Wachezaji wa Uholanzi wakishangilia moja ya goli.Uholanzi

Timu za Taifa Netherlands kwa kiswahili Uholanzi ‘’The Orange’’ na Croatia kesho Jumatano  usiku zitakutana kwenye mchezo wa nusu fainali ya kwanza ya michuano ya kombe la UEFA Nations League itakayopigwa Juni 14,2023 pale Sation Feijenoord ‘De Kuip’ nchini Uholanzi.

Stori kubwa inayoendelea kuzungumzwa kwa sasa ni inayoihusu Uholanzi ambayo inalisaka Kombe lolote la michuano mikubwa tangu watwae michuano ya Euro mwaka 1988.

Uholanzi wanakutana na Croatia ambayo imemaliza kwenye nafasi za pili na tatu katika fainali mbili za Kombe la Dunia zilizopita (1998 walicheza fainali dhidi ya Ufaransa) na (2022 walishinda dhidi ya Morocco katika mchezo wa kuwania mshindi wa tatu).

The Orange wamefikia hatua hii wakitokea kwenye kundi lililokuwa na mataifa ya Ubelgiji, Poland na Wales na walifuzu pasipo kupoteza mchezo hata mmoja.

Duru za michezo barani Ulaya zinaarifu kuwa kocha aliyefanikisha timu ya Uholanzi kuendelea na mashindano haya Louis Van Gaal hatokuwa sehemu ya kikosi hicho.

Kocha huyo alijiengua kufuatia timu hiyo ya taifa ya Uholanzi  kuondolewa katika hatua ya robo fainali ya Kombe la Dunia iliyofanyika mwaka jana nchini Qatar.

Upande wa Croatia inawezekana hii ikawa ndio nafasi ya mwisho kwa kizazi chao cha dhababu kinachoongozwa na Luca Modric kujaribu kutwaa taji lenye hadhi kubwa katika medani ya Soka .

Ni muda mrefu umepita tangu timu ya taifa ya Croatia ipoteze mchezo, ambapo ni takribani mwaka mmoja na ushehe umepita tangu waliponyukwa kwa magoli 3-0 dhidi ya Austria ikiwa ni katika mchezo wa ufunguzi wa michuano hii.

Croatia walipoteza mchezo huo wakati nahodha wao Luca Modric hakuwepo kikosini lakini baada ya kipigo hicho wakali hao walirejea kwa kuichapa Denmark katika michezo miwili(nyumbani na ugenini),wakaitandika Ufaransa na kukusanya alama tatu muhimu dhidi ya Austria huko Vienna.

Wenyeji wa mchezo wa siku ya Jumatano, Uholanzi kwa sasa wananolewa na Kocha Roland Koeman ambaye atakuwa anahitaji kupata mafanikio zaidi ya yale ya mwaka 2019 ambapo The Orange walicheza fainali.

Ingawa kocha Koeman anaweza akakutana na changamoto kufuatia kuikosa huduma ya mshambuliaji wake mahiri, Memphis Depay kujiondoa kikosini kutokana na majeraha.

Lakini uwepo wa nyota wengine waliomaliza vizuri msimu wa mashindano mbalimbali kama Coady Gapko, Frank De Jong bila ya kuwasahau mabeki mahiri kama Virgil Van Dijk na Nathan Ake kunaweza kumpa ahueni Kocha Koeman kufanya vizuri dhidi ya Croatia.

Upande wa Croatia ambayo imekuwa katika ubora wa hali ya juu kwa takribani miaka mitano iliyopita kwa kuvaa medali kwenye mashindano mawili ya kombe la dunia na kutinga hatua ya 16 bora za UEFA Euro 2020 wapo chini ya Kocha Zlatko Dalic.

Wachezaji wa timu ya Croatia

Dalic kwa sasa anategemewa kupeleka taji la kwanza katika historia ya Croatia huku nahodha wa timu hiyo, Luca Modric akijaribu kumaliza kazi yake kwa heshima kwa kubeba Kombe na timu yake ya Taifa kabla ya kutundika daruga.

Akizungumza kuelekea mchezo huo Kocha wa Uholanzi Ronald Koeman amesema’’Mara zote dhidi ya Croatia mechi huwa ni ngumu,wana timu imara  na sote tunapaswa kuwa katika ubora wetu ili tufuzu fainali.Croatia wanacheza katika kilele cha ubora wao,wanatumia ngumu na kwa kushinikiza.Tulifika fainali 2019 na kupoteza, sasa tunayo nafasi tukiwa nyumbani ili tupate tiketi ya kucheza fainali na nina imani tutashinda’’.

Naye Kocha wa Croatia Zlatko Dalic  amesema wanacheza na moja ya timu ngumu katika michuano hii ya Ulaya. ‘’Tunafahamu uwanja utakuwa umejaa, wana Kocha mpya na wanayo timu mahiri, hususan katika idara ya ulinzi. Wana timu imara yenye vijana wengi,wenye nguvu. Ninatarajia mashabiki wetu watatushangilia ili tupate hamasa zaidi’’. Alisema

Timu zote zimekuwa na matokeo mchanganyiko katika michezo sita ya hivi karibuni. Ukiachia Kepteni wa timu ya Croatia Luka Modric wachezaji wengine wanaotegemewa katika mechi hii ni pamoja na Dominik Livakovic, Ivica Ivusic, Mateo Kovacic, Nikola Vlasic, Ivan Perisic, Marko Livaja na Bruno Petkovic.

Uholanzi wameshinda mitatu, wametoa sare michezo miwili na kupoteza mmoja. Croatia kwa upande wao wameshinda mechi 4, wametoa sare mechi moja na wamepoteza mchezo mmoja.

Katika historia ya timu hizi mbili Uholanzi na Croatia zimekutana mara moja tu, ambapo walimenyana kwenye mchezo wa kirafiki mnamo mwaka 2018 na The Orange waliibuka na ushindi wa bao 3-0.

Mshindi katika mchezo wa kesho atacheza fainali dhidi ya mshindi kati ya Hispania na Italia.

Fainali ya Uefa Nations League inategemewa kupigwa June 18,2023 katika Jiji la Rotterdam nchini Uholanzi.

Ukitaka kubashiria mechi hii,ambayo tayari ipo katika tovuti yetu, tembelea sportpesa.co.tz au piga *150*87#.

Share this: