Algeria World Cup 2026
  • Algeria vs Austria Kombe la Dunia 2026, ni mechi ya fainali ya Kundi hili ambapo yoyote atakayeshinda ataungana na Argentina kufuzu hatua ya 32 bora.
  • Mechi hii kali itapigwa kwenye Uwanja wa Kansas City, USA 28 June 2026 saa 11 alfajiri kwa saa za Afrika Mashariki.
  • Wawakilishi wa Afrika Algeria watakuwa na kibarua kigumu cha kuhakikisha hawapotezi mchezo huu, na ikiwezekana kufuzu.
  • Makala hii inachambua h2h, livescore, takwimu na Habari za timu za mechi hii kama ifuatavyo

Algeria watashuka uwanjani kusaka tiketi ya kucheza hatua ya mtoano 32 bora mbele ya Austria, katika mchezo huu wa kukamilisha ratiba ndani ya Kundi J la Kombe la Dunia 2026. Ushindi kwa yoyote, yaani Austria au, Algeria utakuwa unatoa taswira mpya ya Kundi hilo ya timu inayoungana na Argentina kwenda hatua ya mtoano. Swali ni je, Algeria chini ya staa wao Riyad Mahrez watafanikiwa kufanya maajabu?

Hizi hapa Odds bora za SportPesa za mechi ya Algeria vs Austria

Kwa wanaotafuta odds bora, SportPesa inatoa masoko mbalimbali ya ubashiri pamoja na malipo ya haraka. kwa sasa odds zimeborwesha na unaweza kubashiri mechi hii sasa gusa hapo chini, ili kubashiri moja kwa moja.

Jordan vs Argentina
Jordan vs Argentina

Maelezo ya Mechi

Algeria vs Austria Kombe la Dunia 2026
Austria
KipengeleMaelezo
MashindanoMchezo wa mwisho wa hatua ya makundi katika Kundi J la Kombe la Dunia la FIFA 2026, ukiwa ni wa tatu kwa kila timu katika kundi hilo.
Tarehe na MudaPambano litachezwa Jumapili, 28 Juni 2026, kuanzia saa 11:00 alfajiri (EAT).
UwanjaKansas City Stadium, Marekani, utakuwa mwenyeji wa mchezo huu muhimu wa kuamua hatima ya Kundi J.
Msimamo wa Kundi JArgentina wanaongoza kundi wakiwa na pointi 6 na tayari wamefuzu hatua inayofuata. Austria na Algeria zote zina pointi 3, huku Austria wakiwa mbele kwa tofauti ya mabao. Jordan wanashika nafasi ya mwisho bila pointi.
Mchezo Mwingine wa KundiWakati huohuo, Argentina watamenyana na Jordan katika mchezo mwingine wa Kundi J, ambao utahitimisha ratiba ya hatua ya makundi kwa timu zote mbili.

KUJUA RATIBA YA MECHI ZOTE 104, SOMA HII: Ratiba FIFA Kombe la Dunia 2026 | Mechi zote 104 | Tarehe | Muda wa mechi | Uwanja utakaotumika

Muhtasari wa Algeria vs Austria

Algeria na Austria zitakutana katika pambano muhimu la Kundi J la Kombe la Dunia 2026 litakalopigwa Jumapili kwenye Uwanja wa Kansas City. Kila timu itakuwa ikisaka nafasi ya kufuzu hatua ya mtoano. Algeria walipata ushindi wa kihistoria wa 2-1 dhidi ya Jordan katika mchezo wao uliopita, wakati Austria walikubali kichapo dhidi ya Argentina ya Lionel Messi.

Hili ni Kombe la Dunia la tatu kwa Algeria katika karne hii baada ya kushiriki mwaka 2010 na 2014. Sasa wanalenga kufuzu hatua ya mtoano kwa mara ya pili katika historia yao. Algeria wanahitaji ushindi ili kujihakikishia nafasi ya pili, na kufuzu moja kwa moja hatua ya 32 bora. Hata hivyo, kumaliza katika nafasi hiyo kunaweza kuwakutanisha mapema na mabingwa wa Ulaya, Hispania, katika hatua inayofuata.

Austria wanaingia katika mchezo huu wakiwa na kumbukumbu ya kipigo cha mabao 2-0 dhidi ya Argentina ya Lionel Messi. Kikosi cha kocha Ralf Rangnick kilikosa ubunifu wa kutosha mbele ya Argentina. Hata hivyo, Austria wameonyesha kiwango kizuri, katika Kombe la Dunia lao la kwanza baada ya miaka 28.  

