Michael Carrick kufukuzwa Manchester United! : EPL 2026/27, Lives core, taarifa za timu
- Hali ni tete ndani ya viunga vya Carlington, jijini Manchester, kufuatia taarifa kuwa kocha Michael Carrick kufukuzwa Manchester United wiki hii.
- Taarifa hizi zinakuja wakati timu hiyo ikipitia kipindi kigumu cha kucheza mechi 10 bila ushindi na wakiwa nafasi ya 18 kwenye msimamo wa ligi Kuu England EPL.
- Mabosi na wamiliki wa Manchester United, wanatajwa kuwa kwenye harakati za kusaka kocha mpya, huku kocha Mauricio Pochettino akipewa nafasi kubwa ya kuchukua mikoba.
- Makala hii inachambu akwa ufupi taarifa hizi.
Kwenye viunga vya Carlington, jijini Manchester, hali ni tete kufuatia taarifa kuwa kocha Michael Carrick kufukuzwa Manchester United wiki hii. Hii ni kutokana na timu hiyo kupitia kipindi kigumu cha kucheza mechi 10, bila ushindi na wakiwa nafasi ya 18 kwenye msimamo wa ligi Kuu England EPL. Mabosi na wamiliki wa Manchester United, wanatajwa kuwa kwenye harakati za kusaka kocha mpya, huku kocha Mauricio Pochetino akipewa nafasi kubwa ya kuchukua mikoba.
SOMA HII PIA: Manchester United 4-4 Aston Villa, Premier League 2026/27 | Highlights | SportPesa Blog
Hali ya manchester united chini ya carrick

Chini ya uongozi wa Michael Carrick, Manchester United imekuwa ikipitia kipindi kigumu msimu huu. Timu hiyo inashika nafasi ya 18 kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Uingereza 2026/27, hali inayoashiria mwanzo mbaya wa msimu. Moja ya matokeo yaliyozua maswali mengi ni sare ya mabao 4-4 dhidi ya Aston Villa, ambayo ilionyesha udhaifu wa safu ya ulinzi na kutokuwa na utulivu wa timu kwa ujumla. Matokeo haya yameongeza shinikizo kwa Carrick na benchi lake la ufundi.
Shinda mpaka zaidi ya Shilingi Milioni 800, cheza kindege ‘aviator’ sasa gusa hapa chini

Viongozi wapya na mapendekezo yao

Kulingana na ripoti kutoka BBC Sport na The Guardian, viongozi wapya wa Manchester United, Omar Berrada na Jason Wilcox, wanatarajiwa kutoa mapendekezo yao kwa Sir Jim Ratcliffe na familia ya Glazers. Mapendekezo haya yanatarajiwa kujumuisha suala la mustakabali wa Michael Carrick kufukuzwa Manchester United. Ujio wa viongozi hawa wapya umekosolewa vikali na mashabiki wa Manchester United.
SOMA HII ZAIDI: Manchester United: Ratiba, kikosi, usajili na matarajio msimu wa 2026/27
Majina yanayohusishwa na nafasi ya ukocha

Kukiwa na uvumi wa kufutwa kazi kwa Carrick, majina kadhaa yameanza kuhusishwa na nafasi ya ukocha mkuu wa Manchester United. Miongoni mwa majina hayo ni, Mauricio Pochettino anatajwa kuwa mmoja wa wagombea wenye uwezekano mkubwa. Pochettino ana uzoefu mkubwa wa kufundisha vilabu vikubwa barani Ulaya na anajulikana kwa falsafa yake ya soka ya kushambulia, ambayo inaweza kuwavutia mashabiki wa United wanaotamani kuona timu yao ikirejea kwenye ubora wake.
SOMA HII PIA: Manchester United vs Aston Villa 8/11/2026: EPL 2026/27, Live score, h2h, Lineups, prediction na habari za timu
Hitimisho
Suala la Michael Carrick kufukuzwa Manchester United limeendelea kuteka vichwa vya habari barani Ulaya. Hali ya kutokuwa na uhakika inaendelea kutawala katika viunga vya Old Trafford. Uamuzi wa mwisho kuhusu Michael Carrick utakuwa na athari kubwa kwa mwelekeo wa klabu msimu huu na miaka ijayo. Mashabiki wanatumai kuwa uamuzi wowote utakaofanywa utaleta utulivu na mafanikio kwa timu yao pendwa, endelea kufuatilia SportPesa Blog kwa taarifa zaidi.

