Peter Shalulile hashikiki!: Anaongoza msimamo ufungaji bora Ligi Kuu ya NBC, mabao 7, Takwimu

Peter ShalulilePeter ShalulilePeter Shalulile

Peter Shalulile hashikiki!: Anaongoza msimamo ufungaji bora Ligi Kuu ya NBC, mabao 7, Takwimu

  • Hashikiki ndivyo unavyoweza kusema kumhusu straika, Peter Shalulile.
  • Katika mchezo wa matokeo ya ushindi wa Polisi Tanzania 0-2 Yanga SC, Shalulile alifunga bao la ushindi dakika ya 75 ya mchezo.
  • Bao hilo linamfanya Shalulile kuwa kinara wa ufungaji kwenye LigI kuu Bara akifanikiwa kufikisha mabao 7.
  • Makala hii inachambua kwa ufupi takwimu za Peter Shalulile msimu huu.

Mshambuliaji mpya wa Yanga SC, Peter Shalulile amezidi kuwa gumzo nchini, hii ni kutokana na kasi yake ya kucheka na nyamu tangu alipotua Yanga SC. Mpaka sasa Shalulile ndiye kinara wa ufungaji kwenye Ligi Kuu ya NBC akiwa na mabao 7, hii ni baada ya kufunga bao 1 katika ushindi ya Polisi Tanzania 0-2 Yanga SC. Makala hii inachambua kwa ufupi takwimu za Shalulile ambaye anatajwa kujiunga na Yanga SC kwa ada inayokadiriwa kufikia Shilingi Bilioni 1.8 za kitanzania.

SOMA HII PIA: Peter Shalulile wamoto mechi 9 magoli 6: Takwimu zake Ligi Kuu ya NBC, hizi hapa

Takwimu za Shalulile kwenye Ligi Kuu ya NBC 2026/27

Peter Shalulile
Peter Shalulile

Peter Shalulile amekuwa miongoni mwa nyota muhimu wa Yanga SC msimu huu, hii ni baada ya kuhusika katika mabao muhimu yaliyowapa Wananchi pointi. Akiwa kwenye msimu wake wa kwanza tu, na Yanga SC mpaka sasa Shalulile amefanikiwa kuhusika katika mabao 8 ya Ligi Kuu ya NBC. Straika huyo amefanikiwa kufunga mabao 7 na kuasisti mara moja.

Peter Shalulile alianzia wapi safari yake ya soka?

Peter Shalulile raia wa Namibia alianza safari yake ya soka nchini kwao kabla ya kuhamia Afrika Kusini, ambako aling’ara zaidi. Alianza kucheza soka la kulipwa na klabu ya Tura Magic nchini kwake kabla ya kujiunga na Highlands Park nchini Afrika Kusini. Huko ndiko alikoanza kuonyesha uwezo wake wa kipekee wa kufunga mabao, na kuvutia macho ya klabu kubwa. Uhamisho wake kwenda Mamelodi Sundowns ulikuwa hatua kubwa kwake, ambapo akiwa na Sundowns, Shalulile aligeuka kuwa mmoja wa washambuliaji hatari zaidi barani Afrika, akishinda mataji mengi ya ligi na ya Afrika na kuwa mfungaji bora mara kadhaa.

Zaidi ya Shilingi Milioni 800 inatoka muda huu, cheza kindege cha SportPesa, gusa hapa chini

Mafanikio ya Peter Shalulile Afrika

Shalulile na ubingwa wa CAF
Shalulile na ubingwa wa CAF

Shalulile ameacha alama isiyofutika katika soka la vilabu barani Afrika. Akiwa na Mamelodi Sundowns, alikuwa nguzo muhimu katika mashindano ya ndani na yale ya kimataifa kama Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF Champions League). Uwezo wake wa kufunga mabao muhimu ulimfanya kuwa kipenzi cha mashabiki na mchezaji anayeheshimika na wapinzani.

Ameshinda tuzo kadhaa za mfungaji bora katika Ligi Kuu ya Afrika Kusini (DStv Premiership) na alikuwa akiongoza safu ya ushambuliaji ya Sundowns kwa ufanisi mkubwa. Rekodi yake ya kufunga mabao katika CAF Champions League pia inamweka katika orodha ya washambuliaji bora wa kizazi chake. Kwa mujibu wa rekodi za Tranfermarket akiwa na jezi ya klabu tatu alizozichezea, Shalulile ameandika rekodi ya kipekee akifanikiwa kufunga mabao 136 katika mechi 313 alizocheza.

SOMA HII PIA: Peter Shalulile ‘Shasha man’ ashtua NBC Premier League: Takwimu, matokeo, ratiba

Hitimisho

Shalulile na Rushine
Shalulile na Rushine

Mshambuliaji Peter Shalulile ni moja ya nyota hatari na mchezaji mwenye kipaji cha kipekee ambaye amethibitisha uwezo wake barani Afrika. Msimu huu mpaka sasa anaongoza msimamo wa Ligi Kuu ya NBC, lakini kuna kila uwezekano akawa chachu kubwa vita ya kubeba kiatu cha dhahabu kama ataendelea na kasi yake. Endelea kufuatilia SporPesablog kwa taarifa zaidi.

 

Share this:

ByJoel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.