Ateba v Azam GoalAteba v Azam Goal

 

NGOMA ni nzito ndani ya uwanja ambapo dakika 90 za msako wa ushindi kila timu inavuja jasho kufikia malengo yao kumekuwa na ushindani mkubwa kusepa na pointi tatu muhimu. Kwenye Mzizima Dabi, Azam FC yazimwa dakika 90 ndani ya uwanja baada ya kupoteza pointi tatu kwenye mchezo huo.

Mechi zote ambazo zinaendelea iwe kwenye Ligi Kuu Bara, Ligi Kuu England ni muda wa kuweka mkeka wako SportPesa na mchezo ukigota mwisho unakunja mkwanja wako.

Gumzo kubwa imekuwa Mzizima Dabi kukamilika kwenye mchezo uliochezwa Septemba 26 2024 baada ya dakika 90 ubao kusoma Azam FC 0-2 Simba kwa mabao ya Leonel Ateba na Fabrince Ngoma dakika ya 47.

HUYU HAPA MCHEZAJI BORA WA MCHEZO

Camara
Camara Mussa kipa namba moja wa Simba mwenye tuzo ya mchezaji bora dakika 90 za Mzizima Dabi. Source: Simba.

Kipa namba moja wa Simba kwenye mechi za hivi karibuni, Mussa Camara alichaguliwa kuwa mchezaji bora na aliokoa hatari moja iliyokuwa inakwenda langoni dakika ya 84.

Kazi yake nyingine ambayo aliifanya kwenye mchezo langoni kipa huyo ambaye alikuwa na kazi ya kutoka kwenye mchezo huo ambazo zilifika langoni mwake hazikuwa hatari kubwa ilikuwa dakika ya 68, 74, 86, 89 alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mchezo Mzizima Dabi Simba ikisepa na pointi tatu kwenye mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa.

 

TAMBO SEMAJI LA SIMBA

AHMED Ally
Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba. Source: Simba.

Baada ya ushindi waliopata Simba mbele ya Azam FC kwenye mchezo huo tambo zimetawala kwa timu hiyo ambayo inapambana kutwaa taji la ligi lililopo mikononi mwa Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Miguel Gamondi.

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba amebainisha kuwa walikuwa wanahitaji kupata pointi tatu muhimu na ilikuwa hivyo kutokana na mpango kazi ambao ulipangwa na mwisho wameibuka na ushindi jambo ambalo ni furaha kwao.

“Tumefurahi kupata ushindi kwenye mchezo wetu muhimu na ilikuwa hivyo kikubwa ni kwamba kila mchezaji alikuwa anatambua kwamba tunahitaji pointi tatu na walicheza kwa kujituma mwanzo mwisho kwa ajili ya kupata matokeo mazuri uwanjani wanastahili pongezi wachezaji wetu.

“Kazi bado inaendelea kwa kuwa tuna mchezo mwingine dhidi ya Dodoma Jiji hivyo wachezaji wakirudi Tanzania watakuwa na kazi kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wetu ujao hivyo bado kazi kubwa tutaifanya ili kupata matokeo mazuri.”

DAKIKA 270 USHINDI

Mechi tatu ambazo imecheza Simba ndani ya ligi ikikomba dakika 270 Simba imekomba pointi tisa safu ya ushambuliaji imefunga mabao 9 ikiwa na wastani wa kufunga mabao matatu kila baada ya dakika 90 kwenye mechi ambazo wamecheza msimu wa 2024/25.

MATAJIRI WA DAR WAPOTEZA

Leonel Ateba
Leonel Ateba mshambuliaji wa Simba kwenye mchezo wa Mzizima Dabi dhidi ya Azam FC. Source: Simba.

Matajiri wa Dar ni mechi tano wamecheza kwa msmu wa 2024/25 wakikomba dakika 450 ndani ya uwanja kutokana na kazi kubwa ya msako wa ushindi ndani ya uwanja kuwa ngumu kila kona. Azam FC imeshinda mechi mbili na kupoteza mchezo mmoja.

Mechi za Azam FC ilikuwa JKT Tanzania 0-0 Azam FC, Azam FC 0-0 Pamba Jiji kwenye mechi hizi ilitoshana nguvu na mpinzani wake na mchezo dhidi ya KMC 0-4 Azam FC, Azam FC 1-0 Coastal Union ilikomba pointi tatu.

Kwenye mechi nne ni mabao matano ilifunga na kinara wa kutengeneza pasi za mwisho ni Feisal Salum mwenye pasi tatu  ambaye alichaguliwa kuwa mchezaji bora dhidi ya KMC uliochezwa Uwanja wa KMC, Mwenge.

RATIBA LIGI KUU BARA SEPTEMBA 27

Ligi Kuu Bara inaendelea ambapo kuna mechi zitachezwa katika msako wa ushindi wa pointi tatu ndani ya uwanja katika dakika 90 za kazikazi.

Fountain Gate watakuwa nyumbani Uwanja wa Tanzanite, Kwarara dhidi ya Kagera Sugar huku Fountain Gate wakibainisha kuwa watafanya kazi kubwa kwa ajili ya kupata ushindi kwenye mchezo huo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

Issa Liponda Ofisa Habari wa Fountain Gate amesema kuwa wanatambua mchezo huo utakuwa na ushindani mkubwa watafanya kazi kusaka ushindi kwenye mchezo huo kuwapa zawadi mashabiki wao watakaojitokeza uwanjani.

“Kikubwa kwenye mchezo wetu tutafanya kazi kubwa ili kupata matokeo mazuri na inawezekana kwani tutakuwa nyumbani na kazi imekamilika kwa asilimia kubwa, mashabiki wajitokeze kwa wingi kushuhudia mchezo wetu ambao utakuwa na ushindani mkubwa mwanzo mwisho.”

SEPTEMBA 28 ITAKUWA NAMNA HII

Pamba
WACHEZAJI wa Pamba Jiji wakiwa kwenye maandalizi ya mechi za ushindani. Source: Pamba.

Ken Gold v Tabora United, saa 8:00 mchana, Uwanja wa Sokoine, Mbeya

Coastal Union v Pamba Jiji saa 10: 15 jioni, Uwanja wa Azam Complex.

Namungo v Tanzania Prisons, Uwanja wa Majaliwa saa 1:00 usiku.

Share this: