatambua umuhimu wa mchezo huo wataendelea na dozi yao ileile kwa wapinzani wao na lengo ni kuchukua pointi tatu muhimu.

“Mwendo wetu ni uleule kwa wapinzani wetu hakuna kufikiria kwamba kutakuwa na kurudi nyuma, tunasonga mbele kwa ajili ya kupata matokeo mazuri, yale ambayo yalipita tumesahau na sasa ni hesabu kupata pointi tatu muhimu kwenye mechi ambazo tunacheza.

“Tutacheza na Simba hakika ni mchezo mzuri na kikubwa ambacho tunawaambia wapinzani wetu wajishikilie wakija bila gadi tutagawa dozi bila idadi. Tunawaheshimu wapinzani wetu hilo halifichiki ila kwenye suala la ushindi nadhani hata wenyewe wanajua namna tulivyo imara.”

YANGA KIBARUANI LEO

VIUNGO wa Yanga
VIUNGO wa kazi ndani ya Yanga 2024/25. Source: Yanga.

Mabingwa watetezi wa ligi Yanga watakuwa kibiruani leo kusaka pointi tatu dhidi ya Ken Gold mchezo unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Sokoine, Mbeya ambapo timu zote mbili zinapigia hesabu pointi tatu muhimu.

Yanga inayodhaminiwa na SportPesa kete ya kwanza ilikuwa dhidi ya Kagera Sugar ilichezwa Uwanja wa Kaitaba, Bukoba na baada ya dakika 90 ubao ulisoma Kagera Sugar 0-2 Yanga. Ikumbukwe kwamba mfungaji wa bao la kwanza ndani ya Yanga ni Maxi Nzengeli kisha wa pili ni mshambuliaji mzawa Clement Mzize.

Miguel Gamondi Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa kila mchezo ambao wanacheza ni muhimu kupata matokeo na wapinzani wao wamekuwa wakicheza kwa kujitahidi ili kupata ushindi jambo ambalo limekuwa likiongeza ushindani.

“Siku zote timu yoyote ikicheza na Yanga wanakuwa makini na kutafuta matokeo kama sisi, tutacheza kwa tahadhari na tuna wachezaji wazuri wenye uzoefu wa kucheza kwenye mazingira yoyote.”

Ken Gold baada ya kucheza mechi nne ambazo ni dakika 360 haijaambulia ushindi katika mechi zake za msako wa ushindi ndani ya uwanja ikiwa imepanda ligi msimu wa 2024/25.

HII HAPA RATIBA YA SEPTEMBA 25 2024

Fei v JKT Tanzania
MCHEZO wa kwanza wa JKT Tanzania msimu wa 2024/25 ilikuwa dhidi ya JKT Tanzania. Source: Azam FC.

JKT Tanzania itakuwa Uwanja wa Mej Isamuhyo kusaka pointi tatu mbele ya Coastal Union ya Tanga mchezo unatarajiwa kuchezwa saa 8:00 mchana. Ipo wazi kwamba timu hizi zote mbili hakuna ambayo imepata ushindi ndani ya msimu wa 2024/25 kwenye mechi za ligi.

Ken Gold wataikaribisha Yanga, Uwanja wa Sokoine, Mbeya saa 10:15 jioni kwa timu zote mbili kusaka pointi tatu muhimu. Ken Gold haijapata ushindi kwenye mechi zake ilizocheza msimu wa 2024/25.

 

 

Share this: