
Mara baada ya tambo za nje nya uwanja hatimaye ubishi umemalizwa jijini Mbeya baada ya kikosi cha Yanga Combine kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya timu ya Vijana Combine katika mchezo wa kwanza wa ufunguzi wa mashindano makubwa ya SportPesa Shabiki Cup.
Mashindano hayo ya kwanza na ya aina yake yanaratibiwa na Kampuni namba moja bora ya michezo ya kubashiri ya SportPesa kwa kuishirikisha jamii kwa lengo la kuwakutanisha wapenda soka kutoka mikoa mbalimbali kushirikiana na vilabu vinavyodhaminiwa na SportPesa wakiwemo mabingwa watetezi Yanga.
Ikumbukwe kuwa Yanga pia walikuwa jijini Mbeya kuwavaa Fountain Gate kwenye mchezo wa ligi Kuu.
Mashindano haya pia yameanzishwa kwa lengo la kuimarisha uhusiano kati ya jamii na mashabiki wa soka wa maeneo ya karibu kwa kutoa fursa ya kushiriki, kushindana, na kushirikiana.
MALISA MGENI RASMI SPORTPESA SHABIKI CUP

Uongozi wa SportPesa katika mchezo huo kati ya Yanga Comnbine na Vijana Combine unapenda kutoa shukrani za dhati kwa Mgeni rasmi, Mh. Beno M. Malisa – Mkuu wa wilaya Mbeya kwa kutufungulia michuano ya Sportpesa Shabiki Cup.
HISTORIA YAANDIKWA MWENGE STADIUM
Mchezo huo wa kwanza na wa ufunguzi wa mashindano hayo msimu huu ulipigwa katika Uwanja wa Mwenge, Mbeya ambao umeandika rekodi kali ya kuhodhi sherehe za ufunguzi.
VIKOSI VYA TIMU ZOTE MBILI


- Yanga Combine
Kikosi cha kwanza kiliundwa na; Danieli Nyesse, Baraka Moses, Lingo Gigi, Deo Hamis, Kelvin Steven, Innocent Lucas, Samson Kamesa, Jakobo Ndeja, Emmanuel John, Coshudo Mwaipaja, Joel Kyungu.
- Vijana Combine
Kikosi chao kiliundwa na; Evance Leornard, Adolph Kyando, Stanley Gerald, Rodgers Raytou, Ayubu Mwazanji, Ibrahim Hamis, Festo Frank, Abdallah Omary, Halidi Mapuli, Kelvin Kasyupa, Omary Mustapha.
Goli pekee la mchezo huo lilifungwa katika kipindi cha kwanza.
MUUNDO WA MASHINDANO UNAKUWAJE?
Mashindano yanafanyika katika mikoa mbalimbali nchini ambapo kila eneo, timu mbili zitashindana:
Timu 1: Timu iliyoundwa na wachezaji kutoka vilabu vinavyodhaminiwa na SportPesa.
Timu 2: Timu iliyochaguliwa kutoka kwa jamii ya eneo husika.
Washindi wa kila eneo watapokea tuzo zao kama ilivyoelezwa kwenye sehemu ya zawadi.
IKUMBUKWE VIGEZO VYA USHIRIKI NI KAMA IFUATAVYO
Wachezaji lazima wawe na umri wa miaka 18 na kuendelea.
Washiriki lazima wawe raia, au wakazi wa kudumu wa Tanzania.
Kwa Timu 1, wachezaji wote lazima wawe wanachama hai wa tawi linalotambulika.
Kwa Timu 2 (Timu ya Jamii ya Wenyeji), wachezaji wote lazima watoke katika jamii ya eneo linaloandaa tukio.
Usajili
Fomu za usajili zitapatikana kwenye vibanda maalum vya SportPesa katika kila eneo pamoja na ofisi ya Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa. Wachezaji lazima wajisajili mmoja mmoja, wakitoa uthibitisho wa makazi katika jamii husika.