Habari za Timu na Vikosi Vinavyotarajiwa

Algeria huenda wakamkosa mshambuliaji wao muhimu Mohamed Amoura, ambaye bado anauguza majeraha ya misuli ya paja aliyoyapata katika hatua ya makundi. Kutokana na kukosekana kwake, nahodha Riyad Mahrez atabeba jukumu kubwa zaidi la kuiongoza safu ya ushambuliaji. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 35 alitoa pasi ya bao katika ushindi dhidi ya Jordan.

Kwa upande wa Austria, baada ya kupiga shuti moja tu lililolenga lango dhidi ya Argentina, kocha Rangnick anaweza kufanya mabadiliko katika safu yake ya ushambuliaji. Baada ya kuingia akitokea benchi katika michezo miwili iliyopita, mshambuliaji mkongwe Marko Arnautovic anaweza kuanza. Kiungo wa Borussia Dortmund, Carney Chukwuemeka, ambaye hivi karibuni alibadili uraia wa kisoka kutoka England kwenda Austria, pia ana nafasi ya kuanza kikosini.

Vikosi vinavyotarajiwa

Algeria

Algeria World Cup ---- squadd
Kikosi cha Algeria cha Kombe la Dunia 2026
NafasiWachezaji
KipaZidane
WalinziBelghali, Mandi, Bensebaini, Ait Nouri
ViungoBentaleb, Benbouali, Mahrez, Maza, Chaibi
WashambuliajiGouiri

Austria

and this Alexander Schlager;

Posch, Danso, Alaba, Laimer;

Seiwald, Xaver Schlager;

Schmid, Wanner, Sabitzer;

Arnautovic

Utabiri (zaidi ya goli 2 yaani over 1.5)

Algeria World Cup 2026
Algeria wakishangilia bao FIFA World Cup 2026

Kwa kuzingatia umuhimu wa mchezo huu na hali ya msimamo wa kundi, huenda timu zote mbili zikacheza kwa tahadhari kubwa. Austria wanaonekana kuwa na nidhamu zaidi kama timu, lakini ubora wa wachezaji wa Algeria katika eneo la ushambuliaji unaweza kuwasaidia kupata angalau bao. Austria pia bila shaka watalazimika kujibu hivyo uwezekano wa mabao 2 au zaidi. Kumbuka hay ani maoni ya kiuhariri na sio matokeo rasmi hivyo Bashiri kistaarabu.

KUJUA RATIBA NA UCHAMBUZI WA MECHI IJAYO YA ARGENTINA, SOMA HII: Jordan vs Argentina Kombe la Dunia 2026 Kundi J: Live score, h2h, odds na habari za timu

Rekodi ya Algeria vs Austria (H2H)

Timu hizi zimewahi kukutana mara moja tu, nah ii ilikuwa kwenye hatua ya makundi ya Kombe la Dunia 1982. Katika mchezo huu Austria walishinda mabao 2-0. Je Algeria wataweza kulipa kisasi, dakika 90 zitatoa majibu.

Hitimisho

Utabiri wetu wa kiuhariri unayapa nafasi kubwa matokeo ya zaidi ya mabao mawili, yaani over 1.5 katika mchezo huu. Mechi hii itatoa taswira ya nani anaungana na Argentina kwenda hatua ya mtoano ya 32 bora. Endelea kufuatilia SportPesa Blog kwa ratiba, matokeo, utabiri na habari za Kombe la Dunia 2026. Angalia odds za Algeria vs Austria kwenye SportPesa na ubashiri kistaarabu.

Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara (FAQ)

Kombe la Dunia (-)
Kombe la Dunia

Algeria vs Austria itaanza saa ngapi?

Mechi itaanza saa 11 alfajiri kwa saa za Afrika Mashariki (EAT) Jumapili tarehe 28 Juni 2026.

Algeria vs Austria zipo Kundi gani?

Wapo Kundi J pamoja na Argentina na Jordan.

KUJUA UCHAMBUZI NA RATIBA YA MECHI IJAYO YA UFARANSA, SOMA HII: Prediction: Croatia vs Ghana FIFA Kombe la Dunia 2026: H2H, team news, odds

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.