Unaweza ukasema bahati haina mwenyewe. Hivi ndivyo msemo wa Kiswahili ulivyotimia kwa mmoja wa washindi wetu wa Jackpot bonus ya kati kati ya wiki Maria kalosi Gwimile.
Mwanamke huyu ameshinda kitita cha Sh 11,766,592, baada ya kucheza Jackpot ya mechi kumi na tatu na kufanikiwa kupatia kwa usahihi mechi 12 kati yamechi 13.
Mshindi wetu huyu huyu anatokea maeneo ya Matosa, kule Goba, jijini Dar-Es-Salaam anajihusisha na shughuli za ujasiriamali wa bidhaa mbali mbali.
Akizungumza katika ofisi za SportPesa Oysterbay, Dar-Es-Salaam Maria anasema alianza kucheza na Sportpesa kuanzia mwaka jana, baada ya kuvutiwa na namna mume wake (hakumtaja jina) alivyokuwa akicheza na kushinda.
Mimi nilianza kucheza na SportPesa kuanzia mwaka 2022. Nilipata msukumo wa kucheza kutokana na namna mume wangu kipenzi alivyokuwa anacheza na mara nyingine anashinda. Nakumbuka siku mmoja mwanzoni mwa mwaka nilimtania nataka na mimi anifundishe namna ya kucheza’’.
Maria anaendelea kusimulia kuwa baada ya siku chache alianza kufundishwa kidogo kidogo namna ya kujisajili na pia kuweka hela na kucheza mechi chache kuanzia mechi mbili au tatu.
“Tangu nimefundishwa kucheza, naongelea mwaka mmoja uliopita, kwa kweli namshukuru Mungu naweza kucheza mwenyewe. Mimi napenda kucheza hizi Jackpot zaidi kwa kuwa hata usiposhinda moja kwa moja na ukakosea timu chache, labda moja mbili au tatu unapata bonus.
Kuhusu mkeka wa Jackpot bonus ya kati kati ya wiki alioshinda Maria anasema huwa ana kawaida ya kucheza kuanzia mkeka mmoja mpaka mitatu ya Jackpot aplae ambapo anakuwa na pesa ya kufanya hivyo.
‘’Kwa kweli mimi huwa najitahidi kila wiki nicheze mkeka mmoja mmoja, yaani kwenye Mid-Week Jackpot na kwenye Supa Jackpot. Mara chache ikitokea na uchumi unaruhusu, basi huwa najitahidi niweke miwili miwili hadi mitatu.
Mara nyingi kabla sijaweka mkeka wangu huwa najipa muda nikiwa nimetulia sina shughuli yoyote nachukua simu yangu ya Tecno naanza kuzifuatilia timu ambazo zipo kwenye list ya mechi za Jackpot.
Baada ya hapo nikisharidhika ndio huwa naweka timu zangu na mara nyingine huwa naziacha nikisubiria matokeo au kutegemea na aina ya mechi, basi hujaribu kuzifuatailia kwa kutizama wachezaji wangapi wapo katika kikosi.
Pia huwa naangalia wangapi hawatakuwemo, nani anaongoza kufunga magoli na timu gani kati ya mbili ina wastani mzuri wa kufunga na kufungwa magoli, pamoja na rekodi za nyumbani na ugenini’’.
Sasa katika mkeka wake Maria anadokeza kwamba aliweka mkeka wake siku ya Tarehe 17 ya mwezi Mei 2023. Baada ya kuweka mkeka huo, Maria anasema siku ya kwanza ya mechi za Jackpot, kuanza kuchezwa alipata mechi 9.
Kesho yake yaani jumamosi kuna baadhi ya mechi zilianza saa tisa alasiri na nyingine zilianza kuchezwa kuanzia saa moja usiku na kuendelea. Mpaka mida ya saa mbili na nusu kwenda saa tatu za usiku alishajua amebakisha mechi chache ili aweze aidha kushinda Jackpot au kupata bonus.
Mimi baada ya mechi ya saa moja usiku nilikuwa tayari nimepata mechi 10. Hapo presha ilianza kupanda kwa kuwa nilikuwa nimebakisha mechi chache kuchukua Jackpot ya kati kati ya wiki. Shauku yangu ilikuwa kubwa baada ya timu nyingine moja kushinda.
Hapo ilikuwa mida ya saa tatu na ushehe usiku. Huwezi kuamini ni kwa namna gani nilikuwa nimepagawa kwa kuwa nilikuwa na uhakika wa bonus ingawa sikuwa najua itakuwa shilingi ngapi kwa ujumla wake.
Niliachana na simu nikaiweka chaji na ilipotimu majira ya saa tano usiku niliangalia matokeo na kukuta nimeshinda mechi 12. Hapo nilijua nimeshinda hela nzuri ingawaje sikujua ni kiasi gani kwani huwa naona mara nyingi washindi wakitangazwaga wale waliopata hela nzuri kidogo huanzia mechi 11 au 12.
Nilipatwa na furaha iliyoje pale nilipopokea sms rasmi kutoka SportPesa. Nafikiri ilikuwa mida ya saa sita za usiku sms ile iliingia kwenye simu yangu. Nilimwamsha mume wangu na kumwambia nimeshinda Jackpot bonus ya milioni 11 na zaidi. Mme wangu aliniangalia kwa furaha na kunikumbatia.
Baadae nilipigiwa simu na mtoa huduma kwa wateja ambaye aliniambia kwamba ninahitaji kuja ofisi za SportPesa kwa ajili ya uhakiki na makabidhiano wa mfano wa hundi. Ndio hivyo leo nimefika na tayari nimeshapitia hatua hizo na kuzikamilisha.
Akimpongeza Maria kwa ushindi wa Jackpot bonus, mkuu wa kitengo cha mawasiliano wa kampuni ya SportPesa Sabrina Msuya alimtaka kuendelea kucheza Jackpot na huenda siku moja akabeba Jackpot kamili.
‘’Kwanza nikupongeze kwa ushindi wako huu ulioupata, pili wewe ni mshindi wetu wa tatu wa kike katika washindi wetu wa Jackpot bonus tangu mwaka huu umeanza.
Ni faraja kubwa kwetu na kwa akina dada wengine ambao wanatamani au hawaamini kama kwenye mchezo huu hata akina dada, wanawake na akina mama kama Maria wanaweza kushinda kama wewe.
Nitoe rai kwa watanzania wote, kujaribu bahati zenu, kwa kucheza Jackpot na bidhaa zetu zingine kama multibet na michezo ya kasino, kwani bahati haina mwenyewe. Alisema Sabrina.
Jackpot ya Mid-Week imesimamia TZS 591,377,690.

