Azam FC vs Yanga SC (-)Azam FC vs Yanga SC (-)
  • Kikosi cha timu ya Yanga SC leo Ijumaa kimerejea rasmi jijini Dar es salaam, kutokea mkoani Dodoma.
  • Mara tu, baada ya kutua Wananchi wameingia kambini kujiandaa na mchezo wa Azam FC vs Yanga SC.
  • Mchezo huo wa Ligi Kuu Bara (NBC Premier League). Uliopewa jina la ‘Dar es Salaam Derby’ utapigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa Jumapili ya Machi 15, mwaka huu.

Kuelekea mchezo wa Azam FC vs Yanga SC unaofahamika kama ‘Dar es Salaam Derby’ utakaopigwa siku ya Jumapili, Wananchi rasmi leo Ijumaa wametua jijini Dar es Salaam. Yanga SC watavaana na Azam FC katika mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaopigwa keshokutwa Jumapili Uwanja wa Benjamin Mkapa. Makala hii inakuletea dondoo muhimu kuhusu mechi hiyo.

SOMA HII PIA: NBC Premier League ratiba na CAF Champions League robo fainali

Je, bado hujashinda mamilioni? Cheza ‘Kindege’ cha SportPesa uvune pesa sasa

Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

image

Kuhusu mechi ya Azam FC vs Yanga SC

Mechi hii itapigwa Uwanja wa Mkapa siku ya Jumapili, haya yakiwa ni mabadiliko kidogo ya uwanja kulinganisha na ratiba ya awali. Mechi inatarajiwa kuanza majira ya saa 2:30 usiku. kwa saa za Afrika Mashariki. Matokeo yoyote ya mchezo huu yanaweza kutoa taswira ya mbio za ubingwa msimu huu, ikiwa imebaki miezi mitatu tu, kabla ya ligi kufikia tamati.

Azam FC vs Yanga SC h2h

Azam FC sv Yanga SC h-h
Azam FC sv Yanga SC h-2-h

Katika miaka ya hivi karibuni timu hizi zimekutana katika michezo 12, Yanga SC wamekuwa na rekodi bora zaidi wakishinda mechi 7. Azam FC wao wamefanikiwa kushinda mechi 3 tu, huku mechi 2 zilizosalia zikiisha kwa sare. Hii ni nafasi nyingine kwa kila upande kuandika rekodi mpya.

SOMA HII ZAIDI: Ratiba ya Yanga SC 2025/26 ni moto/ Mechi 5 NBC Premier League ugenini/ Msimamo, matokeo

Ratiba ya Yanga SC mwezi Machi, 2026

Kocha wa Yanga SC, Pedro Goncalves ameonekana kutoridhishwa na mpangilio wa ratiba waliyopangiwa. Kwa maelezo yake mechi zao zinaonekana kufuatana, angalau kla baada ya siku mbili. Ratiba ya Yanga SC katika mwezi Machi ilianza na moto wa mchezo wa Kariakoo Dabi, ambapo katika mchezo huo dhidi ya watani zao walitoa Suluhu.

Mechi nyingine zilizo katika ratiba ya Yanga Mwezi Machi ni kama ifuatavyo;

NBC Premier League wiki ya moto
Yanga SC vs Simba SC

Machi 1, 2026 Yanga SC vs Simba SC

Machi 5, 2026 Singida Black Stars   vs Yanga SC     

Machi 12, 2026 Tanzania Prisons    vs Yanga SC     

Machi 15, 2026 Azam FC vs Yanga SC

Machi 18, 2026 TRA United vs Yanga SC        

Machi 21, 2026 Mtibwa Sugar vs Yanga SC   

Msimamo unasemaje?

Mpaka sasa Wananchi wanakamatia usukani wa ligi na pointi zao 32 walizokusanya katika mechi 12 walizocheza. ‘Top Four’ na JKT Tanzania walio nafasi ya pili na Azam FC wanaokamatia nafasi ya 3. Simba wanasalia katika nafasi ya 4 na pointi zao 27 walizokusanya katika michezo 12.

SOMA HII PIA: AZAM FC V YANGA, MZIZIMA DABI YA KISASI, WANAUME 22 KAZINI

Tamko la kubadili uwanja kutoka Azam FC

Uwanja wa Benjamin Mkapa
Uwanja wa Benjamin Mkapa

Uongozi wa Azam umethibitisha kuwa mchezo wake dhidi ya Yanga, utakaopigwa Jumapili ya Machi 15, 2026 utachezwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa. Mabadiliko haya ni kutoka Uwanja wa Azam Complex, ambao ulipagwa awali Dar es Salaam. Azam pia wametoa sababu ya maamuzi hayo.

Akizungumzia hilo kupitia Chombo kimoja cha Habari, Ofisa Habari na Mawasiliano wa Azam FC, Thabit Zakaria ‘Zaka Zakazi’ amesema: “Kabla ya msimu kuanza, Azam FC tulichagua kutumia Uwanja wa Benjamin Mkapa kwa mechi zetu mbili za nyumbani. Mechi hizi ni dhidi ya Yanga na ile dhidi ya Simba SC badala ya Azam Complex. Tulivyoona taarifa kuwa Uwanja utafungwa kwa ukarabati, tukawa tunaangalia uwezekano wa mchezo huo kuchezwa katika Uwanja wa Azam Complex.

“Lakini wamiliki wa Uwanja wa Benjamin Mkapa wakatuelekeza kuwa, hautotumika pale maboresho yake yatakapoanza na sio kwa sasa hivyo tunaweza kuutumia. Uwanja wa Benjamin Mkapa tutakuwa na faida zaidi kucheza dhidi ya Yanga, kwa sababu tumeshakutana nao pale mara nyingi na tumewafunga sana katika Uwanja ule.”

Ikumbukwe mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu ambao Azam ilicheza katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, ulikuwa ni wa mzunguko wa kwanza msimu huu dhidi ya Simba ambao Azam waliibuka na ushindi wa mabao 2-0.

Matokeo ya mechi 6 zilizopita Yanga SC

Tanzania Prisons 0-1 Yanga SC NBC
Depuu

Februari 7, 2026/CAF AS FAR Rabat 1-0 Yanga SC

Februari 15, 2026/CAF Yanga SC 3-0 JS Kabylie     

Februari 22, 2026/NBC Namungo FC 0-1 Yanga SC        

Februari 25, 2026/NBC JKT Tanzania 0-5 Yanga SC        

Machi 1, 2026/NBC Yanga SC 0-0 Simba SC   

Machi 5, 2026 NBC Singida Black Stars 0-3 Yanga

Hitimisho

Azam FC vs Yanga SC mchezo mgumu wa Dar es Salaam Dabi, unasubiriwa kwa hamu kutokana na ubora wa timu zote mbili. Mchezo huu ni wazi unaenda kutoa taswira tofauti ya vita ya ubingwa. Kutokana na umuhimu wake ni kheri maandalizi ya kila timu yafanyike kwa uzito.

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.