Mchakato wa Uteuzi wa vipaji
Kamati ya uteuzi, ikijumuisha makocha wa soka wa eneo, wawakilishi wa matawi, na maafisa wa SportPesa, watapitia wachezaji wote waliosajiliwa.
Maonyesho ya vipaji yatafanyika kwa siku mbili katika kila eneo, ambapo wachezaji waliosajiliwa wataonyesha ujuzi wao mbele ya kamati ya uteuzi. Kamati ya uteuzi itawapima wachezaji kwa kuzingatia ujuzi wa soka, ushirikiano wa timu, na nidhamu ya michezo.
Kamati itachagua wachezaji 14 (11 wa kuanza na 3 wa akiba) kuunda Timu ya Jamii ya Wenyeji. Uteuzi utatangazwa mwishoni mwa majaribio.
Ni zipi sheria za mashindano;
Muda wa Mchezo: Kila mchezo utakuwa na vipindi viwili vya dakika 30, na mapumziko ya dakika 10 katikati.
Kuamua Mshindi: Iwapo mchezo utamalizika kwa sare ya 0-0 katika dakika ya 70, mshindi ataamuliwa kwa kupiga mikwaju ya penalti.
Badiliko la Wachezaji: Kila timu itaruhusiwa kufanya mabadiliko matatu kwa kila mechi.
Madhibiti: Mechi zote zitaendeshwa na waamuzi waliothibitishwa na shirika husika.
Hatua za Nidhamu: Sheria za kadi ya njano na nyekundu zitatumika kulingana na kanuni za kawaida za soka. Wachezaji watakaopokea kadi nyekundu watafungiwa kushiriki.
Kuhusu Zawadi
Timu Inayoshinda: Timu itakayoshinda mechi ya mwisho ya mashindano itazawadiwa Kikombe cha SportPesa Shabiki Cup na zawadi ya Fedha kiasi cha TZS 500,000.
Jezi za Timu: Seti kamili ya jezi za mpira kwa wachezaji wote na benchi la ufundi.
Medali: Medali kwa kila mshiriki wa timu.
Timu ya Pili
Zawadi ya Fedha: TZS 250,000, Medali: Medali kwa kila mshiriki wa timu.
Zawadi za Wachezaji Binafsi
Mfungaji Bora: TZS 100,000.
Kipa Bora: TZS 100,000.
Mchezaji Bora (MVP): TZS 100,000.
Sheria za Jumla
Uamuzi wa waamuzi na kamati ya waandaaji ni wa mwisho na lazima uheshimiwe.
Timu lazima zifuate ratiba ya mashindano. Kushindwa kufika kwa wakati wa mchezo kutasababisha kupoteza.
SportPesa inahaki ya kuwaondoa timu au mchezaji yeyote atakayekiuka sheria za mashindano au kuonyesha tabia isiyo ya kimichezo.
Kuhusu udhamini na uwekaji Nembo
SportPesa inahifadhi haki zote za kipekee kwa matangazo na shughuli za utangazaji zinazohusiana na mashindano.
Timu zote zinahitajika kuvaa jezi zenye nembo za SportPesa wakati wa mechi.
Vyombo vya Habari na Matangazo
Kwa kushiriki kwenye mashindano, wachezaji na timu wanakubali kuruhusu SportPesa kutumia picha zao, majina, na sura kwa ajili ya matangazo na uendelezaji kwenye majukwaa mbalimbali ya vyombo vya habari.
Mabadiliko
SportPesa inahifadhi haki ya kubadili Masharti na Vigezo hivi wakati wowote washiriki watajulishwa mapema kuhusu mabadiliko yoyote.
Dhima
SportPesa haitahusika kwa majeraha, ajali, au uharibifu wowote utakaotokea wakati wa mashindano na washiriki wanahimizwa kuchukua tahadhari.

