Anuary Jabir: Mshambuliaji Mtanzania anayemnyima usingizi Peter Shalulile mbio za ufungaji bora Ligi Kuu ya NBC 2026/27

Anuary JabirAnuary JabirAnuary Jabir

Anuary Jabir: Mtanzania anayemnyima usingizi Peter Shalulile mbio za ufungaji bora Ligi Kuu ya NBC 2026/27

  • Vita ya ufungaji bora kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara inazidi kupamba moto, huku jina la straika wa Polisi Tanzania, Anuary Jabir likiwa la moto
  • Anuary Jabir mpaka sasa amefanikiwa kufunga mabao 7 akiongoza msimamo wa chati ya wafungaji akifuatiwa na Peter Shalulile wa Yanga SC mwenye mabao 6.
  • Nafasi ya 3 inashikiliwa na Obrey Chirwa mwenye mabao 5, saw ana Herbert Lukindo wa Namungo.
  • Makala hii inamchambua kwa ufupi kinara wa ufungaji kwenye Ligi Kuu Bara.

Harakati za mbio za ufungaji bora kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara zinazidi kupamba moto, huku jina la straika wa Polisi Tanzania, Anuary Jabir likitajwa kwa ukubwa.  Anuary Jabir anayeichezea Polisi Tanzania mpaka sasa amefanikiwa kufunga mabao 7 akiongoza msimamo wa chati ya wafungaji akifuatiwa na Peter Shalulile wa Yanga SC mwenye mabao 6. Nafasi ya 3 inashikiliwa na Obrey Chirwa mwenye mabao 5, saw ana Herbert Lukindo wa Namungo.

SOMA HII PIA: Orodha ya wafungaji NBC Premier League 2026/27 | Jabir na Peter Shalulile kwenye vita | SportPesa Blog

Anuary Jabir anaongoza mbele ya Peter Shalulile ufungaji bora

Screenshot ---------- ------
Chati ya wafungaji NBC PL 2026/27

Katika msimu wa NBC Premier League 2026/27, Anuary Jabir mpaka sasa anakimbiza tuzo ya kuwa mfungaji bora. Hadi sasa, amefanikiwa kufunga mabao 7, hii inamfanya kuwa kileleni mwa chati ya wafungaji bora wa ligi huku Shalulile wa Yanga SC akisalia nafasi ya 2. Uwezo wake wa kumalizia mipira na kujipanga vizuri ndani ya eneo la hatari umekuwa chachu ya mafanikio yake. Mabao haya yamekuwa muhimu sana kwa Polisi Tanzania FC katika harakati zao za ligi.

Shida mpaka Milioni 800 muda huu, cheza kindege ‘Aviator’ ya SportPesa gusa hapa chini 

image
Win big with Aviator

Takwimu muhimu za Anuary Jabir msimu wa 2026/27

Anuary Jabir
Jabir Anuary

Takwimu za Anuary Jabir zinaonyesha mchango wake mkubwa uwanjani. Kwa mabao 7 aliyofunga, anashika nafasi ya juu kati ya wafungaji bora, akionyesha uthabiti na umakini mbele ya lango. Ufanisi wake wa kufunga mabao umemfanya kuwa tegemeo kubwa kwa kocha wake na mashabiki wa Polisi Tanzania FC. Kila anapokuwa uwanjani, matarajio ya kufunga bao huwa makubwa.

SOMA HII PIA: Polisi Tanzania 2-0 Mbeya City NBC Premier League | Msimamo | Highlights | SportPesa Blog

Mchango wake katika nbc Premier League

Kikosi ch Polisi Tanzania
Kikosi ch Polisi Tanzania

Anuary Jabir sio tu mfungaji wa mabao, bali pia anachangia pakubwa katika uchezaji wa timu yake. Harakati zake uwanjani, uwezo wa kucheza na wenzake, na presha anayoweka kwa mabeki wa timu pinzani, yote yanamfanya kuwa mchezaji kamili. Msimu huu wa 2026/27 umempa fursa ya kuonyesha uwezo wake kamili na kujithibitisha kama mmoja wa washambuliaji hatari zaidi nchini Tanzania. Anuary Jabir anaendelea kuwa mchezaji muhimu wa kutazamwa katika NBC Premier League.

SOMA HII PIA: Polisi Tanzania 2026/27: Ratiba, Matokeo na Msimamo Ligi Kuu Bara

Hitimisho

Kwa kiwango anachokionyesha, Anuary Jabir msimu huu anaweza kuweka rekodi mpya ya kuendelea kuwa mfungaji bora katika ligi. Mashabiki wa soka wanatarajia kuona mengi zaidi kutoka kwake katika mechi zijazo. Endelea kufuatilia SportPesa Blog kwa taarifa zaidi.

Share this:

ByJoel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.