Bayern MunichBayernMancity

Kipute cha michezo ya mkondo wa pili Ligi ya mabingwa bara la Ulaya, (UEFA Champions Legue) kitaendelea tena kesho, Jumatano ya April 19,2023, safari hii ikiwakutanisha timu ya Bayern Munich dhidi ya Manchester City, wakati Inter Milan watakuwa nyumbani wakiwakaribisha Benfica.

Manchester City wakiwa nyumbani Etihad waliwavurumisha Bayern Munich kwa kipigo kizito cha bao 3-0, shukrani za dhati kwa nyota wake Rodri,Erling Braut Haaland na Bernardo Silva waliosababisha ushindi huo huku ukiwaacha The Bavarians wakibaki na mshangao na kuwapa kazi nzito katika mchezo wa marudiano.

Upande wa Inter Milan wao wakiwa ugenini Estadio da Luz waliwashangaza Benfica kwa kuwapa kipigo cha bao 2-0 huku Nicola Barrela na Romelu Lukaku ndio nyota waliowapa Nerrazuri ushindi huo muhimu huko nchini Ureno.

Tukianza kwa Bayern Munch ambao kipigo kutoka kwa Manchester City kilikuwa ni cha kwanza katika michuano hii mikubwa ya Ulaya,wana mlima mrefu wa kupanda ikizingatiwa kiwango kilichoonyeshwa na The Citizen ni cha hali ya juu sana ikilinganishwa na wao.

Licha ya Bayern Munich kuwa na umiliki wa mchezo kwa asilimia 54 dhidi ya 46 za Manchester City lakini vijana wa Pep Guardiola walikuwa wakicheza kwa malengo zaidi ya kuumaliza mchezo, The Citizens walipiga jumla ya mashuti 9 yaliyolenga lango wakati Bayern walipiga mashuti 4 tu,mashuti ambayo hayakulenga lango ya Man City yalikuwa 5 wakati Bayern ni 3.

Takwimu zinaonyesha pia Man City ilipata kona 8 wakati Bayern walipata kona 5, The Citizen walipiga krosi 22 wakati Bayern Munich walipiga krosi 15, mashambilizi ya kushtukiza kwa Man City yalikuwa 5 wakati The Bavarians yalikuwa 6, kipa wa Man City,Ederson aliokoa hatari 4 wakati wa Bayern Munich Soma aliokoa hatari 6.

Ukipitia takwimu hizi unakiri kuwa Manchester City walikuwa bora na hatari zaidi kuliko Bayern Munich licha ya kwamba katika mchezo wa mpira wa miguu lolote linaweza kutokea.

Bayern Munich wakiwa Allianz Arena huwa wanabadilika lakini tayari wametengeneza tofauti kubwa ya idadi ya mabao,ingawa kwa aina ya wachezaji walionao kama Leroy Sane,Sadio Mane,Thomas Muller,Serge Gnabry unaweza kusema wanayo nafasi ya kupindua matokeo.

Kwa Thomas Tuchel mchezo huo ulikuwa ni wa tatu kwake tangu achukue mikoba ya kocha Julien Naggelsman ambapo ameshapoteza miwili na kushinda mmoja tu dhidi ya Borussia Dortmund.

Kocha Tuchel alikosolewa kwa uteuzi wa kikosi cha kwanza ambacho hakuwajumuisha washambuliaji asili kama Thomas Muller na Maxim Choupo Moting  vilevile Sadio Mane walioanzia benchi.

Kitendo hicho kinasadikika kuifanya safu ya ulinzi ya Man City kuwa huru na kumuacha Ederson kutopata misukosuko na kuanzisha mashambulizi kama ilivyo kawaida yake.

Ukiachana na hilo Thuchel alisema kuelekea mchezo wa marudiano siku ya kesho mechi bado ni ngumu na kwakuwa itachezwa Ujerumani lolote linaweza kutokea.

Rekodi zinaonyesha mara ya mwisho Manchester City kucheza katika dimba la Allianz Arena ilikuwa Julai 29,2028 ambapo The Citizens waliibuka na ushindi wa bao 3-2, hivyo tafsiri yake ni kwamba licha ya ushindi walioupata Etihad lakini bado Pep Guardiola kwa aina ya timu aliyonayo wanaweza kulazimisha ushindi wakiwa hata nchini Ujerumani.

ACMilanNapoliIkumbukwe Pep Guardiola anawania taji lake la kwanza la UCL tangu afanye hivyo alipokuwa na Barcelona na njia pekee aliyonayo ni kuhakikisha anaiondoa Bayern Munich ambayo nayo alishindwa kuipa mafanikio katika michuano hii hivyo bila shaka atatilia mkazo mchezo huo.

Upande wa Inter Milan,watakuwa Guisepe Meazza nchini Italia wakiwa na kazi moja tu ya kupunguza machungu ya kutokufanya vizuri katika Sere A,ambako hawana mwenendo mzuri na wanapambana kumaliza nafasi ya nne.

Ushindi wa bao 2-0 umewafanya vijana wa Kocha Simone Inzaghi kuwekeza nguvu zao katika michuano hiyo ambayo mara ya mwisho kwa kutwaa ubingwa ulikuwa ni msimu wa 2009-2010 walipokuwa wakinolewa na mjivuni Jose Mourinho ambaye kwa sasa yupo na AS Roma.

Takwimu za mchezo wa kwanza zinaonyesha Inter Milan walipiga mashuti manne tu yaliyolenga lango, na na mawili yalizalisha mabao mawili, huku wenyeji Benfica walipiga mashuti mawili tu, yaliyolenga lango lakini hawakufunga.

Inter walipiga mashuti matatu ambayo hayakulenga lango huku Inter wao walipiga matano, Benfica walimiliki mchezo kwa asilimia 57 wakati Inter walimiliki kwa asilimia 43.

Wenyeji walipata kona 4 wakati wageni walikuwa na kona 6, Benfica walipiga krosi 22 wakati Inter walipata krosi 19, Inter walifanya mashambulizi ya kushtukiza manne huku Benfica walishindwa kufanya hivyo hata mara moja, na walinda milango wa timu zote walizuia michomo ya hatari mara 2 kila mmoja.

Kwakuwa Inter Milan ni wazoefu wa michuano hii ya Ulaya na wameshatwaa taji hili mara tatu, haitokuwa kazi rahisi kuutupa ushindi wa bao 2-0 walioupata ikizingatiwa wanao washambuliaji hatari kama Lautaro Martinez, na kina Romelu Lukaku, ambao wanauwezo mkubwa wa kupachika mabao tena wakiwa nyumbani na mashabiki wao nadhani utakuwa mlima mrefu kwa Benfica kupindua matokeo.

SportPesa tayari tumeshakuwekea mechi hii. Kubashiri tembelea sportpesa.co.tz au piga *150*87#

Share this: