ITAFAHAMIKA Uwanja wa Mkapa kwenye hatua ya nusu fainali ya Ngao ya Jamii, Agosti 8 2024 kwa kutambua nani atakutana na mshindi wa mchezo wa nusu fainali itakayochezwa Zanzibar Agosti 8 2024 Simba itakuwa na mchezo dhidi ya Yanga, Uwanja wa Mkapa nusu fainali ya Ngao ya Jamii mshindi atacheza fainali Agosti 11 na mshindi wa nusu fainali kati ya Coastal Union na Azam FC.
Bofya link hii hapa ubashiri mechi zote za Ngao ya Jamii, Agosti 8 2024 https://sportpesa.co.tz/

Bruno Ferry, Kocha Mkuu wa Azam FC ameweka wazi kuwa wamefurahi kukutana na Coastal Union kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii kwa kuwa wanatambua ni moja ya timu nzuri. Miongoni mwa wachezaji waliopo katika kikosi cha Azam FC ni Yannick Bangala, Feisal Salum.
“Tumefurahi kukutana na Coastal Union kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii. Hii ni timu nzuri kwa kuwa tulikutana nao kwenye mechi za ligi lakini tupo tayari kupata matokeo mazuri uwanjani mbele yao.”
Kocha wa Coastal Union David Ouma ameweka wazi kuwa wanamachaguo mawili kwenye mchezo wa nusu fainali,kuchagua wawe wakakamavu ama wawe wavivu kwa kurudi nyuma katika kupambania vikombe.
“Kuna mbinu ambazo tumepanga kuzitumia kuwakabili wapinzani wetu Azam FC kwani tunatambua ni timu imara. Tuna mambo mawili ya kuchagua, ama kujikaza kuwa wakakamavu tuendelee kupambania vikombe au tuwe wavivu na kuanza kurudi nyuma.”
ITAFAHAMIKA KUTOKA JANGWANI
Miguel Gamondi, Kocha wa Yanga amesema wanatambua ni mchezo mgumu kuwakabili Simba katika Ngao ya Jamii wapo tayari kupata matokeo mazuri kwa kuwa yaliyopita hayana nafasi bali ni kuangalia wakati uliopo.
“Yaliyopita hayo hatuyatazami bali tunaangalia kile kilichopo mbele kwa sasa ambacho ni kupata matokeo mazuri na maandalizi yapo vizuri kwa ajili ya mchezo wetu, Nina amini wachezaji watafanya vizuri mashabiki wajitokeze kwa wingi.”.
HUYU HAPA KOCHA WA UNYAMANI

Fadlu Davids, Kocha Mkuu wa Simba amesema: “Tunahitaji kuanza msimu na kombe hilo litatuongezea nguvu kwenye mechi zijazo, tupo tayari na tunaamini tutafanya vizuri.”
Mohamed Hussen nahodha wa Simba amebainisha kuwa wapo tayari kwa mchezo wao wa Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga na hesabu kubwa ni kupata matokeo mazuri kwenye hatua ya nusu fainali ili kutinga fainali.
“Tunaamini tutakuwa na mchezo wenye ushindani na wachezaji tupo tayari kwa ajili ya mchezo wetu hivyo mashabiki wajitokeze kwa wingi kutupa sapoti.”
Kwa upande wa Yanga, kiungo Aziz Ki mwenye tuzo ya MVP, mfungaji bora ambaye alifunga jumla ya mabao 21 kwenye ligi hivi karibuni aliweka wazi kuwa malengo yao ni kupata matokeo kwenye mechi ambazo wanacheza.
“Tunashirikiana na wachezaji kutafuta matokeo uwanjani hilo linatupa nguvu ya kutazama yale yanayofuata, hatufikirii yaliyopita bali tunafikiria sasa.”
REKODI ZA NGAO YA JAMII

Septemba 25 2021 kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii, Simba mapema walipoteza mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa. Baada ya dakika 90 ubao ulisoma Simba 0-1 Yanga.
Bao la ushindi kwa Yanga lilifungwa na Fiston Mayele dakika ya 12 kwa mguu wa kulia akiwa ndani ya 18 akimtungua kipa namba moja wa Simba Aishi Manula.
Pasi ya Mayele ilitoka kwa mwamba Farid Mussa kwa mguu wa kulia akiwa nje ya 18. Kwenye mchezo huo zilipigwa pasi tatu mpaka kupatikana bao. Ni Djigui Diarra ambaye ni kipa alipiga pasi ndefu iliyokutana na Farid.
Maamuzi ya Farid ilikuwa ni kumpa Mayele ambaye chaguo lake ilikuwa ni shuti kuelekea upande wa lango la Simba na kuandika bao la mapema lililoipa taji Yanga.
YANGA WALIBEBA TENA

Agosti 13 2022, Simba 1-2 Yanga, Uwanja wa Mkapa ni Simba walipoteza kwa mara ya pili licha ya uongozi mapema katika dakika 15 za mwanzo za mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa.
Ni Pape Sakho alitangulia kufunga bao la utangulizi dakika ya 15 akiwa ndani ya 18 kwa mguu wa kulia akitumia pasi ya mguu wa kulia ya Clatous Chama ambaye alikuwa nje ya 18.
Aziz Ki alitoa pasi kwa Mayele dakika ya 49 alifunga bao la usawa akitumia mguu wake wa kushoto akiwa ndani ya 18 na mtoa pasi naye alitumia mguu wa kushoto ila alikuwa nje ya 18.
Bao la ushindi kwa Yanga lilifungwa na Mayele ilikuwa dakika ya 80 kwa mguu wa kushoto akiwa nje ya 18 alitumia pasi ya beki Dickson Job aliyetoa kwa mguu wa kulia akiwa nje ya 18. Mwisho taji lilikwenda Jangwani langoni mwa Simba alikuwa ni Beno Kakolanya.
MKWAKWANI TANGA
Agosti 13 2023. Kwa mara ya kwanza mtindo wa fainali ulianza kutumika kwa timu ambazo zinamaliza nne bora kucheza fainali. Katika mchezo huu wa fainali ilikuwa ni Tanga. Mshindi alipatikana kwa penalti ilikuwa ni Simba.
Simba walipata penalti 3-1 Yanga ambapo langoni alianza Ally Salim kwa upande wa Simba na kwa upande wa Yanga ni Djigui Diarra ambaye alikuwa kwenye majukumu yake uwanjani.

