Nani kushinda SportPesa Jackpot 985,669,400/- kwa dau la 2000 tu?
03.03.2022 Dar-Es-Salaam Kampuni ya burudani na michezo SportPesa inapenda kuutaarifu, uma wa watanzania, wadau na wapenda michezo ya kuwa Jackpot yetu endelevu imefikia kiwango cha shillingi 985,669,400.
Akizungumza na waandishi wa Habari Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Tarimba Abbas alianza kwa kuwakaribisha waandshi wa Habari kwenye mkutano huo’
“Tunapenda kuchukua fursa hii kutoa taarifa kupitia vyombo vyote vya habari hapa nchini kwamba kwa sasa hakuna kampuni yoyote yenye dau kubwa zaidi ya hili na kumtangaza mshindi wa Jackpot kubwa kama hii, ambapo mpaka sasa hii ni mara ya tatu kwa Jackpot endelevu kupanda kwa dau zaidi ya nusu bilioni, baada ya kuanzia shilingi milioni 200.
“Kwa hakika, kiwango hiki kama hakitapata mshindi mwishoni mwa wiki hii, basi dau litakalofuata, litaweka historia ya kuwa dau la kwanza la ubashiri kufika bilioni moja kwa viwango vya Jakipoti endelevu nchini”
‘’Tunapenda kuwasisitiza watanzania wote kwa ujumla kucheza mara nyingi kadiri muwezavyo Ili kupata nafasi kubwa ya kushinda Jackpot hii nono ambayo ilianza kushindaniwa kuanzia mwezi wa 4, 2021 baada ya mshindi wa 7 wa Jackpot Abdulaziz Ngámilo kupatikana.
“Jambo jema ama zuri kwa wachezaji ni kwamba hata kama hukufanikiwa kushinda dau hili moja kwa moja una nafasi nyingine ya kushinda kupitia Jackpot bonasi kwa washindi wanaopatia kuanzia timu 10,11 na 12’’. Alisema Mkurugenzi wa utawala na udhibiti. Tarimba Abbas.

Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi SportPesa Tarimba Abbas akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Jackpot ya SportPesa ya TZS. 985,669,400 katika ofisi za Sportpesa jijini Dar es Salaam.
Tangu kuanza kwa Jackpot hii karibu miezi 11 Iliyopita, SportPesa tumeshatoa washindi wa kitanzania zaidi ya 200 kila wiki kwa waliobashiri kwa usahihi kuanzia mechi 10, 11 na 12.
“Washindi wa SportPesa jackpot kwa mara ya kwanza walipatikana mwaka 2019 Agosti ambapo Magabe Marwa na Kingsley Pascal waligawana 825,913,8640 Tsh baada ya jackpot hii kukaa kwa miaka miwili.”
“Kwa mara ya pili na tatu walipatikana washindi wengine ambao ni Scolastika Ngwaluweson na Jamal Khalfan Abdallah ambapo waliondoka na kiasi cha shilingi 260,319,980Tsh na 288,974,720Tsh kila mmoja.”
“Washindi waliofata ni Lilian Laizer na Yassini Ridhiwani ambao walijishindia 267,800,060 Tsh na 437,631,320 Tsh kila mmoja.”
Akiongezea kuhusiana na dau hilo na namna ya kushinda, Meneja uhusiano wa kampuni ya Sportpesa amewataka watanzania kuchangamkia fursa bila kusita wala kuwa na visingizio ili kuwa mabilionea.
‘’Jackpot ndio njia rahisi kabisa ya kuwa bilionea ajae kwa kufuata taratibu nyepesi za uchezaji, kwa kutumia mitandao yetu ya kijamii na tovuti ya sportpesa. www.sportpesa.co.tz, App ya sportpesa na USSD (*150*87#) alisema Sabrina Msuya.
Story za washindi mbalimbali wa Jackpot bofya hapa.
MWISHO