Steven MukwalaSteven Mukwala
SIMBA
Kocha, Fadlu Davis (mwenye t-shirt ya nyeupe)

Zikiwa zimesalia siku chache kabla ya kufungwa kwa dirisha kubwa la usajili, hatimaye kocha mkuu wa Simba, Fadlu Davis amekiri kuwa timu yao ipo katika mpango wa kusajili straika mpya wa kuiongezea nguvu timu hiyo.

Akizungumzia kuhusu mahitaji hayo ya kikosi chake kocha, Fadlu kwenye mkutano na waandishi wa habari wa maandalizi ya mchezo wa kusaka mshindi wa tatu ambao utapigwa kesho Jumapili kocha juyo alikiri kuwa jambo hilo aliliweka wazi kwa viongozi wao kabla ya mchezo wa kilele cha Simba day tamasha ambalo limewahi kudhaminiwa na Kampuni ya michezo ya kubashiri ya SportPesa wakati ikiwa mdhamini mkuu wa timu hiyo.

“Kabla ya mchezo wetu wa kilele cha siku ya Simba Jumamosi iliyopita niliweka wazi kuwa bado tuna mahitaji kwenye eneo la ushambuliaji na tuna kazi ya kufanya.

“Nafurahia ubora wa kikosi nilichonacho, napewa sapoti kubwa kutoka kwa viongozi, najua wanafanya kazi kubwa nyuma ya pazia, tuna siku 5 kabla dirisha la usajili halijafungwa subiri tuone nini kitatokea.”

ISHU YA KAGOMA, AWESU, MASHAKA, NGOMA BADO NGUMU

Wakati Simba wakiendelea kupambana kuhakikisha wanapata saini ya straika mpya kwa bajili ya kukiongezea makali kikosi chao, inaelezwa mastaa watatu wa timu hiyo ambao ni, Valentino Mashaka, Awesu Awesu na Yusuph Kagoma wanakabiliwa na kesi za mapingamizi ya kuichezea timu hiyo kwa sababu mbalimbali.

Taarifa kutoka ndani ya timu hiyo na watu wa karibu wa wachezaji hao zimethibitisha kuwa wachezaji hao watatu wana mashauri tofauti ya mapingamizi kutoka kwenye timu zinazowasimamia.

MWANASHERIA KMC AFUNGUKA KUHUSU AWESU AWESU

SIMBA
Awesu Awesu

Kuhusiana na nyota huyu, taarifa za ndani kutoka kwa Mwanasheria wa KMC, Chief Said amesema: “Walichokifanya Simba ni kumsajili Mchezaji ambaye ana mkataba wa miaka miwili na KMC, ni kweli kuna kifungu ambacho kinamruhusu Mchezaji kuondoka kwa thamani hiyo ya Milioni 50.

“Lakini mwisho kifungu kinasema kwa kufuata taratibu za klabu ambazo Simba na Awesu Awesu hawakuzifuata ndio maana fedha yake tulimrudishia, kama wanamtaka Mchezaji waje mezani na MILLION 200”

YANGA WAKOMAA NA YUSUPH KAGOMA

SIMBA
Yusuph Kagoma

Kuhusu ishu ya kiungo, Yusuph Kagoma yeye amewekewa pingamizi na Yanga ambao wanadai ni mchezaji wao na wanataka kurudishiwa fedha zao.

Kuhusu Valentino ishu yake inataka kufanana na Awesu kwani uongozi wa Geita Gold una dai kuwa nyota huyo amesajiliwa na Simba bila wao kuhusishwa.

KESHO JUMAPILI FAINALI KINAWAKA KWA MKAPA

Ukiachana na masuala ya kesi za masuala ya usajili ambazo zinaendelea ndani ya Simba, timu hiyo kesho Jumapili inatarajiwa kushuka uwanjani kuvaana na Coastal Union katika mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu wa mashindano ya Ngao ya Jamii.

Simba ambao walikuwa mabingwa watetezi wa mashindano hayo walivuliwa ubingwa na Yanga juzi Alhamisi baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0 katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Mara baada ya matokeo hayo Yanga sasa watavaana na Azam katika mchezo wa fainali ambao utapigwa kesho Jumapili.

Kuelekea michezo hiyo, Simba, Yanga wanasemaje?

ALLY KAMWE

Baada ya ushindi dhidi ya Simba, Ofisa habari wa Yanga akiwa na uzi wa SportPesa, Ally Kamwe amesema: “Tulikuwa na nafasi ya kupata matokeo mazuri zaidi ya mabao mengi dhidi ya Simba, lakini maamuzi ya waamuzi waliosimamia mchezo ni kama yaliwasaidia Simba kuepuka kipigo kikubwa.

“Sisi kama Yanga tumeridhishwa na ubora wa kikosi chetu na hii inaonyesha tumedhamiria kufanya nini msimu huu, sasa huu ni ujumbe kwa Azam FC kuwa Jumapili wanapaswa kujipanga kwa dozi nzito, tunafahamu ubora wa kikosi chao na tumejipanga kuhakikisha tunashinda ubingwa huu.”

AHMED ALLY

Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally akizungumzia kikosi chao amesema: “Tunakila sababu ya kujivunia maendeleo ya ‘Project’ yetu ya muda mrefu iliyohusisha wachezaji wengi wapya, wenye vipaji vikubwa na umri mdogo. Wanasimba matokeo yaliyopita yasiwatie unyonge kwani tupo katika njia sahihi sana na punde tutaanza kuogelea kwenye mito ya asali na maziwa.

“Hii ni tofauti na msimu uliopita tulichukua ngao ya jamii lakini hatukua na timu imara ndio maana tulikosa Mataji yote, Msimu huu tumekosa Ngao ya Jamii lakini tunayo timu imara ya kutupa heshima hapo baadae, na tunaanza na mchezo dhidi ya Coastal Union Ubaya Ubwela.”

 

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.