skip to Main Content
JE YANGA KUCHUKUA KOMBE UGENINI DHIDI YA USM ALGER.
YangaAziz-Ki

JE YANGA KUCHUKUA KOMBE UGENINI DHIDI YA USM ALGER.

Mechi ya marudiano ya Kombe la Shirikisho itapigwa kesho Jumamosi kwenye dimba la Omar Hamadi, jijini Algiers, lenye uwezo wa kuchukua mashabiki 17,500 watakaowashuhudia USM Alger wakiwaalika timu ya Wananchi, Yanga kutoka Tanzania.

Mtanange huo wa marudiano ambao utaamua ni timu ipi iwe bingwa wa Kombe la Shirikisho msimu wa 2022/23 utapigwa kuanzia majira ya saa 4 Usiku, kwa saa za Afrika Mashariki.

Wenyeji wa mchezo wa kesho, USM Alger wao walichanga karata zao vyema kupitia mchezo wa kwanza uliopigwa kwa Mkapa Jijini Dar Es Salaam waliposhinda bao 2-1 na kupata faida ya kufunga mabao ya ugenini na kuwafanya Yanga kuwa na mlima mrefu wa kuupanda katika mchezo wa kesho June 3,2023.

Wachezaji waliozamisha jahazi la Yanga katika mchezo wa mkondo wa kwanza ni mshambuliaji Aymen Mahious na Islam Merilli wakati Fiston Mayele alifunga bao la kufutia machozi kwa Wananchi.

USM AlegrUSM Alger wao ili wawe mabingwa wanahitaji sare ya aina yoyote na kama kupoteza isiwe zaidi ya bao moja lakini wakipoteza kwa bao zaidi ya mbili tafsiri yake Yanga watakuwa mabingwa wa Kombe la Shirikisho.

Ugumu wa mchezo huu kwa Yanga unatokana na rekodi tata za USM Alger wanapocheza kwenye Uwanja wao wa nyumbani, kwakuwa katika michezo mitano ya michuano ya CAF msimu huu, wameshinda mechi zote, wamefunga mabao 13 na wameruhusu bao moja tu mpaka tunapoandika makala hii.

Balaa pekee ambalo USMA wanaweza kukutana nayo kutoka kwa Yanga ni kwamba Wananchi nao wameshinda mechi 4 kati ya 6 walizocheza ugenini katika mashindano hayo, wakipoteza moja tu dhidi ya US Monastir na sare dhidi ya Real Bamako.

Wakali wa Algeria walikuwa timu ya kwanza kuifunga Yanga katika Uwanja wa Mkapa kwenye michuano ya CAF, Je Yanga nayo inaweza kuvunja mwiko kwa USM Alger kwa kupoteza mchezo wa michuano hiyo kwa mara ya kwanza msimu huu?

Kupitia mchezo wa kwanza,ambao Yanga walipoteza, walikuwa na takwimu bora, walimiliki mchezo kwa asilimia 65 dhidi ya 35 za USMA. Yanga walipiga mashuti 15 huku (4) ndiyo yaliyolenga lango, wakati USM Alger walipiga mashuti 11(6) kati ya mashuti hayo ndiyo yaliyolenga lango.

Katika mchezo huo Yanga ilipata kona 9 wakati USMA ilipata kona 5, Yanga walipiga pasi 449 na USM Alger walipiga pasi 239.

Licha ya takwimu hizi kuonyesha Yanga aliukamata mchezo, lakini USM Alger ndio waliokuwa hatari zaidi na wachezaji wake walifanya matukio muhimu yenye tija katika mchezo huo katika dakika zote 90 za mchezo.

Katika takwimu(ratings) za utendaji kazi wa wachezaji inaonyesha nyota wa USM Alger walikuwa juu zaidi ya wachezaji wa Yanga, ambao wengi wao walionekana kutokuwa makini au kuwa na uwezo mdogo wa kumiliki mpira na kucheza kwa presha ya hali ya juu.

Mchezaji Azizi ki alionyesha mchezo wa kiwango kisichoridhisha na kupelekea mashabiki wa Yanga kumlalamikia hata baada ya mechi kuisha. Aziz Ki alitolewa na nafasi yake kuchukuliwa na Morrison ambaye alianzisha shambulizi lililopelekea Mayele kufunga goli la kusawazisha kwa kumpasia pasi ya kiufundi Mudathir yahya ambaye kwenye mechi hiyo alingára vilivyo.

Kinara kabisa alikuwa kiungo Haithen Loucif aliyepata (4.8) akifuatiwa na mfungaji Aymen Mahious (4.6 naye Islam Merilli (4.4).

Kiungo Loucif alihusika kutibua mipango ya Yanga na kumpoteza mchezoni Stephane Aziz Ki ambaye hakuwa na mchezo mzuri.

Upande wa Yanga wachezaji ambao walikusanya alama nzuri ni Fiston Kalala Mayele ambaye alipiga mashuti matano na kufunga bao moja kiwango kilichompa alama (4.3) sawa na Djuma Shaban ambaye licha ya kutokea benchi alipata alama (4.3) ambaye alipiga pasi muhimu 5 huku Bernard Morrison ndiye aliyekuwa kinara kwa Yanga akiwa na alama (4.4) tena akitokea benchi na kusababisha bao kwa pasi ya awali ilitotua kwa Mudathir Yahya kabla ya kumpa Mayele aliyefunga.

Kwa magolikipa, Oussama Bennot wa USM Alger alizuia michomo 8 wakati Djiguir Diarra alikuwa na siku mbaya kazini aliruhusu bao 2 na aliokoa michomo 4 katika mchezo huo.

Kocha Nassredine Nabi alisema walifungwa mabao ya kizembe ingawa akisisitiza mechi hiyo bado iko wapi sawa kabisa na Kocha wa USM Alger, Abdelhak Benchikha alisema kutokana na uzoefu alionao mechi hiyo iko wazi kwa Klabu zote.

Mechi hii Tayari ipo katika tovuti yetu. Kubashiria tembelea sportpesa.co.tz au piga *150*87#

Share this:
Back To Top