skip to Main Content
SPORTPESA YACHANGIA SACCOSS YA KINA MAMA KIZIMKAZI.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi SportPesa Tarimba Abbas akitoa salamu za ponezi kwa raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwananchi wa Kizimkazi kwenye kilele cha Kizimkazi day, Zanzibar.

SPORTPESA YACHANGIA SACCOSS YA KINA MAMA KIZIMKAZI.

Kampuni ya michezo ya burudani na ubashiri Sportpesa wikiendi imeshiriki Tamasha maalum la kizimkazi na kuchangia mfuko wa Saccoss ya kina mama kwa ajili ya kuboresha hali zao za kiuchumi.

Akizungumza wakati wa tamasha, baada ya kupewa nafasi ya kutoa neno la shukrani, Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya Sportpesa Tarimba Abbas, alimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu kwa mwaliko na pia kwa nafasi ya ushiriki.

‘’Napenda kuchukua nafasi hii kukushukuru kwa kunialika mimi binafsi na kwa upande mwingine kampuni yetu ya Sportpesa, na pia kwa kunipa nafasi ya kutoa neno la shukrani kwa wananchi wa eneo hili’’.

Tarimba anaendelea kusema kwamba kampuni ya Sportpesa ilivutiwa na wazo la kushiriki kuchangia ama kuongeza mtaji kwenye Saccoss ya akina mama, ambapo kupitia saccoss hiyo akina mama watapata fursa ya kupata mikopo midogo midogo itakayowasaidia katika kuboresha hali zao.

“Kwa kuanzia Kampuni yetu ya Sportpesa tayari imeshatia fedha katika Saccoss hiyo ya akina mama na nisingependa kutaja kiasi ila tambueni ni fedha nyingi. Na pia inshallah mwakani pia tutaweka tena fedha zingine ili iwe chachu ya kuleta maendeleo kwa akina mama’’. Alisema Tarimba.

Akimalizia Tarimba alimshukuru Rais Samia kwa namna ambavyo amepeleka maendeleo katika jimbo la Kizimkazi ambapo kwa yeyote ambaye ameshabahatika kufika miaka kadhaa iliyopita ataona tofauti baina ya siku za nyuma na sasa.

‘’’Napenda kukupa pongezi kwa namna ulivyowaletea maendeleo wananchi wa maeneo haya kwani kwa sisi ambao tumebahatika kufika hapa mara kwa mara tunaona tofauati.

Kwa mara ya kwanza SportPesa ilishiriki kwa kukarabati nyuma ya madaktari wawili ambazo zinatoshelezea familia mbili ili kuhakikisha urahisi wa wanakizimkazi kupata huduma pale inapohitajika.

Kama ilivyo nia ya SportPesa kuendeleza na kukuza mpira wa miguu nchini tuliendea kudhamini timu ndogo ndogo za mpira wa miguu kwa kuwapatia vifaa vya michezo ikiwemo jezi.

Share this:
Back To Top