Kikosi cha EnglandKikosi cha England
ENGLAND
Kikosi cha England Vs Jamhuri ya Ireland (Photo-England)

KOCHA wa muda wa kikosi cha timu ya Taifa ya England, Lee Carsley amethibitisha kuwa anatarajia kufanya mabadiliko ya kikosi chake leo usiku wakati ambapo England wanatarajia kuwa wenyeji wakiikaribisha timu ya Taifa ya Finland.

England leo Jumanne usiku watashuka kwenye Uwanja wao wa nyumbani wa Wembley kuvaana na Finland katika mfululizo wa michezo ya mashindano ya UEFA Nations League. Ikumbukwe unaweza kubashiri michezo hii kupitia Kampuni bora ya michezo ya kubahatisha nchini ya SportPesa.

Kocha huyo wa England ameweka wazi kuwa sababu kubwa ya kufanya maamuzi hayo ni kwa kuwa anahofia baadhi ya mastaa wa timu hiyo hawana ‘fitness’ ya kutosha kiasi cha baadhi yao kucheza chini ya kiwango kwenye mchezo dhidi ya Jamhuri ya Ireland.

Katika mchezo huo dhidi ya Jamhuri ya Ireland, England walifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0, mabao yao yakifungwa na viungo, Decline Rice na Jack Grealish.

Maamuzi hayo yanaonekana kuelezea kwanini kocha huyo hajamjumuisha kwenye kikosi chake mlinzi, Kyle Walker ambaye amekuwa na wakati mgumu kupata nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha Manchester City msimu huu.

 

Carsley pia ameweka wazi kuwa asingependa kupangua sana kikosi chake, lakini analazimika kutoka na mahitaji ya klabu za England ambazo kwa kiasi kikubwa ndipo wachezaji wanaounda kikosi chake wanatokea.

ALICHOSEMA CARSLEY

ENGLAND
Lee Carsley

Kocha huyo wa England amesema: “Ukiangalia kikosi utagundua kuwa kuna mnabadiliko kadhaa kutokana na dakika ambazo wachezaji hawa wamecheza hususani katika klabu zao, baadhi ya wachezaji hawa wamekuwa hawana nafasi ya ya kudumu, lakini pia wapo ambao wamekuwa panga pangua katika timu zao.

“Ni lazima tuwe wakweli kuwa tulicheza chini ya kiwango licha ya kushinda mchezo uliopita dhidi ya Jamhuri ya Ireland nah ii kwa kiasi fulani imechangiwa na baadhi ya wachezaji kutokuwa na daraja zuri la ufiti

“Na hii imetupa nafasi ya kufanya kazi kubwa katika program zetu za mazoezi ili kuhakikisha wanakuwa sawa na tayari kwa ajili ya ratiba ya michezo yetu ijayo.

“Kwa namna program hiyo ya mazoezi ilivyoendeshwa, naona kuna angalau wachezaji wanne au watano ambao wanaonekiana kuhitaji programu ya ziada na ni matumaini yangu kuwa programu hii itawasaidia sana na nimeshuhudia kundi hili la wachezaji likiwa limehamasika sana kufanya bora zaidi.”

Katika hatua nyingine, Carsley amegusia uwezekano wa kukutana na mtangulizi wake na kocha wa zamani wa England, Gareth Southgate ili kuongeza mawazo ya jinsi gani ya kukifanya kikosi hiko kiwe bora.

Carsley amethibitisha kuwa tayari alipata nafasi ya kuzungumza na kocha huyo kwa kifupi mara baada ya kukabidhiwa makukumu  ya kuiongoza timu hiyo.

Kocha huyo amesema: “Nilipatana nafasi ya kuzungumza naye kwa ufupi baada ya kupewa majukumu haya. Najua nitapata nafasi ya kuzungumza naye kwa urefu mara baada ya kumalizika kwa kambi. Gareth amekuwa mtu muungwana sana kwangu hususani kwa namna ya kikosi nilichokiita.

“Kwa kweli bado sijajua nini tutazungumzia, lakini natamani zaidi kusikia kutoka kwao, njue maoni yao juu ya hili suala.

“Ni lazima tuseme ukweli kuwa Gareth na msaidizi wake Steve wamekuwa na uzoefu mkubwa wa soka kulinganisha na mimi kama mnavyofahamu mpaka sasa kuhusu mechi za kimataifa nimeongoza timu kwenye mchezo mmoja tu.

“Hivyo chochote nitakachopata kutoka kwao kitasaidia sana timu na wahezaji kufanya vizuri zaidi.”

Leo Jumanne Septemba 10, mwaka 2024 England watashuka tena uwanjani kuvaana na Finland katika mchezo ambao unatabiriwa kuwa na ushindani mkubwa.

Pamoja na mchezo huo, leo Jumanne pia kunatarajiwa kupigwa mchezo mwingine utakaozikutanisha timu za Uholanzi na Ujerumani katika mfululizo wa michezo ya mashindano ya UEFA Nations League katika kipindi hiki cha ratiba ya Shirikisho la soka Duniani (FIFA).

Kuendana na ratiba ya FIFA ligi nyingi zimesimama kwa ajili ya kupisha michezo ya kimataifa ambapo barani Afrika pia michezo ya kusaka tiketi ya kufuzu mashindano ya Kombe la Mataifa Afrika (AFCON), zitakazopigwa nchini Morocco inaendelea ambapo timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars imeshuka uwanjani leo pia kuvaana na Guinea.

 

 

 

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.