AFCON 2027: Hizi hapa timu 9 ambazo zimefuzu, Tanzania, Morocco, Senegal kimeeleweka

ByJoel Thomas

November 23, 2026
AFCON ----AFCON ----AFCON ----

AFCON 2027: Hizi hapa timu 9 ambazo zimefuzu, Tanzania, Morocco, Senegal kimeeleweka

  • Joto la mashindano ya Kombe la Mataifa Afrika (AFCON 2027), linazidi kupanda.
  • Ikumbukwe kuwa mashindano haya yanatarajiwa kuandaliwa kwa mashirikiano ya mataifa matatu ya Tanzania, Kenya na Uganda.
  • Mashindano haya kwa sasa yameingia katika hatua ya mechi za kusaka tiketi ya kufuzu yaani Qualifying Stage.
  • Mpaka sasa tayari timu 9 zimefanikiwa kukata tiketi ya kushiriki na Makala hii inachambua safari zao za kufuzu.

Kuelekea mashindano ya Kombe la Mataifa Afrika AFCON 2027, Joto la mashindano hayo sasa limezidi kuwa juu. Mashindano haya yanatarajiwa kuandaliwa kwa mashirikiano ya mataifa matatu ya Tanzania, Kenya na Uganda. Mashindano haya kwa sasa yameingia katika hatua ya mechi za kusaka tiketi ya kufuzu yaani Qualifying Stage. Mpaka sasa tayari timu 9 zimefanikiwa kukata tiketi ya kushiriki na Makala hii inachambua kwa ufupi safari zao za kufuzu.

Je, hujashinda pesa? Cheza ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa

Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

Tottenham Hotspur

AFCON 2027 timu 9 hizi zimefuzu moja kwa moja

AFCON ---- Timu zilizofuzu
AFCON 2027 Timu zilizofuzu

Mpaka sasa timu zimefanikiwa kufuzu mashindano haya yatakayofanyika mwakani, ambapo zimefuzu katika namna mbili. Kundi la kwanza linahusisha timu za mataifa 3 ambayo yamefuzu moja kwamoja, hizi ni zile timu waandaaji ambazo ni; Tanzania, Kenya na Uganda. Kundi la pili ni la timu 6 ambalo linahusisha timu ambazo zimekusanya pointi nyingi zaidi ambazo haziwezi kufikiwa na timu nyingine ambazo wako nazo kundi moja. Ikumbukwe ili kufuzu timu zinahitajika kumaliza kwenye nafasi za juu, (Nafasi ya 1 na ya 2), kwenye makundi yao.

Kundi la kwanza timu 3 waandaaji wa pamoja

Tanzania

Tanzania National Football Team
Tanzania National Football Team current squad

Wanajulikana zaidi kama Taifa Stars. Tanzania imefuzu kushiriki michuano hiyo kutokana na kuwa miongoni mwa nchi tatu zitakazoandaa mashindano hayo. Mpaka sasa Tanzania imetangaza kuwa wanatarajia kuwa na viwanja vitatu vikubwa vitakavyotumika ambavyo ni Uwanja wa Benjamin Mkapa, Uwanja wa Amaan na Uwanja wa Arusha.

Kenya

Wanafahamika zaidi kama Harambee Stars. Kama ilivyo kwa Tanzania, Kenya nao wamekata tiketi ya ushiriki kwa kuwa timu mwenyeji. Kenya wao wanatarajiwa kuwa na viwanja viwili ambavyo vitatumika kwenye AFCON ambavyo ni; Raila Odinga International Stadium, ambao unajulikana kama Talanta Sports Stadium, na Uwanja wa Moi International Sports Centre maarufu Uwanja wa Kasarani.

Uganda

Uganda Cranes nayo imejihakikishia nafasi ya kushiriki kutokana na kuwa mwenyeji mwenza. Kama ilivyo Kenya, Uganda nao wanatarajiwa kuwa na viwanja viwili ambavyo ni; Mandela National Stadium uliopo Kampala na Hoima City Stadium uliopo Hoima.

Kundi la 2 timu 6 zilizofuzu kwa kukusanya pointi nyingi

Kikosi cha Senegal (-)
Kikosi cha Senegal (-)

Mataifa 6 yamejihakikishia nafasi ya kufuzu baada ya kukamilika kwa michezo minne ya awali ya hatua ya kufuzu, iliyohitimishwa Novemba 17, 2026. Mataifa haya 6 yataungana na wenyeji watatu ambao wamepata nafasi moja kwa moja.Mataifa hayo 6 yaliyosalia ni; Morocco, Senegal, Cameroon, Mali, Burkina Faso na Benin. Ataifa haya yamefuzu baada ya kila timu kukusanya angalau pointi 10.

Hitimisho

Baada ya kukamilika kwa timu 9 ambazo zimefanikiwa kufuzu AFCON 2027, zimesalia nafasi 15 tu ambazo zitapiganiwa na timu zilizosalia. Hii itafanya jumla ya timu 24 kupata nafasi ya kufuzu mashindano hayo. Baadhi ya mataifa makubwa ya soka barani Afrika ambayo bado yanapigania nafasi ni pamoja na Nigeria, Misri, Ivory Coast, Ghana, Algeria, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DR Congo) na Afrika Kusini.

Share this:

ByJoel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.