Manchester United vs Aston Villa 8/11/2026: EPL 2026/27, Live score, h2h, Lineups, prediction na habari za timu
- Ligi Kuu England EPL itaendelea tena leo Jumapili 8/11/2026, huku mechi inayosubiriwa kwa hamu ikiwa ni Manchester United vs Aston Villa.
- Mechi hii inatarajiwa kupigwa kwenye Uwanja wa Old Trafford saa moja na nusu jioni kwa saa za Afrika Mashariki, jijini Manchester England.
- Baada ya matokeo ya Manchester United 3-2 AS Roma, kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika Manchester United watatamani kuona wanafufua matumaini yao katika ligi Kuu England.
- Unaweza kufuatilia matokeo ya mchezo huu live kupitia SportPesascore.
Kitawaka kwenye Ligi Kuu England EPL leo Jumapili 8/11/2026, huku mechi inayosubiriwa kwa hamu ikiwa ni Manchester United vs Aston Villa. Mechi hii inatarajiwa kupigwa kwenye Uwanja wa Old Trafford, jijini Manchester England saa 1:30 usiku kwa saa za Afrika Mashariki. Baada ya matokeo ya Manchester United 3-2 AS Roma, kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika Manchester United watatamani kuona wanafufua matumaini yao katika ligi Kuu England.
Weka mkeka wako wa mechi ya Manchester United vs Aston Villa, ushinde kupitia odds kubwa zilizoboreshwa za SportPesa kwa kugusa hapa chini.

Manchester United vs Aston Villa h2h
Historia ya makutano ya timu hizi mbili katika Uwanja wa Old Trafford unawabeba wenyeji. Manchester United imeshinda michezo 13 kati ya 15 iliyopita waliyocheza dhidi ya Aston Villa wakiwa nyumbani. Hata hivyo, historia hiyo inaweza isiwe na maana kubwa sana ukizingatia hali ya sasa ya kikosi cha Carrick.
SOMA HII PIA: Manchester United: Ratiba, kikosi, usajili na matarajio msimu wa 2026/27
Fomu za timu

Licha ya ushindi wao wa katikati ya wiki dhidi ya Roma, Manchester United bado inapitia kipindi kigumu. Ikiwa karibu na eneo la kushuka daraja, huku ikikabiliwa na ongezeko la wachezaji majeruhi na kukosa mfululizo mzuri wa matokeo katika ligi, Mashetani Wekundu wanaonekana kukosa hali ya kujiamini. Wakati huohuo, Carrick bado anatafuta kikosi chake bora cha kuanza nacho, hasa katika eneo la kiungo, ambako mabadiliko ya mara kwa mara ya wachezaji yamekuwa jambo la kawaida. Katika safu ya ulinzi, hali haijawa nzuri pia. Manchester United imeruhusu mabao 15 katika michezo tisa pekee ya ligi, jambo linaloonyesha udhaifu wa ulinzi ambao Aston Villa bila shaka itajaribu kuutumia kupata faida.
Kwa upande wa Aston Villa, licha ya kukaa katikati ya msimamo wa ligi. Kikosi cha Unai Emery kinaingia kwenye mchezo huo kikiwa na mwendelezo mzuri zaidi wa matokeo ya ligi, baada ya kutopoteza mchezo wowote tangu katikati ya Septemba. Hata hivyo, changamoto za safu ya ulinzi hazipo kwa Manchester United pekee, Aston Villa pia imekuwa na matatizo katika eneo hilo, baada ya kuruhusu mabao 13 na kufanikiwa kutoruhusu wapinzani kufunga katika michezo miwili pekee.
Shinda mpaka Milioni 800, cheza sasa kindege ‘Aviator’ ya SportPesa sasa gusa hapa chini

Msimamo

Kikosi cha Michael Carrick, kinaingia katika mchezo huu kikiwa katika nafasi ya 18 kwenye msimamo wa ligi. Aston Villa wao wanakamatia nafasi ya 12 na pointi zao 12 baada ya mechi 9. Kwa kuangalia ubora wa timu zote mbili, hakuna inayoonekana kuwa imara vya kutosha katika safu ya ulinzi, huku zote zikiwa na uwezo mkubwa wa kushambulia na kuleta matatizo kwa wapinzani. Hii inaufanya mchezo huu kuwa wazi.
SOMA HII PIA: Manchester United vs AS Roma: Utangulizi wa Mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya 2026/27
Utabiri wa matokeo over 1.5
Kwa mtazamo wa wahariri mizania ya mchezo huu inatarajia kushuhudia mchezo wenye mabao 2 au zaidi yaani 0ver 1.5. Ikumbukwe kuwa haya si matokeo halisi na wanaobashiri wanapaswa kuchambua mikeka yao vizuri. Kumbuka kubashiri kistaarabu.
Vikosi vinavyotarajiwa
Unatarajiwa kuwa na maadiliko kadhaa ya vikosi vya timu zote mbili. Mabadiliko haya yanaweza kusababishwa na changamoto za majeraha, vifungo na utimamu wa wachezaji. Kwa kiasi kikubwa wanaoonekana kuathirika ni Manchester United. Vikosi tarajiwa ni kama ifuatavyo;
Manchester United

Kipa: Lammens
Walinzi: Yoro, Heaven, Maguire, Dalot
Viungo: Tielemans, Mainoo, Lacey, Fernandes, Cunha
Mshambuliaji: Mbeumo.
Aston Villa
Kipa: Suzuki
Walinzi: Wan-Bissaka, Lindelöf, Torres, Maatsen
Viungo: Kamara, Barkley, Alysson, McGinn, Manzambi
Mshambuliaji: Jackson.
Hitimisho
Manchester United vs Aston Villa sio tu ni ratiba ya mchezo wa Ligi Kuu England EPL, ni vita ya matumaini mapya kwa simu wa ligi 2026/27. Unatarajiwa kuwa mchezo wenye ushindani mkubwa hivyo si mchezo wa kukosa. Endelea kufuatilia SportPesa Blog.

