skip to Main Content
JACKPOT BONUS YA SPORTPESA YAENDA ZANZIBAR
Seif-kundi-

JACKPOT BONUS YA SPORTPESA YAENDA ZANZIBAR

Waswahili wanamsemo ‘’hakuna linaloshindikana chini ya Jua’’. Hivi ndivyo msemo huu ulioasisiwa na mababu zetu ulivyotimia kwa Seif Kundi Seif, mfanyakazi wa hoteli anayepatikana maeneo ya Amani kisiwani Zanzibar.

Kijana huyu wa makamo ameweza kujishindia Jackpot bonus ya Supa Jackpot ya SportPesa ya Sh 5, 423,697 baada ya kupatia kwa usahihi mechi 14 kati ya 17 alizocheza kwenye Jackpot iliyochezwa mwisho wa wiki ya Tarehe 30 April 2023.

Akizungumza baada ya uhakiki na makabidhiano ya mfano wa hundi, seif anasema alianza kucheza na SportPesa kuanzia mwaka 2020, baada ya washkaji zake wa karibu kumwambia kuna fursa ya katika mtandao wa SportPesa.

‘’Mimi nilikuwa sijui mambo haya ya ubashiri lakini nakumbuka nikiwa nimetulia na marafiki zangu miaka kama miwili iliyopita walinishawishi na mimi nianze kucheza ama kubashiri kama wao. Si unajua kwetu kule mambo haya hayako wazi kama mahala pengine nchini.

Ilinichukua muda kuweza kukubaliana na wazo kutoka kwa marafiki zangu kwamba na mi nianze kucheza hii michezo. Nilianza kwa kujifunza kidogo kidogo kwa kutumia simu janja na baada ya muda nilijua namna ya kucheza.

Baada ya kujua namna ya kucheza  nilibahatika kuwahi kushinda Tshs 62,000  katika michezo ya mechi nyingi, inayojulikana kama multibet. Hiyo ilinitia moyo na hivyo kuendelea kucheza. Kwa kweli kabla ya kupata ile hela niliyoshinda nilikuwa naliwa tu.

Nilitaka kukata tamaa na kuacha kucheza, Sasa jambo moja lilinijia kichwani niachane na mchezo huu, lakini maskini ya mungu, siku kata tamaa, pamoja na kwamba sikujua kama huku mbeleni nitakuja kushinda kiasi kikubwa cha pesa. Anasema Seif.

Anaendelea kwa kusema kwa Supa Jackpot yeye ni mara yake kucheza na anamshukuru Mungu mara moja hiyo imekuja na baraka na amefanikiwa kushinda Jackpot bonus ya Supa Jackpot katika wakati muhimu wa maisha yake.

‘’Kwa hakika najisikia furaha sana kushinda fedha hii, kwa sababu itafanya nikamalizie nyumba yangu ambayo ilikuwa imekaa muda mrefu bila kuendelezwa’’.

Kuhusu mkeka wa Supa Jackpot ambao umeshinda Seif anasema aliuweka Tarehe 18/4/2023. Yeye huwa na kawaida akirudi nyumbani baada ya kufanya kazi siku nzima, hutulia kwanza alafu hutafuta muda wa kukaa na kutulia.

Baada ya hapo huchukua simu yake na kuanza kuchambua timu. Sasa kwa mkeka huu ambao umeshinda anasema aliweka mkeka mmoja tu.

Jackpot bonus SMS‘’Mimi nafikiri kwa watu wenye bahati, nafikiri na mimi ni mmoja wapo. Kwa hili namshukuru Mungu sana kwa kunijalia baraka kubwa namna hii, kwa sababu mkeka huu nilioshinda ndio mkeka wa kwanza kwenye Supa Jackpot niliyouweka tangu nimeanza kucheza na SportPesa. Anasema Seif.

Anadokeza kuwa kutokana na presha ya matokeo kwa timu ambazo amezibashiria huwa hazifuatilii mpaka pale ambapo mechi zote zitakapokuwa zimeisha. Na baada ya hapo ndio anaweza kuangalia baadhi ya mechi kuona amepata kwa kiasi gani.

Seif anaendelea kusema alipata sms ya ushindi wakati yupo na washikaji zake wametulia lakini hakuamini kama kweli ile sms ilikuwa inamaanisha kwamba ameshinda zaidi ya Milioni 5.

‘’Wakatai sms ya ushindi wangu inaingia mimi nilikuwa kitaani kwangu na marafiki zangu tunapiga stori za mambo mbali mbali ya kijamii na michezo na mambo ya vijana. Sasa wakati ile sms inaingia niliingalia nikawaambia washikaji zangu jamani, kuna sms imeingia inanipa hongera nimeshinda bonus ya zaidi ya Tsh milioni 5.

Seif Kundi akishikilia mfano wa hundi wa pesa ya Jackpot bonus aliyoshindaKwa wakati ule, washikaji zangu ndio walikuwa na shauku, na kwakuwa mimi ushindi huu ni mara yangu ya kwanza kushinda kiasi kikubwa cha hela kwenye ubashiri, nilikuwa natafakari kama kweli nitalipwa hiyo pesa kwa sababu maneno ya huku mtaani watu hawalipwi wanazungushwa zungushwa tu.

Sasa baada ya muda watu wa huduma kwa wateja wa SportPesa waliwasiliana na mimi na kunitaka kufika ofisini, kama ambavyo unaniona leo kwa ajili ya uhakiki. Hapo ndipo mimi nilipoamini’’.

Anamalizia kwa kuwashauri watanzania wenzake hasa hasa vijana kuwa na malengo kwani kwenye michezo hii ukiwa na malengo ni rahisi kufanikiwa.

‘’Nipende kuwashauri vijana wenzangu kwanza kuwajibika, pili kuwa na malengo wakati unacheza. Kwangu mimi hii pesa nitaenda kumalizia kibanda change ambacho kilikuwa kimekaa muda mrefu bila kuendelezwa’’.

Akimpongeza Seif kwa ushindi wake wa Jackpot bonus ya kati kati ya wiki, Mkuu wa kitengo cha mawasilinao SportPesa Sabrina Msuya alimpa pongezi na kumtaka kuendelea kucheza Jackpot za Sportpesa, Multibet pamoja na michezo mingine kama ya Kasino na Virtual Pro.

Jackpot ya kati kati ya wiki kwa wiki hii imesimamia TZS 575,472,890.

Share this:
Back To Top