AzamAzamYanga

Fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports Federation Cup inatarajiwa kupigwa leo Juni 12,2023 katika dimba la CCM Mkwakwani mjini Tanga, kuanzia majira ya saa tisa alasiri, ikizikutanisha mabingwa watetezi Yanga ambao watawakabili na wanalamba lamba Azam Fc.

Mechi hii ya fainali, inategemewa kuwa moja ya fainali kabambe kwa timu zote mbili. Kwa kuanzia Azam wao watakuwa wakiwania ubingwa wa pili, tangu kurejeshwa rasmi kwa michuano hiyo msimu wa 2015/16 ambapo wao walitwaa taji katika msimu wa 2018/19 walipowanyuka Lipuli ya Iringa kwenye fainali iliyopigwa katika dimba la Majaliwa mkoani Lindi.

Kwa Yanga hiyo ni fainali yao ya nne ambapo wao ndio walikuwa mabingwa wa kwanza baada ya kurejeshwa kwa mashindano hayo msimu wa 2015/16 walipowanyuka Azam Fc jumla ya mabao 3-1.

Tafsiri yake ni kwamba mtanange wa leo pale Mkoani Tanga ni mechi ya kisasi ambacho Azam watahitaji kukilipa ili nao wajivunie kubeba taji kubwa nchini, tena dhidi ya Yanga. Lakini Wananchi nao kwa upande wao, leo wanacheza fainali ya tatu ya kombe la ASFC, nao pia watataka kuendeleza rekodi nzuri ya makombe ambayo tayari wamejiwekea katika misimu hii miwili.

Vile vile Yanga watakuwa wanawania kuendeleza ubabe dhidi ya Azam, lakini pia kuwania ubingwa huu kwa mara ya watatu baada ya kulitwaa msimu uliopita walipoinyuka Coastal Union kwa mikwaju ya penati.

Yanga wao walitinga fainali ya pili katika msimu wa 2020/21 na wakapoteza mbele ya watani zao Simba SC ambao waliibuka kidedea kwa ushindi wa bao 1-0 mchezo uliopigwa katika dimba la Lake Tanganyika mkoani Kigoma.

Tafsiri yake ni kwamba Yanga wao wanawania pia kuifikia rekodi ya Simba ya kutwa mataji matatu ya michuano hiyo tangu msimu wa 2015/16, lakini pia wanawania taji la tatu msimu huu baada ya kushinda ngao ya jamii,Ligi Kuu Tanzania bara na FA.

Yanga vs AzamKlabu hizi mbili zilitupa mechi nzuri sana katika duru la kwanza na la pili katika Ligi Kuu ya Tanzania bara msimu huu,wa kwanza walitoshana nguvu ya sare ya bao mbili  huku katika mechi ya marudiano Yanga wakaibuka washindi.

Yanga wakiwa wanajivunia kwa kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu wakimaliza vinara na alama zao 78 wakati Azam wao wamemaliza ndani ya nafasi tatu wakiwa na alama 59.

Katika michezo ya mwisho ya Ligi Kuu tumeishuhudia Azam ikiisambaratisha Polisi Tanzania kwabao 8-0 huku mshambuliaji hatari wa wana lambalamba Prince Dube akifunga bao nne peke yake jambo ambalo limeonyesha kutishia amani katika mchezo wa siku ya Jumatatu.

Upande wa Yanga katika mchezo wa mwisho waliinyuka Tanzania Prisons kwa bao 2-0 huku mshambuliaji wake hatari Fiston Mayele akitupia bao na kumfanya kuwa amejiweka tayari kwa ajili ya mchezo wa fainali,maana yake washambuliaji vinara wa Klabu hizo mbili wote wapo katika moto,je yupi atabeba sifa za kuivusha Klabu moja katika mafanikio ya mwisho ya kubeba taji?

Ikumbukwe Fiston Mayele amemaliza kinara wa kufunga mabao(17) sawa na Saido Ntibazonkiza wa Simba wakati Prince Dube ndiye mfungaji namba tatu kwenye orodha hiyo akiwa na bao 12.

Kuelekea mchezo huo Yanga inatarajiwa kumkosa Jesus Moloko ambaye alionyeshwa kadi nyekundu katika mchezo dhidi ya Mbeya City ambao wananchi walitoka nyuma na kusawazisha bao zote tatu.

Lakini Bernard Morrison na Khalid Aucho wote wamemaliza adhabu ya kutumikia kadi za njano na watakuwepo katika mchezo huo.

Hakuna taarifa zozote za kukosekana kwa wachezaji kutoka kambi ya Azam Fc, lakini kwa Yanga watawakosa Azziz Ki na Fiston Mayele, baada ya mashirikisho yao ya soka kuwakatalia kubaki Tanzania kwa kuwa wanamechi za kufuzu Afrika baadae wiki hii.

Azam watakuwa nao wakiwategemea kina Prince Dube, kiungo, Mbombo, Abdul Sopu, Iddi Nado, Tape Dinho, Tepsie na wengineo.

Azam wao walitangulia kuwasili mjini Tanga mapema zaidi ili kuzoea hali ya hewa na mazingira wakati wenzao Yanga walikuwa na sherehe zao maalum za kulitembeza taji la Ligi Kuu walilolitwaa msimu huu na hivyo kulazimika kuingia Tanga siku ya jana.

Mechi hii inatarajiwa kuwa na upinzani mkali na pia ya kusisimua, ikiwa inachagizwa na kisirani cha kuchukuliana mchezaji ambapo wiki hii Azam Fc imechochea utamu wa mchezo wa leo,  baada ya kuthibitisha kuinasa saini ya aliyekuwa kiungo wa Yanga, Feisal Salum, almaarufu kama (Fei toto), jambo ambalo linaweza kuwachochea wananchi kutaka kuwaadhibu wana lambalamba uwanjani alasiri ya leo.

Mechi hii tayari ipo kwenye tovuti yetu. Kubashiri tembelea sportpesa.co.tz au piga *150*87#

 

Share this: