skip to Main Content
Newcastle VS Arsenal -NI VITA YA WABABE WA EPL MSIMU HUU
ArsenalNewcastle

Newcastle VS Arsenal -NI VITA YA WABABE WA EPL MSIMU HUU

Kesho katika dimba la St. James Park, Newcastle United watakuwa wanawaalika washika mitutu wa London, klabu ya Arsenal ambao ndio vinara wa Ligi kuu ya England EPL.

Newcastle wapo katika nafasi ya 3 katika msimamo wa ligi wakiwa na alama 65, wakati Arsenal wamekamata usukuani wakiwa na alama zao 76 katika michezo 34 waliyocheza.

Mtanange huo unatarajiwa kuwa na upinzani mkali, huku ukitarajiwa kuvuta hisia mchanganyiko kwakuwa Newcastle United wameibuka kusikojulikana na sasa wapo kwenye kipaumbele cha kumaliza ndani ya nne bora.

Kwa upande wa Arsena itakuwa ni sehemu ya kuendelea kuanikiza nafasi ya ubingwa hadi tone la mwisho wa msimu huu, wakati ligi inaelekea kumalizika.

Ushindi kwa The Magpies ni muhimu kwani wakivuna alama tatu watafikisha 69 zitakazowasogezea karibu na ndoto zao za kushiriki Ligi ya mabingwa Ulaya msimu ujao,mbio ambazo wao na Man United wapo katika safari nzuri hadi sasa iwapo wataendelea kushinda mechi zao.

Upande wa Arsenal ambayo imezinduka kutoka usingizini walipoindunda Chelsea 3-1 na kuondoa mikosi ya kutokupata ushindi kwenye michezo minne ya nyuma,watahitaji alama 3 ili wafikishe alama 81 ambazo zitaendelea kuwaweka katika kinyang’anyiro dhidi ya Manchester City wenye mechi mbili za viporo.

Eddie Howe ameibuka shujaa wa Newcastle United ambaye hadi sasa ni kama ameushangaza ulimwengu kwa kuingia kwenye njia ya vigogo Liverpool,Tottenhan Hotspurs,Chelsea na hata Man United na sasa kikosi chake ambacho kinajengwa baada ya matajiri kutoka Saudi Arabia kuichukua timu hiyo.

Wengi waliamini kutokana na utajiri mkubwa wa Amanda Staveley na Yasir Al-Rumayyan basi tungeshuhudia usajili wa majina makubwa lakini ikawa tofauti sana.

Tukaona ingizo la nyota kama Alexander Isak, Bruno Guimares, Kieran Trippier,- Antony Gordon, Nick Poppe, Matt Target, Sven Bottman umeonekana kulipa kwa kiasi kikubwa.

Upande wa Arsenal ambayo nayo imeibukia kutoka kusikojulikana kwenye kuwania ubingwa msimu huu, wakupongezwa ni Mikel Arteta na Mkurugenzi wa Ufundi wa kikosi hicho Edu.

Hawa wawili wanahusika kwa ailimia 100 katika sajili zenye tija mfano rahisi ni wa mchezaji Gabriel Jesus ambaye amefunga mabao 10 katika EPL hadi sasa.

Mchezaji Oleksandr Zinchenko kutoka Manchester City.  Leandro Trossard kutoka Brighton ameingia kipindi cha dirisha dogo na tayari ameshatoa pasi 8 za mabao.

Wachezaji Joginho kutoka Chelsea na William Saliba kutoka Marseille kwa pamoja  wameimarisha ukuta wa The Gunners kwa kiasi kikubwa na kufanikiwa kuifanya Arsenal kuwa imara msimu huu, tofauti na misimu ya nyuma.

Mara ya mwisho Newcastle United kupoteza mchezo ilikuwa March 4,2023 waliponyukwa na Manchester City bao 2-0 lakini tangia muda huo tim hiyo imeshinda mechi 9 mfululizo  na katika michezo mitatu ya mwisho wamefunga 13 wakiruhusu mabao matatu pekee.

Upande wa The Gunners wao wamekuwa na matokeo mchanganyiko ambapo ukiachana na mechi nne za mwisho kabla ya ushindi dhidi ya Chelsea,wamecheza mechi 7 za EPL ambazo wameruhusu bao katika kila mchezo jambo ambalo lina ashiria kuwa safu yao ya ulinzi imeweweseka kwa sasa.

Arsenal imefunga mabao 81 katika Ligi Kuu ,idadi kubwa kuliko Newcastle waliofunga mabao 61 lakini The Gunners wameruhusu mabao 39 huku Newcastle wakiruhusu 27 tu huku takwimu nyingine inayovutia ni kwamba wapinzani hawa wawili wote wamepoteza mechi 4 kila mmoja katika Ligi Kuu ya England msimu huu.

Timu hizi zinavutia kutokana na namna ambavyo wachezaji wao wana takwimu bora zinazokaribiana ambazo zinaweza kuzalisha namba nzuri katika mchezo huo.

Mfano kinara wa kupachika mabao kwa Newcastle ni Callum Wilson aliyefunga bao 15, akifuatiwa na Miguel Almiron mwenye bao 11. Naye Aleksander Isak ana magoli 10.

Kwa upande wa Arsenal vinara wa mabao ni Gabriel Martinelli mwenye magoli 15, akifuatiwa na Martin Odegaard (14), Bukayo Saka (13) na Gabriel Jesus ana magoli 10.

Hii ni ishara tosha kwamba timu zote mbili zinawafungaji hatari, hivyo mchezo huu baina yao unatarajiwa wenye upinzani mkali na unategemewa kuzalisha magoli mengi.

Wachezaji wa Newcastle United wakijiandaa dhidi ya ArsenalTukigeukia kwa wakali wa kutoa pasi za mabao, Newcastle United inatamba na Kieran Trippier (6), Joseph Willock (6), Bruno Guimares(5) na Allan Saint-Maximum (5).

Kwa upande wa Arsenal vinara wanaoongoza kwa kutoa pasi za mwisho au ‘’assist’’ ni pamoja na Bukayo Saka (11), Martin Odegaard (8), Leandro Trossard(8) na Granit Xhaka (7).

Gabriel Martinelli ndiye anayeongoza kwa kupiga mashuti yaliyolenga lango(30) akifuatiwa na Gabriel Jesus na Martin Odegaard. Kila mmoja  kati yah awa wachezaji amepiga mashuti 27 wakati kwa Newcastle kinara ni Callum Willson(28), Alexander Isak (22) na Miguel Almiron(18). hivyo ni timu ambazo zinauwezo mzuri wa kusaka nafasi ya kufunga.

Rekodi inatuonyesha kwamba wababe hawa wamekutana mara 49, Newcastle imeshinda mara 6, wakati Arsenal imeshinda michezo 32, huku michezo 11 ikimalizika kwa sare.

Timu zote mbili zina wastani wa kutoa mabao 2.45.

Katika mechi mbili za mwisho kwa timu hizi kukutana, Newcastle imeshinda mechi moja na suluhu moja, wakati Arsenal haijapata ushindi.

Ni matumaini yetu kwa takwimu hizi tulizokuwekea katika makala hii itakupa mwanga ni kwa namna gani ubashiri mechi hii.

Ili kucheza tembelea sportpesa.co.tz au piga *150*87#.

Share this:
Back To Top