Wakali wa Penati Ligi Kuu ya NBC 2026/27: Rushine, Sopu, Chirwa, Anuary kwenye vita kali, Takwimu, live score.

Simba SCRushine (-)Rushine (-)

Wakali wa Penati Ligi Kuu ya NBC 2026/27: Rushine, Sopu, Chirwa, Anuary kwenye vita kali, Takwimu, live score.

  • NBC Premier League 2026/27 iko kwenye mapumziko mafupi kupisha ratiba za kimataifa, mpaka sasa rekodi nyingi zimeandikwa ikiwemo wakali wa Penati Ligi Kuu ya NBC.
  • Mpaka sasa nyota wanne ambao ni; Anuary Jabir, Rushine De Reuck, Sopu na Obrey Chirwa wanakabana koo vikali.
  • Penalti hizo zimekuwa msaada mkubwa kwa baadhi ya washambuliaji kuboresha takwimu zao za mabao.
  • Makala hii inachambua kwa ufupi nyota hatari kwa upigaji wa penalty msimu huu.

Msimu wa NBC 2026/27 uko kwenye mapumziko mafupi kupisha ratiba za kimataifa, mpaka sasa rekodi nyingi zimeandikwa ikiwemo wakali wa Penati Ligi Kuu ya NBC. Nyota wanne ambao ni; Anuary Jabir, Rushine De Reuck, Sopu na Obrey Chirwa wanakabana koo vikali katika rekodi za Penati. Penalti hizo zimekuwa msaada mkubwa kwa baadhi ya washambuliaji kuboresha takwimu zao za mabao msimu huu.

SOMA HII PIA: YANGA, SIMBA, SINGIDA BLACK STARS WAKALI KWENYE NYAVU 2024/25

Anuary Jabir (4)

Anuary Jabir
Anuary Jabir

Kwenye msimamo wa wafungaji anakamatia nafasi ya 1 akiwa na mabao 7, kati ya hayo Anuary amefunga mabao manne ya mkwaju wa penati. Amefunga Penati hizo katika mechi za Polisi Tanzania dhidi ya Azam katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha, Polisi Tanzania dhidi ya Pamba Jiji, Mashujaa dhidi ya Polisi katika uwanja wa Lake Tanganyika na Polisi dhidi ya Mbeya City. Hii inamfanya kuwa miongoni mwa nyota hatari linapokuja suala la Penalti.

Shinda mpaka Milioni 800 muda huu, cheza kindege ‘Aviator’ gusa hapa chini

image
Win big with Sportpesa Aviator

Abdul Suleiman ‘Sopu’(3)

Sopu
Sopu

Abdul Suleiman wa Azam ndio anafuatia akifanikiwa kuweka mabao matatu ya mkwaju wa penati nyavuni. Sopu amefanya hivyo katika michezo ya Polisi dhidi ya Azam katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha, Azam dhidi ya Pamba Jiji mchezo uliofanyika Azam Complex Dar es Salaam. Mechi nyinine ni Geita Gold dhidi ya Azam katika uwanja wa Bukombe mkoani Geita.

Obrey Chirwa (3)

Chirwa
Chirwa

Straika Mkongwe wa Zamba, Obrey Chirwa wa Geita Gold amefunga mabao ya penati matatu katika michezo ya Geita Gold dhidi ya Kagera Sugar uwanja wa Bukombe. Geita dhidi ya Azam uwanja huo huo na mchezo wa TRA dhidi ya Geita Gold uliochezwa uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha. Hii imemsaidia kufikisha mabao 5 kwenye chati ya wafungaji bora.

SOMA HII PIA: YANGA WAFOSI DAKIKA 90, PENALTI SIMBA YALETA KILIO, AZAM NGOMA NZITO

Maabad Maabad (2)

Maabad Maabad wa Coastal Union ameweka mikwaju 2 ya penati katika michezo kati ya Coastal na JKT Tanzania uliochezwa uwanja wa Mkwakwani Tanga na Coastal Union dhidi Polisi Tanzania uliochezwa Mkwakwani Tanga. Hii inamfanya kuwa moja ya wachezaji muhimu wa Coastal Union. Mabao yake yameifanya Simba kuvuna pointi muhimu.

Rushine de Reuck

Wakali wa Penati Ligi Kuu ya NBC
Rushine na Libase

Rushine De Reuck wa Simba amefanikiwa kufunga mikwaju ya penati miwili katika michezo ya Singida dhidi ya Simba uwanja wa Airtel mkoani Singida na Simba dhidi ya Namungo katika uwanja wa Uhuru Dar es Salaam. Pamoja na mabao hayo amekuwa na mchango mkubwa wa mabao ya mipira ya kona. Rushine pia anaipa uimara mkubwa safu ya ushambuliaji ya Simba SC.

SOMA HII PIA: Simba SC vs Pamba Jiji FC NBC Premier League Juni 14 2026 |H2H | Wachezaji wakuchungwa | SportPesa Blog

Hitimisho

Huku Ligi ikiwa mapumzikoni rekodi mbalimbali zinaendelea kukusanywa. Wakali wa penati Ligi Kuu ya NBC wamekuwa mhimili muhimu wa timu zao. Endelea kufuatilia SportPesa Blog.

Share this:

ByJoel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.