Abuya kimataifaAbuya kimataifa

KAZI imekamilika kwenye ngwe ya kwanza kwa wawakilishi wa Tanzania Yanga katika anga la kimataifa baada ya kutinga hatua ya makundi kwa kishindi ikiwa ni mara ya pili mfululizo huku wakipata ushindi mkubwa mbele ya wapinzani wao CBE SA ya Ethiopia kwenye dakika 90 za funga kazi zilizokuwa za ushindani mwanzo mwisho wakishinda mechi zote mbili kimataifa ambazo ni dakika 180.

Kimataifa Yanga hi sifa mashabiki walikuwa wakisikika wakisema hivyo baada ya kutinga hatua ya makundi kwa ushindi kwenye mechi mbili za raundi ya pili ambazo ni dakika 180 huku wakicheza mchezo wa kasi na kufunga mabao mengi kwenye mchezo wa pili wakiwa kwenye ardhi ya Tanzania.

Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi alionyesha ukubwa wa kikosi cha Yanga kinachodhaminiwa na SportPesa ambapo alifanya mabadiliko makubwa kikosi cha kwanza kikiwa na mfumo tofauti kabisa na kile ambacho kilicheza ugenini.

Ushindi wa Yanga ni salamu kwa watani zao wa jadi Simba ambao watakuwa na kibarua cha kusaka ushindi kwenye mchezo dhidi ya Al Ahli Tripol ya Libya ukiwa ni mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika.

Mshindi wa mchezo huo unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa atakata tiketi ya kutinga hatua ya makundi hivyo kila timu ina nafasi ya kutinga hatua hiyo kwa sababu kwenye mchezo wa kwanza ubao ulisoma Al Ahli Tripoli 0-0 Simba.

HUYU HAPA MASTA GAMONDI

Gamondi Masta
Gamondi Masta mpanga mipango ndani ya Yanga 2024/25. Source: Yanga.

Mchora mipango ndani ya kikosi cha Yanga, Miguel Gamond amesema kuwa ulikuwa ni mchezo muhimu kwao kupata ushindi na walikubaliana kupambana mwanzo mwisho kwa kufanyia kazi makosa yaliyotokea kwenye mchezo wa kwanza wakiwa ugenini.

“Tulifanya makosa kwenye mchezo wa kwanza ugenini licha ya kwamba tulipata ushindi bado kuna nafasi ambazo tulitengeneza na hatukuzitumia hivyo ilikuwa ni muhimu kwetu kupata ushindi ukizingatia tulikuwa nyumbani.

“Pongezi kwa wachezaji wamejituma kutimiza majukumu yao hilo ni jambo la muhimu, mashabiki wamekuwa nasi kwenye hatua zote hivyo tunawashukuru na wazidi kuwa pamoja nasi kwa kuwa hatua hii imekwisha inakuja hatua nyingine ambayo nayo itakuwa na ugumu zaidi.”

ANGALIA KOSI LA KWANZA NEW AMAAN COMPLEX

Mzize
Mzize Clement kwenye mchezo wa kimataifa dhidi ya CBE SA 2024/25. Source: Yanga.

Djigui Diarra alianza langoni, Yao, Boka, Dickson Job, Bacca, Jonas Mkude, Maxi Nzengeli, Mudathir Yahya, Clement Mzize, Clatous Chama na Pacome hawa walianza kikosi cha kwanza.

Wachezaji waliokuwa wakisoma mchezo wakiwa benchi kwa upande wa mlinda mlango alikuwa ni Aboutwalib Mshery, Nickson Kibabage, Aziz Ki, Dennis Nkane, Duke Abuya, Khalid Aucho, Kennedy Musonda na Prince Dube.

Kwa wachezaji waliokuwa benchi wapo walioinga na kufunga ikiwa ni Duke, Aziz Ki walikuwa benchi wamekaa na mabao yao kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika na walipoingia walifanya kwelikweli.

CBE WAPIGWA NJE NDANI, YANGA YAKOMBA MINOTI

Dube
PRINCE Dube, Mudathir, Aziz Ki nyota wa Yanga kwenye mchezo wa kimataifa dakika 90 za ugenini dhidi ya CBE SA. Source: Yanga.

CBE SA ya Ethiopia wamepigwa nje ndani na Yanga huku wakikomba minoti ya kutosha kutokana na ushindi mkubwa ambao wameupata katika anga la kimatafa kwenye hatua ya raundi ya pili.

Yanga ni milioni 35 imevuna kwa kuifunga jumla ya mabao 7-0 ndani ya dakika 180 CBE SA katika anga la kimataifa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika. Ikumbukwe kwamba kwenye mchezo uliochezwa nchini Ethiopia Yanga ilishinda bao 1-0 likifungwa na Prince Dube dakika ya 45.

Rekodi imeandikwa Septemba 21 2024 Yanga inayonolewa na Gamondi kutinga hatua ya makundi kwa ushindi wa mabao 6-0 CBE SA katika mchezo uliochezwa Uwanja wa New Amaan Complex ikiwa ni mara ya pili mfululizo kutinga hatua hiyo kubwa.

HAWA HAPA WALIOPELEKA KILIO KIMATAIFA

Chama v CBE SA
CLATOUS Chama akitimiza majukumu yake anga la kimataifa dakika 90 za kazi dhidi ya CBE SA. Source:Yanga.

Mastaa wa Yanga walikuwa kazini kweli na walipeleka kilio kwa wapinzani wao kimataifa kupitia kwa Clatous Chama dakika ya 35, Clement Mzize dakika ya 46, Aziz Ki dakika ya 74, 90, Mudathir Yahya dakika ya 88 na Duke Abuya dakika ya 90.

Ikumbukwe kwamba msimu wa 2023/24 Yanga ilitinga hatua ya makundi Afrika na kugotea hatua ya robo fainali hivyo ina kazi nyingine kufanya kwa msimu mpya wa 2024/25 kuvunja rekodi hiyo kimataifa. Ushindi huo umewapa Yanga kiasi cha milioni 30 za goli la mama ilikuwa baada ya dakika 90 kugota mwisho. Hivyo CBE SA wameipa Yanga milioni 35.

Rais wa Yanga, Injinia Hersi Said ameweka wazi kuwa ni jambo kubwa ambalo limefanywa na wachezaji na ushindu ni mkubwa kupatikana wakitinga hatua ya makundi.

“Ni furaha kwetu na tunamshukuru Mama kwa zawadi. Furaha yetu kuona tumetinga hatua ya makundi haikuwa rahisi lakini wachezaji wamepambana.”

Share this: